picha

DUA BAADA YA TAHIYATU, NA KUTOA SALAMU KWENYE SWALA

13.

DUA BAADA YA TAHIYATU, NA KUTOA SALAMU KWENYE SWALA

13. Dua kabla ya salamu
Ni sunnah kuleta dua kabla ya salamu. Dua hizi ni nyingi ila miongoni mwanzo ni
Dua aliyotufundisha Mtume (s.a.w) kwa msisitizo mkubwa kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ya Muslim, iliyosimuliwa na Ibn Abbas, ni hii ifuatayo: Allahumma Inni-audhubika min-’adhaabi-lqabri,Wa-auudhubika min fitnatil masiihi-ddajjaal, Wa-auudhubika min fitnatil-mahyaa wal-mamaati, “Ee Allah najikinga kwako kutokana na adhabu ya kabr, na najikinga kwako kutokana na fitina za masiihi Ddajjaal na najikinga kwako kutokana na matatizo ya maisha na mauti.

Sijidat-Sah-wi (Sijda ya kusahau)
Sijdat Sah-wi ni sijidah anayoileta mtu kabla ya kutoa salaam ili kufidia kitendo cha sunnah alicho kisahau kwa mfano kusahau kukaa tahiyaatu ya kwanza.Vile vile mtu akisahau au akikosea jambo lolote ambalo halibatilishi swala kwa mfano akaswali rakaa tano badala ya rakaa nne kwa swala ya Adhuhuri. Kabla hajamaliza swala alete sijidat Sahau. Hivi ndivyo tunavyojifunza kutokana na Hadithi zifuatazo: Abdullah bin Mas’ud (r.a) amesimulia: Mtume wa Allah alituswalisha Adhuhuri rakaa tano.Tukamuuliza kama pameamrishwa na Mwenyezi Mungu kurefushwa swala akajibu, La! Tukamuambia: “Umetuswalisha rakaa tano. Akasema (Mtume): Mimi ni binaadamu kama nyinyi, nakumbuka kama mnavyokumbuka na nasahau kama mnavyosahau. Kisha akasujudu sijdah mbili zikawa ni fidia kwa kusahau. (Bukhari na Muslim).

Muhimu:
Kumbuka kuwa sijda hii Mtume (s.a.w) aliileta baada ya kutoa salaamu na baada ya kukumbushwa. Abdullah bin Buhaymah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliswalisha swala ya adhuhuri, akasimama baada ya rakaa mbili, alipomaliza swala akasujudu mara mbili huku akisema: “Allah Akbar” katika kusujudu na katika kuinuka, wakati amekaa kabla ya kutoa salaam, na watu wakasujudu pamoja naye. Hii ilikuwa ni kufidia ile tahiyyatu ya mwanzo aliyoisahau”. (Muslim)

14. kutoa salamu.
Kutoa salamu ni nguzo katika nguzo za swala. Ukamilifu wa kutoa salamu ni kusema “as-salaamu alykum warahmatullahi wabarakaatuh” salamu zipo mbili yakwanza utatoa upande wa kulia na ya pili utatoa upande wakushoto. Sifa ya kugeuka kwa kutoa salamu ni kuwa utageuka mpaka mashavu yawze kuonekana kwa mtu aliye nyuma.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views 7280

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 web hosting     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

DUA 94 - 114

DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 94.

Soma Zaidi...
AINA ZA HADITHI

Aina za HadithKuna aina kuu mbili za Hadith- (a) Hadith Nabawiyyi.

Soma Zaidi...
AL-ARBAUWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 4: Uumbwaji wa mwanadamu

HAdithi hii itakufundisha namna ambavyo mwanadamu anapitia hatuwa mbalumbali tumboni mwa mama yake

Soma Zaidi...
Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu

Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.

Soma Zaidi...
Fadhila za udhu yaani faida za udhu

Katika makala hii utajifunza faida za kuwa na udhu

Soma Zaidi...