picha

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 4: Sehemu ya pili ya safari ya Sinbad

Muendelezo wa hadithi ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.....

SAFARI YA PILI YA SINBAD

 

Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi. Walipokusanyika watu wote vikaagizwa vinywaji na vileja na kuanza kula huku wakisikiliza hadithi. Sinbad wa baharini akaanza kusema “basi tambueni kuwa sfari hii ya pili nilikutwa na makubwa zaidi kuliko hii ya kwanza. Ha ilikuwa hivi:-

 

Basi tulipozungumza na nahodha kuwa wiki ijayo wataanza safari nilirudi nyumbani na kujiandaa kwa safari. Ndugu zangu walijaribu kunizuia lakini sikuwasikia “sikio la kufa halisikii dawa” wengine wakanambia najipeleka nikafe ila sikuwasikiliza. Maandalizi yalikamilika kwa siku mbili na nikawa nasubiria safari tu. Wiki ilipofika tukaanza safari kwa amani lakini siku ya tatu kabla ya kuingia kisiwa cha kwanza kufanya biashara hali ya hewe ikabadiliki ghafla.

 

Nikiwa na woga sana juu ya roho yangu nikabaki namuomba msamaha mwenyezi Mungu. Jahazi lilikwenda ovyo ovyo kwa muda wa masaa sita. Manahodha walifanya wawezapo hata wakaamua sasa kuachia hatima kwa Mwenyezi Mungu. Abiria tulianza kutapika na mimi nikiwa mmoja wapo. Kwamuda kadhaa nilipotelewa na kumbukumbu na sikufahamu zaidi. Nilikuja kupata fahamu chombo kilianza kutulia mbele yetu kukiwa na weupe kwa mbali. .

 

Nilikaa vizuri nipate lujua kinachoendelea. Manahodha walituambia kuwa kwa sasa tunaingia kisiwa cha roc. Kisiwa hiki hakuna wakazi na wanyama pia hakuna au ni wachache. Kuna hadithi ya zamani sana walokuwa wakisimulia mababu kuwa kuna roc aliyekuwa akila mali za watu kama mifugo na kujeruhi wakazi. Hivyo watu wamehama kisiwa hiki. Ni miaka mingi sasa na ni mababu tu wanasimulia hadithi hii. Huenda ni ngano tuu au ni kweli. Hivyo tutaingia hapa kwa ajili ya kupumzika kidogo na kuangalia kama tutapata maji maana safari ni ndefu. Basi tukaingia kisiwani pale na kuanza kuranda randa. Kwakuwa nilitapika sana sikuwa na nguvu za kutosha hivyo nikaelekea kwenye kivuli kikubwa na kujilaza. Nililala sana na nilipokuja kuamka sikuona watu wala jahazi. Kumbe nilisha kimbiwa, niliogopa sana na nisijue nitatokaje pale kisiwani ambapo hakuna watu wala chakula. Nilianza kujuta kwa kukubali kuja. Nilijua sasa hapa kisiwani nitakufa pekeangu kwa kukosa chakula.

 

Nilianza kukizunguka kisiwa chote kujua nini nitafanya. Jua nalo lilikuwa likizama. Katika kuzunguka nikaona kuna kitu cheupe kwa mbali. Nikaanza kukifata taratibu na nikakuta kama limpira kubwa sana na laiiini. Kuangalia vizuri sikufahamu nini kitu kile. Ghafla nikaona anga inafunikwa na kuna kivuli kikubwa kinaingia nilikimbia kwenda kujificha. Kumbe alikuwa ni ndege roc mkubwa sana yaani mguu wake mmoja ni kama shina la mti. Kumbe lile dude kubwa jeupe ni yai lake.

 

Basi kiza kilipoingia nilikwenda karibu na ndege yule nikavua kanzu yangu na kufifunga vizuri kwenye miguu ya yule ndege. Niliamini kuwa akiruka atanibeba na kunitoa kwenye kisiwa kile. Basi nilifanya hivyo na kuendelea na imani yangu hiyo. Mambo yakawa kama nilivyotaka asubhi ndege yule aliruka na kunibeba, kwa kuwa sikuwa mzito sana hakujua kama amebeba kitu lamda alijua ni guo tu.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Mankaa image Tarehe: 2024-09-10 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Burudani File: Download PDF Views 655

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 web hosting    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 19: Kinyozi

Hii ni simulizi iliyopo ndani ya kitabi cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 4: Simulizi ya chongo wa kwanza mtoto wa Mfalme

Tusikilizie simulizii inahusu chongo wa kwanza wa mtoto wa mfalme iliyopo ndani ya kitabu cha kwanza cha Hadithi za HALIF LELA U LELA.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 11: Kisa cha Kalid na Jalid

Tuendelee kusikiliza na kusoma visa, hadithi, na simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza tuwe pamoja mpka mwisho......

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 5: Simulizi ya samaki wa ajabu

Simulizii hii inapatikana kwenye hadhithi za HALIF LELA U LELA katika kitabu cha kwanza....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 1: Hadithi ya jini na mfanya biashara.

Hadithi hii ya jina na mfanya biashara imetoka katika kitabu cha kwanza cha simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza karibu tusikilize simulizi nzuri na zakusisimua

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 6: Hadithi ya Ndoa ya siri

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili muendelezo....

Soma Zaidi...