image

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini na mtumwa

Muendelezo.......

NURDINI AMLAGHAI MTUMWA.

 

 

 

 

 

Siku ya tano Nurdini alipata taarifa kutoka kwa watu wake yaani wafanyakazi wa chumba chake kuwa kuna binti mgeni ameletwa ila ametengewa sehemu yake maalumu. Na kuna walinzi wa kike hivyo haruhusiwi mwanaume yeyote kwenda hasahasa nurdini. Nurdini alitabasamu kusikia hivyo. Tabasamu lililowaacha wafanyakazi wa chumba chake mioyo yao kuwaenda mbio. hakikaNurdini alikuwa ni kijana mzuri. Sharubu zake fupi zilizokuwa zikichomoza kama mbegu za mpunga zinazoota sasa, pua iliuotokeza kwa mbele kidogo, mashavu yaliyojaza na kutengeneza uso usio duara kama wanawake wa nchi za Balkan.

 

 

 

 

 

Siku hiyo Nurdini hakuamua ubaya ila alitamani kwenda kumuona huyo mtumwa japo kwasiri. Alipenda kujiridhisha macho yake kama huyo mtumwa ni kiwango cha kuweza kuchukuliwa na mfalme kama ilivyokusudiwa na baba yake. Siku hiyo mtumwa alikwenda kuoga, Nurdin alitumia fursa hiyo kuingia chumbani kwa binti kisha akajificha nyuma ya pazia. Alipomaliza kuoga binti akaingia ndani, hapo Nurdini akajifanya anamtafuta mama yake. Wakati anaulizia yule binti akapatapo kusikia sautti ya kijana Nurdini, na hapo nafsi yake ikaingia udadisi kutaka kujuwa hasa kama sauti ya kijana huo imemridhisha kiasi kile vipi sura yake.

 

 

 

 

 

Binti akatoka kwenda varandani kumuona kijana aliyekuwa akimuuliza mama yake, Loo akakutana na sura nzuri. Hapo alitamani hata kumkumbatia, loo pepo la uchafu na hisia za uharibifu zikaanza kuzunguka kaiyao kama kibirinzi. Nurdini akajifanya kusema maneno ya uwongo “dah ivi wewe ndiye mtumwa ambaye baba yangu amekununua kwa ajili yangu, binti bila hata kufikiri akajibu “ndio bwana wangu”. Nurdini akasogea karibu, akamuangalia vyema, kisha akaongeza ukaribu hata pasibakie na nafasi kati yao. Nurdini akamuangalia vyema kisha akasema “kwa hakika baba amenichagulia mke na si mtumwa”

 

 

 

 

 

Maneno haya yalipenya ndani sana kwenye moyo wa binti na kuchokoa hisia zilizolala toka zamani sana. Kisha nurdini akaongeza “je utakubali kuwa mke wangu, ama kuwa mtumwa sehemu nyingine” nyundo ya mapenzi ikapenya ndani zaidi na kwenda kugonga msumari wa mapenzi uliokuwa umelegea kwenye moyo wa binti. Hapo akajikuta kuruhusu hisia zake kupokea Nurdini. Binti hakujibu kitu, ila kwa ishara ya macho Nurdini alishatambua jibu. Nurdini akamkumbatia na kumpusu, hapo binti akaanza kutetemeka. Hakuna hakika kama sababu I baridi, uwoga ama ndio mambo ymefana.

 

 

 

 

 

Wakiwa katika hali hiyo ghafla mlango ukafunguliwa na loo! Mama Nurdini akashuhudia wawili hawa wakiwa wamekumbatiana. Mama nurdini akaangalia vyema akagundua kuwa binti alikuwa bado amevaa zile nguo alizotoka nazo kuoga. Mama nurdini alikasirika sana, ila kwa upande wa pili aliona pia bora iwe hivi maana mwanzo alikuwa akimuonea wivu mtumwa kwa mumewe. Lakini sasa mwanaye ndiye amemchukuwa mtumwa kabla ya kufikishwa kwa mfalme. Kilichokuwa kikimpataaba mama ni kuwa mumwe wake mzee faridi atachukuwa maamuzi gani?

 

 

 

 

 

Nurdini kuona vile alikimbia kwa kumuogopa mama yake. Yule binti moyo ulimruka na kutamani ardhi ipasuke ili apotelee ardhini. Mama Nurdini alimpiga kibao kimoja kizito sana. “huna hata haya wewe, hivi ukaribu wote mume wangu aliokupa ndio unamuharibia hivyo, ataiweka wapi sura yake mume wangu pindi mfalme akigundua jambo hili, ivi unajuwa kuwa ulichokifanya unaweza kuhatarisha maisha ya familia nzima, ikiwemo huyo kibwana chako Nurdini, shetani mkubwa wewe” yalikuwa ni maneno ya mama Nurdini. Hakika yule mtumwa alijiona ni mkosaji sana. Kisha akasema “nisamehe mama, ila Nurdini ndio chaguo langu, la kwanza na ni la mwisho”.

 

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:58:17 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 63


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 14: Wageni
Simulizii hii ni nzuri na ni mojawapo ya hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 28: Hadithi ya mshona nguo (fundi cherehani)
Muendelezo...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 15: Baba tajiri na kifo chake
Muendelezo....... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 4: Ndoa ya kwanza
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 7: Taharuki
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 11: Vidole gumba vilikatwa
Kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA kina simulizi nyingi nzuri na za kusisimua, muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 2 Part 1: Hadithi ya jini na mfanya biashara.
Hadithi hii ya jina na mfanya biashara imetoka katika kitabu cha kwanza cha simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza karibu tusikilize simulizi nzuri na zakusisimua Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 1 Part 2: Simulizi ya kisa cha mfugaji na mkewe
Simulizii hii ni inatoka katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 16: Usaliti
Hadithi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi sana na zinavutia na zinasomwa na kusikilizwa kwa wakubwa na wadogo na hii simulizi inatoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 22: Kaka wa kwanza wa kinyozi
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 10: Ndoa ya binti mfalme na Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 1 Part 1: Simulizi ya kiapo cha Sultan
Simulizi hii inatoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadidhi za HALIF LELA U LELA. Soma Zaidi...