Tajwid somo la 2: herufi saba katikausomaji wa quran

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu herufi saba katika usomaji wa tajwid.

Herufi Saba

Wataalamu wa Tajwid wanaeleza kuhusu herufi saba za usomaji wa Qur'an. Qur'an imeshuka kwa lugha ya Kiarabu, na Waarabu wenyewe walitofautiana katika lahaja za lugha ya Kiarabu. Lahaja hizi zilikuwa za makabila saba ya Kiarabu yaliyopo Makkah. Hii ina maana kuwa Waarabu walikuwa na makabila saba wakati huo, na ingawa walizungumza Kiarabu, walitofautiana katika maneno, utamkaji, na hata uandishi. Lahaja hizi zilijulikana kama herufi saba za usomaji wa Qur'an.

 

Lahaja hizi saba ndizo chanzo cha hizi herufi saba. Hili linathibitika katika maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w) aliposema: "Jibriyl alinisomea kwa herufi moja, nikaifanyia marudio mpaka akanifundisha nyingine, nikaendelea kumuomba nyinginezo mpaka mwishowe zikawa herufi (lahaja) saba" (Bukhari na Ahmad).

Makabila haya yalikuwa Quraysh, Hudhayl, Thaqiyf, Hawaazin, Kinaanah, Tamiym, na Yemen. Hivyo, Qur'an ilishuka katika lahaja saba kulingana na makabila haya, na kila kabila linasoma Qur'an kwa namna ambavyo lahaja yao inawafanya waelewe. Wakawa watu wanaandika Qur'an kwa namna wanavyoelewa wao kulingana na lahaja ya kabila lao. Hali hii ilifanya usomaji wa Qur'an utofautiane. Mifano ni kama ifuatavyo: "‘alayhim" wengine walitamka "‘alayhimuw," neno "swiraatw" walitamka wengine "zwiraatw" na wengine "siraatw," na "muumin" wengine walitamka "muwmin."

 

Amesimulia ‘Umar Ibn Al-Khatab kuwa: “Nilimsikia Hishaam ibn Hakiym akisoma Suratul-Furqan tofauti na vile ninavyoisoma na alivyonifundisha Mtume (s.a.w). Nilikaribia kumsimamisha (asiswalishe) lakini nikamvumilia mpaka akamaliza, kisha nikamshika nguo yake shingoni na kumvuta mpaka kwa Mtume (s.a.w) na kusema: "Nimesikia huyu mtu akisoma (Suratul-Furqan) kinyume na ulivyonifundisha." Mtume (s.a.w) akasema: "Mwachie!" Akamwambia (Hishaam): "Soma." Akasoma. Akasema: "Hivi ndivyo ilivyoteremshwa." Kisha akaniambia mimi: "Soma." Nikasoma. Akasema: "Hivi ndivyo ilivyoteremshwa. Hakika Qur'an imeteremshwa kwa herufi saba, hivyo someni iliyokuwa sahali kwenu."

 

Kuenea kwa Uislamu na Uhitaji wa Msahafu Moja

Uislamu ulipoenea zaidi, ikaonekana haja ya kuiandika Qur'an katika lahaja moja ili kuepuka makosa katika usomaji. Katika utawala wa Uthman (r.a), kikundi cha maswahaba kilichokuwa kikiongozwa na Hudhayfah bin al-Yamaaniy kilikuja kwa Uthman (r.a) na kumsihi "auokoe ummah wa Kiislamu kabla haujatofautiana juu ya Qur'an." Uthman (r.a) akaamrisha chini ya uongozi wa Zayd bin Thaabit (r.a) nakala za Qur'an ziandikwe na nakala zote zisizo rasmi zichomwe moto.

 

Lahaja iliyotumika kuandika Qur'an ilikuwa ile ya Kikuraysh, na msahafu ukajulikana kama 'Msahafu wa Uthman'. Nakala hizo zilisambazwa miji mikuu ya Waislamu kama nuskhah (nakala) rasmi, na nuskhah ya asili ikabakishwa kwa Mama wa Waumini Hafsah (r.a). Zayd bin Thaabit alibaki Madina, 'Abdullah bin Swa’ib alitumwa Makkah, Mughiyrah bin Shu'bah alitumwa Syria, Abu 'Abdur-Rahmaan As-Sulamy alitumwa Kufa, na 'Aamir bin 'Abdil-Qays alitumwa Basra.

 

Baada ya msahafu huu kusambazwa katika dola ya Kiislamu, lahaja zote zisizo rasmi zilipotea. Msahafu huu ndio chimbuko la misahafu tuliyonayo leo. Ingawa kuna tofauti kubwa za kiuandishi kati ya misahafu ya leo na msahafu huu, kwa mfano, msahafu huu haukuwa na nukta kwenye herufi au irabu pia hazikuwepo. Hayo yalifanyika baadaye kadiri Uislamu ulipoenea maeneo mbalimbali ya dunia na ikaonekana ugumu wa kutumia msahafu ule kwa watu wasiokuwa Waarabu.

Mwisho:

Tukutane somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu aina za viraa katika usomaji wa Tajwid

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Darsa za Tajwid Main: Dini File: Download PDF Views 401

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Tajwid somo la 3: aina za viraa katika usomaji wa Quran

Katika somo hili utajifunza kuhusu viraa vya usomaji wa Quran. Viraa hivi ni tofauti na herufi saba

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 13: sheria za Al-ikhfaa

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za Al ikhfaa katika usomaji wa Tajwid

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 12: sheria za Iqlab

Katika somo hili utakwenda kujifunzakuhusu hukumu za iqlab katika usomaji wa tajwid.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 18: hukumu za waqf wal ibtidai

Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu hukumuza waqfu katika usomajiwa quran.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 14: kuhumu za mim sakina

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu hukumu za ki tajwid za mim sakina.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 9: hukumu za nun sakina na tanwin

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za kitajwid za nun sakina na tanwin

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 7: haraka na irabu katika lugha ya kiarabu

Katika somo hili utakwenda kujifunzakuhusu haraka na irabu katika lugha ya kiarabu

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 22: hukumu za sijdat tilawa

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu sijda zinazotokea wakati wa kusoma Quran.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 5: makharija al khuruf

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu makharijal khuruf

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 15: hukumu za qalqala

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za Qalaqala katika usomaji wa tajwid.

Soma Zaidi...