Simulizi za Hadithi EP 6 Part 12: Tabibu asimulia hadithi

Hii ni hadithi iliyopo ndan ya kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA TABIBU:

Tambua ewe Sultani mwadilifu kuwa mimi nimezaliwa katika familia ya wachamungu waabuduji wanaofata mila za kiyahudi. Wazazi wangu wanafuata torati vyema kama inavyofundisha. Nilipokuwa mdogo nilipata kuhifadhi kurasa kadhaa za torati katika moyo wangu. Nilipata kusoma historia za watoto wa Israeli na nikajuwa Habari na maisha yao. Nilipata pia kujifunza historia yao kwenye vitabu vya dini nyingine kama duni ya Kikristo na Kiislamu. Niliweza kujua mitihani waliopewa na Mungu na walivyotatua mitihani hiyo.

 

 

 

Nilijifunza pia tiba zao za kiasili walizokuwa wakitumia toka wakiwa Misri na hata walipokuwa jangwani wakitangatanga kama adhabu waliopwewa na Mungu. Nilivutiwa sana na kuhamasika sana na maisha ya kundi hili la watu. Nikaaza pia kuvutiwa na tiba zao na ndipo nilipojifunza utabibu. Niliweza kujifunza pia mishoro (matarasimu) ya majini na njia walizotumia watu kumiliki majini. Nilitambua kuwa takribani kila jamii zina aina zao za utabibu. Nilianza kuvutiwa kujifunza tabibu za nchi mbalimbali.

 

 

 

Nilihama kutoka Palestina na kuelekea Iraki na kujifunza mengi, nikaelekea India na kujifunza tiba za wahindi na hatimaye nikafika Iraki. Sifa za utabibu wangu hakika zilifika mbali hata tangu ya Sultani aliyepita alikuwa akija kwangu nyakati za usiku wa kiza. Usiku wa manane watu wakiwa wamelala. Ilifika siku moja nililetewa mgonjwa kutoka Damaska naye alikuwa ni wa kiume. Alikuwa akisumbuliwa na majini waliokuwa wameiteka nusu ya akili yake. Kwa malipo mazuri sana tulioahidiana niliweza kukaanaye kwa muda wa wiki 3.

 

 

 

Nilikuwa nikimpa dawa za kunywa na kufukiza. Mpaka nikaanza kuona kuwa ameanza kupata nafuu. Siku ya saba ilibidi nikampake dawa nyingine maeneo yote ya mwili wake, hivyo ilihitajika niende nae bafuni. Nikamueleza avae nguo ya ndani tu na ajifunge saruni. Nikamueleza mke wangu achemshe dawa niliyompa aweke na tangawizi ndani, achanganye na mafuta ya miski nyekundu pamoja na mafuta ya kunazi. Nikampa na dawa nyingine pia. Maji yalipoanza kupata umoto na kuchemka kwa mara ya kwanza nikamweleza ategue. Mke wangu akapeleka maji bafuni.

 

 

 

Nikamweleza mgonjwa awahi kwenda bafuni na atangulize mguu wa kushoto na nikamweleza maneno ambayo ayaseme alopokuwa akiingia chooni “Ewe Mwenyezi Mungu, Mimi najikinga kwako na Majini wa Kike na wa kiume (wanaopatikana chooni)”. na mimi nikatamfatilia. Nikaanza kumuogesha na kumpata dawa katika maeneo nilioyataka. Nilistaajabu sana kuona mgonjwa amekata mkono wake wa kushoto kwenye kiganja chako. Nilijizuia juu ya kumuuliza sababu ya kukatwa kwa mkono wake. Alinigundua kuwa ninataka kumuuliza ila nashindwa.

