picha

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 2: Sehemu ya safari ya kwanza ya sinbad

Muendelezo wa stori ya safari ya Sinbad ambayo ipo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

SAFARI YA KWANZA YA SINBAD

 

Tambua kuwa baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana katika nchi ya baghdad wakati wa utawala wa sultan harun Rashid. Baba yangu alifariki miaka 21 iliyopita nilipokuwa kijana kama wewe. Wakati huo nilikuwa na marafiki wengi sana. Na nilianza kutumia mali aloniachia baba na hatimaye akakaribia kuisha na marafiki wakanikimbia. Na hapo ndipo nilipoamua kuanza biashara za majini, yaani kuuza bidhaa sehemu mbalimbali za visiwa.

 

Nilijiandaa vizuri kwa ajili ya safari yangu ya kwanza. Na maandaliizi yalipokuwa tayari tulianza safari ya kubiashara. Safari ilikuwa salama kabisa kwa muda wa masiku. Tulipita visiwa kadhaa tukiuza na kununua. Kwa upande wangu biashara haikuwa mbaya ijapokuwa ugeni ulinisumbuwa sana. Kwa ujumla nilifurahia safari ile. Baada ya kutembea visiwa kadhaa tuliamua kumalizia katika viziwa vingine ili tuweze kurudi nyumbani. Ilitikea sikumoja ghafla upepo ulianza kubadilika na jahazi likashindika na kudhibitiwa na manahodha.

 

Upepo ulizidi mpaka nahodha akaamua kukiachia chombo kiende kokote, hali iliendelea kuwa mbaya mpaka bidhaa zikaanza kutumbukizwa majini ilikuokoa ualama wa maisha. Haliiliendelea kuwa mbaya hata chombo kikaanza kunywa maji. Watu wakaanza kuania rohozao, na kuanza kushika mbao zilizovunjika kutoka kwenye jahazi. Mimi nilipata mbao moja na ilinipeleka mbali zaidi ambapo sikuweza kuona hali za wenzangu kilicho endelea.

 

Kwa upande wangu mawimbi ya maji yalinipeleka mbali sana, nikiwa nimeshikilia tawi lile hata sikusubutu kuliachilia. Nilipofika hali ambapo sijielewi kwa kuchoka ghafla nikaona kunaweupe mbele yangu, kuangalia vizuri kilikuwa ni kijisiwa kidogo. Basi nikajitahidi kujizuia huku nikawa naiba maji ili yanipeleke kule. Kwa bahati njema kaupepo kakanipeleka kwenye kisiwa kile. Kwa msaada wa mizizi ya miti niliweza kutoka kwenye maji yale.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Mankaa image Tarehe: 2024-09-10 09:27:35 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Views 858

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP4  Part 5: Hadithi ya pili ya mtoto chongo wa mfalme

Hadithi za HALIF LELA U LELA huwa zina muendelezo na hadidhi hii ni muondelezo wa kisa cha pili cha mtoto chongo wa mfamle ambayo imetoka ndani ya kitabu cha kwanza cha Hadithi za HALIF LELA U LELA.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 9: Hadithi ya deni la mapenzi

Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 1: Hadithi ya chongo watatu, watoto wa mfalme na wanawake wa Baghdad.

Skmulizii hii pia imetoka kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza

Soma Zaidi...