Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 13: Wageni wa Baraka kujongea

Muendelezo.....

UJIO WA WAGENI WA BARAKA.

Kama nilivyokueleza kuwa baba alikuwa ni mchamungu na mpendwa na watu. Alikuwa akisaidia anaowajuwa na asiowajuwa, wageni na wenyeji. Basi sikumoja walikuwa wageni wakitokea nchi za Uarabuni huko Yemeni. Wageni wale walikuja Misri na kukutana na baba. Hakuwa akiwafahamu wala hawakuwa wakimjuwa. Walipokuja walianza kutafuta nyumba za wageni lakini hawakufanikiwa kupata vyumba. Jumla walikuwa ni watu watatu. Vijana wawili wenye maumbo ya kawaida na mzee mmoja wa makamo, aliyekuwa na ndevu nyeupe zilizolala vyema.

 

 

 

Umri wa vijana hawa naweza kuufananisha kati ya miaka 20 hadi 25. hawakuwa wenye ndevu nyingi ndio sasa masharubu yalikuwa yakionekana kama kipara ninachoota nywele. Wageni walipokutana na baba baada ya kuelekezwa na watu wakaomba hifadha. Walitaka kufadhiliwa kwa muda wa masiku 7 tu. Walikuja kutafuta mali ili wakauze nchini kwao. Basi baba akawaruhusu kwa sharti kuwa hawatasababisha uharibifu wowote ndani ya mji wala katika mali za wananchi zilizopo mjini ama mashambani.

 

 

 

Baada ya makubaliano baba aliwapa karatasi wasaidi na iwe ni kumbukumbu. Pia wageni wakaongeza kwa kusema kuwa sisi tutakuwa tukiwinda na kuvua. Kwa kila tutakachokipata wewe tutakupatia kichwa. Sharti hili lilionekana la utata sana lakini baba alikubwali. Maana ya sharti hili ni kuwa wakivua samaki baba atapewa vichwa vya samaki, na wakiwinda mnyama baba atapewa kichwa. Baba aliweka saini na akaichukuwa karatasi na kuipeleka kwa kadhi wa mji naye akaweka saidi na kuihifadhi.

 

 

 

Wageni waliweza kulala nyumbani kwa siku tatu bila hata ya kufanya kazi yeyote na hata kutoka nje. Tulipokuwa tukiwapelekea chakula walisema wanachochakula chao na wakatuonyesha nyama kavu iliyokaushwa. Tulipowapelekea maji ya kunywa wakasema wanamaji yao na wakatuonyesha viriba vya ngozi, wakidai ndimo wamehifadhi maji yao. Watu wa mtaani hawakuweza kuwajuwa wageni wetu japo walisikia kuwa baba amepokea wageni.

 

 

 

Wasichana wa mtaani walikuwa wakija myumbani wakidai kuomba chumvi mara sukari mara moto ilimradi waone sura za wageni wetu, ila bila ya mafanikio hawakupata chochote. Siku ya nne baada ya alfajiri kuisha wageni walimfata baba na kumuomba akawaonyeshe sehemu mto ulipo. Wakamwambia awaelekeze kwenye matope ambapo samaki aina ya kambale wanapatikana.

 

 

 

Baba akawaelekeza sehemu karibia na maporomoko ya maji yalipo ambapo kuna dimbwi mbele lina matope mengi na maji machache sana. Hapo kuna kambale wengi wanaojificha kwenye matope. Wale mabwana wakachukuwa kipande cha shuka waliopewa wajifunike kisha wakashika wawili kila mmoja kashika upande mmoja. Kisha yule mzee akaingia kati na kuanza kushakia samaki waende kwenye ile chuka.

 

 

 

Kitu cha ajabu walipokuwa wakivua samaki tofauti na kambale walikuwa wakimwacha. Na wanapovua kambale mdogo walikuwa wakimwacha na wakisema “Mwenyezi Mung ampe umri mrefu samaki huyu”. hapa nikagundua kuwa hawa ni wachamungu sana. Lakini sikujua sababu ya yale waliokuwa wakiyafanya. Basi walipotimiza idadi ya kambale 11 wakaondoka. Kisha wakasema “Asiyeshukuru kidogo hata akipewa kingi hawezi kushukuru”.