 

 

 

Baada ya kumaliza shughuli yetu nilitoka nikiwa na mawazo kichwani. Nilitambua kuwa kwa mujibu wa sheria za Waislamu Mwizi ndiye anayekatwa mkono. Nilianza kujiuliza je huyu mgonjwa nilieletwa ni mwizi/ ama amekatwa kiganja chake kwa ukorofi wake. Nikiwa katika dimbwi la mawazo ghafla mgonjwa wangua akaja na kuniuliza Je! Ungetaka kujuwa chochote kuhusu mkono wangu?. nikamjibu Ndio ewe kijana, tafadhali ridhisha masikio yangu juu ya habari iliyofishika katika kiganja chako. Hao akaanza kuhadithia kama ifuatavyo:-

 

 

 

Baba yangu alikuwa ni mtu masikini sana katika baadhi ya miji ya Misri. Alikuwa na kaka zake 6 na kaka zake hawakubahatika kuwa na watoto. Baba yangu hakubahatika kuwa na watoto wengi hivyo ni mimi tu ndiye niliyekuwa mtoto kwake na wa pekee. Baba yangu aliminyana saba kuweza kujikwamua katika umasikini bila hata na mafanikio. Alifikiri lamda umasikini ndio ilikuwa hatima yake ama ndivyo alivyopangiwa.

 

 

 

Tofauti na kuwa baba yangu alikuwa ni mtu masikini alkini alitambulika kwa ucheshi wake na ukarimu. Alipenda sana kusaidia watu anaowajua na asiowajua. Alipenda sana kusaidia wageni na wasiojiweza kwa hali yoyote awezayo. Watu waliamini kuwa ndio maana baba yangu haendelei ni kwa sababu amezidisha ukaribu. Lakini yaye katu hakuwasikiliza watu hawa. Baba aliamini ipo siku Mungu anaweza kumfanya tajiri bila hata kujuwa.

 

 

 

Baba yangu alikuwa ni Mfanyaibada anayefata dini ya Kiyahudi na alikuwa akisoma sana torati. Aliamini kuwa ukarimu na tabia njema ndiyo iliyokuwa sifa ya Mitume kama Mtume Abraham (Ibrahimu), Mtume Musa na Mtume Haruna. Hali ya umasikini katika familia yetu iliendelea hata mimi nikawa mkubwa katika hali ile ile. Ijapokuwa hatukuwa na kipato lakini nyumba yetu ilikuwa na furaha sana, tuliweza kuishi na baadhi ya ndugu zetu pale nyumbani. Wakati mwingine amani na furaha ni bora kuliko utajiri na mapesa, na hivi ndivyo familia yetu ilivyokuwa.

 

 

 

Umasikini wetu uliendelea hata nilipofikia umri wa miaka 12, na hapo ndipo mambo yalipoanza kubadilika. Hali ya kiuchimi nyumbani kwetu ilibadilika ghafla ndani ya masaa machache tu ya masiku. Yote haya yalitokea pale walipokuja wageni wa ajabu. Wageni wenye mashaka na hali zao. Wageni hawa waliweza kubadili maisha yetu na hadhi yetu katika jamii. Habari nzima ilikuwa hivi:-

 

 

 

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Mankaa image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Burudani File: Download PDF Views 338

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 6: Sehemu ya tatu ya safari ya Sinbad

Muendelezo wa sehemu ya tatu ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Mtumwa wa mfalme na mawaziri

Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha tatu.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 11: Vidole gumba vilikatwa

Kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA kina simulizi nyingi nzuri na za kusisimua, muendelezo....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 15: Mji uliogeuzwa mawe

Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 17: Ufupisho wa ALIFU LELA U LELA KITABU CHA KWANZA

Huu ni ufupisho mfupi kuhusiana na kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA...

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 8: Hadithi ya kisiwa cha uokozi

Simulizi hii ipo ndani ya kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 4: Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu.

Hadithi za HALIF LELA U LELA hii ni moja wapo imetoka katika kitabu cha kwanza imaelezea kisa cha mzee wa tatu....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 7: Mjakazi wa sultani

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili .....

Soma Zaidi...