Kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA kina simulizi nyingi nzuri na za kusisimua, muendelezo....
KWA NINI VIDOLE GUMBA VILIKATWA?
Baada ya harusi niliendelea kukaa pale kwa muda wa miezi mitatu hata bila ya kurudi kwangu au kuwasiliana na ndugu zangu. Siku moja mkewangu akanieleza kuwa ana ujauzito. Nilifurahi sana, nilimkumbatia kwa furaha. Habari njema zikamfikia mke wa Sltani, basi akaandaa tafrija ndogo ya pale ndani kama kusherekea furaha ya mdogo wake kuata ujauzito. Katika tafrija hiyo muda wa kula ulipofika vyakula mbalimbali vikaletwa.
Nikanawa mikono na kuanza kula. Mkewangu hakuwepo alitokakidogo. Nilitamani hata awepo nipate kumlisha. Nilianza kula na kunywa kisha kikala Zerbajeh, nilipogusa tu chakula kile badhi ya wajakazi walikunja sura, Mke wa Sultani akanieleza kuwa mke wako anachukia sana harufu ya chakula hiko, na ndo umeshaanz akula, hivyo itakubidi uvumilie kwa lolote litakalo tokea. Sisi katu hatuta ingilia ugomvi wenu. Basi nilijitahidi kunawa vyema kwa sabuni. Baada ya tafrija kwisha nikarudi kujipumzisha.
Ghafla nikaona mkewangu amebadilika sura, na kuniambia “yaani mtu kama wewe unakula zerbajeh bila hata ya kunawa”? nikamueleza mkewangu kipenzi mbona nimenawa” kama umenawa na hii harufu ninayoipata ni ya nini” “ nimejitahidi kunawa ila hii harufu haikati kwa urahisi” haya ni maneno tuliokuwa tukijibizana.
Looo!!! Looo!!!! huwezi amini kumbe kubishana ndipo nikawa nauchochea moto wa kifuu. “nilikuona mstaarabu, nikakupenda, na nakupenda sana kipenzi, lakini kwa hili katu siwezi kuvumilia….,” mtu mstaarabu kama wewe unakula bila kunawa jamani, hapana …!! hapana…!!! kwa hili lazima nikupe adhabu, itabidi ukatwe vidole vyako. Ulivyokulia bila ya kunawa.
Aliagiza wajakazi wanifunge wanipeleke kwa hakinu ili nikakatwe vidole. Wakanifunga kamba na kunifungia kwenye chumba. Nilikaa kwa siku 10 kwenye kachumba hako huku nikawa ninakula mlo mmoja tu kwa siku. Siku ya kumi akawaambia wajakazi wanitoe, akaninusa mikono yangu na kujiridhisha kuwa harufu imekoka. Hapo akaagiza dawa ziletwe na mkasi, bendeji na vitu vingine. Akawaambia wajakazi wanikamate madhubuti, na hapo akanikata vidole gumba vyangu vyote
“nakukata hivi vidole vilivyokuacha ukala zerbajeh bila ya kunawa. Nataka ukumbuke kuwa chakula hiki, utakapokula unawe mara 40 kwa alita, mara 40 kwa sabuni na mara 50 kwa maji. Vinginevyo nitamaliza na vingine. Nilijiwazia mambo mengi hata nikasema huwenda ni huu ujauzit ndio unamsumbuwa. Lakini ujauzto ndi anikate vidole. Baada ya hapo alilia sana na akachukuwa dawa akanipaka na kuendelea kuniuguza.
Niligunduwa kuwa ananipenda sana, japo sikupatapo kujuwa hasa kilichomtokea hata akachukia sana chakula hiki. Milipanga siki moja nije nimuulize. Baada ya wiki kama 3 vidonda vyangu vilipona na hapo akaja mke wa sultani na aliponikuta akapiga tema makofi na kuniambia kuwa “umefaulu mtihani wa nne” sasampohuru kuondoka. Sikuwa naelewa maneno ya mke waSultani kuhusu mitihani ile lakini pia nilifurahi.
Jioni mke wangua akanipatia pesa nyingi na vipande vya dhahabu na kunieleza kuwa nikanunue nyumba nzuri ya ssi kuishi. Nilifanya hivyo, nilitafuta nyumba nzuri sana nje kidogo ya mji na sasa nina watoto wawili. Nimeamua leo kuja kufurahi na watu wa mjini ndipo nikakutana na shuhuli hii.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:09:02 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 108
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 2: Sultani mtoa buradani kufariki
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini na mtumwa
Muendelezo....... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 18: Binti wa pili mwimba mashahiri mwenye makovu
Mwendelezo wa hadithi kutoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 7: Hadithi ya safari ya majibu juu ya maswali mawili
Wapendwa wasomaji na wasikilizaji wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza karibu tuendelee kusikiliza hadithi zetu mzuri na za kusisimua.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 19: Mfalme na waziri wake
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 5: Bonde la uokozi
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza....... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 8: Aliyekatwa kidole gumba
Kojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 9: Hadithi ya binti wa ndotoni.
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 12: Sehemu ya tano ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 16: Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 23: Kaka wa pili wa kinyozi
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 22: Kaka wa kwanza wa kinyozi
Muendelezo.... Soma Zaidi...