Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP4  Part 5: Hadithi ya pili ya mtoto chongo wa mfalme

Hadithi za HALIF LELA U LELA huwa zina muendelezo na hadidhi hii ni muondelezo wa kisa cha pili cha mtoto chongo wa mfamle ambayo imetoka ndani ya kitabu cha kwanza cha Hadithi za HALIF LELA U LELA.....

HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME.

 

Kwanza utambuwe kuwa mimi nimekuwa chongo si kwa sababu ya ajali ama bahatimbaya kama iliyompata mwenzangu huyu. Mimi ni kwa sababu ya ujeuri wangu wa kutaka kujuwa mambo yasiyo nihusu. Hadithi yangu ni hii:-

 

Kama nilivyotangulia kusema mimi ni mtoto wa mfalme na ni wa kipekee katika uzawa na baba yangu akanichagulia jina la Agib. Baba yangu alinipa taaluma nyingi sana. Ila kwa upand wangu nilipenda kuwa mfanya biashara. Hivyo nilikuwa nikisafiri kwa kufanya biashara maeneo mengi ya dinia. Tulikuwa tukiuza vitu mabalimbali. Kwa ufupi nilikuwa nimejaaliwa kwa kuwa na nuru ya biashara. Nilikuwa nikiuza sana na kupata faida nzuri.

 

Siku moja tulikuwa tumetoka kibiashara kwa njia ya majini. Nahodha alikuwa mjuzi sana wa safari hizi na safari yetu ilikuwa nzuri sana. Tulifanya biahsra katika visiwa kadhaa na kuelekea upande wa kusini kutoka kisiwa tulichotoka. Upepo ulikuwa mzuri kwa muda wa siku nzima. Hali ilibadilika pale ilipofika asubuhi. Upepo ulikuwa mbaya sana na chombo kilikuwa ninakwenda uelekeo usiojulikana. Nahodha na wenzie walijitahidi kutuwa nanga lakini kamba ilikuwa fupi. Basi wakakiachia chombo kiende tu.

 

Ilipofika asubuhi nyingine tupepo ulitulia na tukaona mbele kuna mlima uliotanda kiza kinene sana. Nahodha alipoulizwa alisema hana ujuzi na eneo hilo lakini anachoweza kusema ni kuwa mlima uliopo mbele yetu ni mlaima wa sumaku hivyo misumari yote iliyopo kwenye chombo chetu itatoka na kuvutwa kwenye mlima. Hivyo nahodha akatutaka kila mmoja ajiandae na ajali hiyo.

 

Mambo yalikuwa hivyo hivyo baada ya muda kadhaa misukari ikaanza kung’oka na kwenda kunata kwenye mlima. Jabir tukaanza kung’ang’ania mbao. Kwa upande wangu mbao nilioipata ilikuwa ni madhubuti hivyo niliogelea naye kwa muda wa siku kadhaa. Mapaka siku ya 5 nikaona kuna kisiwa kidogo. Nikajitahidi nai kufika pale nikaona kuna mti wa mpera nikafika hini pale na kuanza kula mapera.

 

Nilikaa pale kwenye mti ule kwa muda mpaka nikapitiwa na usingizi. Nilipoamka nikaona kuna msafara mkubwa sana unakuja kuelekea pale nilipo. Nikapanda juu ya mpera ule na kujificha pale. Msafara ule ukaja mpaka pembeni kidogo ya mpera ule kwa futi 50 wakachimba chini na kufungua mlango pale chini na msafara wote ukaingia pale. Baada ya muda wa masaa kama matatu walitoka wote kasoro mtu mmoja tu ndiye aliyebaki mule ndani.

 

Walipoondoka nilisubiri kama masaa 2 nikafungua pale na kuingia ndani. Nilipofika nikamkuta kijana wa umri wa miaka 10 ivi. Nikamsalimu na kumuuliza kilichomsibu hata wenzake wakamuacha mulendani. Akaanza kunieleza stori yake kama ifuatavyo;-.....

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-09 14:04:10 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 89


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 9: Hadithi ya binti wa mfalme kufichwa.
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 8: Harusi ya aladini kufanyika na binti wa mfalme
Muendelezo...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 7: Mjakazi wa sultani
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili ..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 2: Sultani mtoa buradani kufariki
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 10: Ndoa ya binti mfalme na Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 4: Sehemu ya pili ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP7  Part 17: Jaribio la tatu kwa Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 9: Hadithi ya deni la mapenzi
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 19: Mfalme na waziri wake
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 6: Ndoa ya pili
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 3: Kisa cha mke na kasuku
Simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizii hii inasimulia kisa cha mke na Kahuku wake.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 17: Hadithi ya Malipo ya wema ni wema
Mwendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...