 

 

 

Walikusanyika sehemu moja na kunza kuosha samaki wale kisha mkubwa wao akasema “wala hatabeba mtu kubeba mzigo wa mwengine” baba akiwa akiwaangalia vyema yule mdogo kuliko wote akachukuwa kishu na kuanza kukata vichwa vya samaki wale. Akisha anayefata kwa ukubwa akaanza kupasua matumbo ya samaki wale na kuyaweka kwenye mfuko. Kisha akarudia kauli ile “ asiyeshukuru kwa kidogo hata kwa kingi hatashukuru kisha wakamkabidhi baba mfuko wa vichwa vya samaki”. Wakamueleza kuwa vichwa vyote kula ila hiki kihifadhi mpaka siku ya miadi yetu” wakamuonyesha kichwa hicho na kumueleza “hakupata hasara mwenye kusubiri n akufata maelekezo”

 

 

 

Alistaajabishwa sana na watu hawa. Hawakuwa watu wa maneno mengi wala kupiga stori. Vitendo vyao vilikuwa ndio maneno yao. Na walizungumza maneno machache ambayo ni mistari kutoka kwenye vitabu vya dini Alivyowahi kusomaga. Akafata maelekezo na kuondoka na wageni wake. Alipofika nyumbani akamkabidhi mama vichwa vile na akamueleza apike supu. Kisha kichwa kile akaenda kukihifadhi sehemu salama.

 

 

 

 

Asubuhi ya siku ya pili wageni hawakwenda kuvua ila mmoja kati yao akatoka na kuchukuwa ule utumbo wa kambale akaenda kwenye uwanja wa michezo. Wakati hue wenzake wawili wakaanza kukausha samaki wale nyuma ya nyumbni kwetu kwa ndani. Walikuwa na jiko lao na mafuta yao ya kuwashia moto. Hawakuhitaji kitu chochote. Kama kawaida hawakuwa na maneno mengi na maneno yao machache yalikuwa ni mistari kutoka vitabuni. Nikaelekea uwanjani nikaone anachofanya yule mwenzao mwengine.

 

 

 

Alikaa katikati ya uwanja na kuanza kupiga winja wa ajabu sana. Katu sijapatapo kusikia winja kama huo. Sikujuwa hasa ni ni anakusudia. Haukupita muda wakaja kunguru na ndege wengine wa porini pamoja na mabata maji. Alianza kutoa utumbo wa samaki waliovua jana na kuanza kuwapa wale ndege. Nikiwa naangalia kwa ukaribu nini kinaendelea, nikashhudia anatoa kisu chake. Wale ndege walikuwa ni kama wake waliweza kumsogelea sana. Alizungumza maneono kadhaa sikupata kuyasikia maana nilikuwa mbali.

 

 

 

Basi akamkamata kunguru mmoja na kumchinja kisha akakamata bata maji na kulichinja. Kisha akamaliza utumbo alio nao na kurudi nyumbani. Alimpatia baba kichwa cha kunguru na kumueleza akihifadhi mpaka siku na miadi na kile cha bata maji akamueleza akitumie kwa chakula. Sikuweza kujuwa kabisa maana ya haya mambo waliokuwa wakiyafanya. Wana siku tano sasa. Wamebakiwa na siku mbili. Walisema kuwa siku ya saba ndiyo wataondoka mapema asubuhi hivyo wamebakiwa na siku moja tu.

 

 

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:12:00 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 137


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 7: Mjakazi wa sultani
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili ..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 1: Hadithi ya chongo watatu, watoto wa mfalme na wanawake wa Baghdad.
Skmulizii hii pia imetoka kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 6: Hadithi ya mwenye kutabiriwa mtoto wa tajiri
Tunapfatilia simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizi hii imetoka ndani ya kitabu cha kwanza karibuni tuendelea kupata skmulizi nyingi za kusisimua ..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 8 Part 2: Siri ya kifo
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 5: Nani ni binti?
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 1: Muuaji ni nani?
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 3: Simulizi ya kuingia kwa wageni
Simulizii hii ya kuwasili kwa wageni inapatikana ndani kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... moja kwa moja tusikilize kisa hichi.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini na mtumwa
Muendelezo....... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 14: Wageni
Simulizii hii ni nzuri na ni mojawapo ya hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Bostani la kifalme baghadad
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 10: Mapenzi kwenye mtihani
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 16: Hadithi ya safari ya saba ya Sinbad
Muendelezo wa safari ya Sinbad....... Soma Zaidi...