Navigation Menu



image

DUA ZA KUSWALIA, KUAMKA, WACHAWI, MAJINI, ASUBUHI, NA JIONI NA NYINGINEZO

DUA ZA KUSWALIA, KUAMKA, WACHAWI, MAJINI, ASUBUHI, NA JIONI NA NYINGINEZO

Darsa za Dua

Ustadh Rajabu

DUA 120

Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Sala na amani zimfikia kipenzi cha Allah Mtume muhammad SwalaLlahu ‘Alyh wasallam. Ama baada ya utangulizi huu. Hiki ni kijitabu kidogo kilichoandaliwa kwa lugha ya kiswahili kikiwa kimekusanya Dua mbalimbali zaidi ya 120. Ni muhimu kwa kila muislamu kuzifahamu dua hizi.


Huu ni mwendelezo tu wa kitabu chetu cha kwanza kilichozungumzia Darsa mbalimbali za Dua, na sasa tunakuletea dua mbalimbali. Ni matumaini yetu msomaji utafaidika. Kitabu hiki unaweza kukisoma bure bila hata ya malipo ukiwa mtandaoni. Tunatarajia dua zenu wasomaji.


Ikitokea umeona kosa lolote ndani ya kitabu hiki a,ma vitabu vyetu vingine tunakuomba haraka sana wasiliana nasi. Pia tunatoa ombi kwa yeyote anayetaka kuungana nasi katika kusambaza da’wa kwa ajili ya Allah kama kuandika vitabu au kuvisambaza mitandaoni awasiliane nami haraka sana.


Mwandishi: Al Ustadhi Rajabu Athuman Phone: +255675255927 Email: admid@bongoclass.com Website: www.bongoclass.com.


1.Dhikri ya kuleta wakati wa kuamka kutoka usingizini Mtume (s.a.w) alipoamka kutoka usingizini alikuwa akisema: Al-hamdulillahilladhy ahyaanaa ba'adamaa amaatanaa wailayhi nnushuuru" “Sifa zote njema anastahiki Allah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na ni kwake tu ufufuo." Mtume (s.a.w) amesema: "atakaye amka usiku kisha akasema: Laailahaillallaahu wah-dahu laa shariika lahu, lahulmulku walahul-hamdu wahuwa a'laa kulli shay-in qadiiru, “Hapana Mola ila Allah, Mpweke asiye na mshirika, ni wake ufalme na ni zake sifa njema, ni muweza juu ya kila kitu; Kisha akasema "Rabbigh-fir-ly" “Ee, Mola nisamehe" Basi atasamehewa. Na kama atasimama akaenda kutawadha kisha akaswali basi swala yake itakubaliwa."


2.Dhikri ya kuleta wakati wa kuvaa nguo Al-hamdulillaahi lladhy kasaany hadha (thawba) warazaqaniihi min ghairi hawlin minny walaaquwwat" "Sifa zote njema ni za Allah ambaye amenivisha nguo hii na kuniruzuku pasina uwezo wala nguvu kutoka kwangu."


3.Dua ya Kuvua Nguo "Bismillah" "Kwa jina la Allah (nina vua)."


4.Dua ya Kuingilia Chooni Muislamu akiingia chooni atangulize mguu wa kushoto na kusema: (Bismillah) “Allahumma inni a'uudhubika minal-khubuth wal-khabaaithi" (Kwa jina na Allah). Ee, Allah najikinga kwako na maovu yote na wafanya maovu"


5.Dua ya Kutoka Chooni Muislamu akitoka chooni hutanguliza mguu wa kulia na kusema: “Ghuf-raanaka" “Nakuomba msamaha (Ee Allah)


6.Dhikri wakati wa kutoka Nyumbani Bismillahi tawakkal-tu 'alallaahi walaahawla walaaquwwata illaabillaahi Kwa jina la Allah, ninajitegemeza kwa Allah, na hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatokana na Allah"


7.Dhikri wakati wa kurejea nyumbani Bismillahi walaj-naa, wabismillaah kharaj-naa wa'alaa Rabanaa tawakkal-naa. “Kwa jina la Allah tunaingia na kwa jina la Allah tunatoka, na kwa Mola wetu tunategemea."


8.8.Dua ya Kuingia Msikitini Tukiingia msikitini tunatanguliza mguu wa kulia na kusema: “A'udhubillaahil-'adhiim wabiwajhi-hil-kariim. 'Wasul-Twaanihil-qadiimi minash-shaytwaanir rajiim Bismillaah wasw-swallatu wassalaam a’laa rasuulillah , Allaahummaf-tahaly ab-waaba rah-matika". “Najikinga kwa Allah aliye mtukufu, na kwa uso wake mtukufu, na kwa utawala wake wa kale, kutokana na sheitwani aliyeepushwa na rehema za Allah,Kwa jina la Allah na Rehma na Amani ziwafikie Mtume wa Allah Ee! Allah nifungulie milango ya rehema zako."


9.9.Dua ya kutoka Msikitini Tukitoka msikitini tunatanguliza mguu wa kushoto na kusema: “Bismillahir wasw-swalaatu was-salaamu 'alaa rasuulillaahi, Allaahumma inny as-aluka min fadh-lika, Allaahumma A'iswimniy, minash-shaytwaanir-rajiimi." “Kwa jina la Allah na rehema na amani zimfikie Mtume wa Allah; Ee! Allah,nakuomba katika fadhila zako, Ee! Allah nilinde kutokana na shetani aliyeepushwa na rehema zako (aliye laaniwa)."


10.Dhikri za Kuleta Asubuhi na Jioni “Allahumma 'aafiniy fiy badaniy,Allahumma 'aafiniy fiy sam-'iy. Allahumma 'aafiniy fiy baswariy,Laailaha illaa anta. (Mara tatu) Ee! Allah nipe afya ya mwili wangu,Ee! Allah nipe afya ya usikivu wangu (masikio yangu),Ee! Allah nipe afya ya uoni wangu (macho yangu). Hapana Mola ila wewe (mara tatu).


11.Allahumma inniy a'uudhubika minal-kufri, walfaq-ri, waa'uudhubika min'adhaabil-qabri, Laailaha illa anta. (mara tatu) Ee! Allah hakika mimi najilinda kwako kutokana na ukafiri; na ufakiri; na najilinda kwako kutokana na adhabu ya kabri; Hapana Mola ila wewe." (Mara 3)


12.“Has-biyallahu laailaha illaahuwa 'alayhi tawakkal-tu wahuwa rabbul-'arshil-adhiimi. (Mara saba asubuhi na jioni). Allah ananitosha, hapana Mola ila yeye. Kwake yeye ninategemea, na yeye ni Mola wa arshi tukufu (mara saba asubuhi na jioni).


13.“A'uudhubikalimaatillaahi ttaammaati min-sharri maa khalaqa." (mara tatu jioni) “Najikinga kwa maneno timilifu ya Allah kutokana na shari ya alivyoviumba" (mara tatu jioni).


14.“Bismillahi lladhii laayadhurru ma'asmihi shay-un fiyl-ardhi walaa fissamaai wahuwas-samii'ul-'aliimu. (mara tatu). “Kwa jina la Allah ambaye hakidhuru kwa jina lake kitu chochote kile kilichoko ardhini wala mbinguni, naye ni Msikivu Mjuzi.


15."Sub-haanallahi wabihamdihi, 'adadakhalqihi, waridhwaa nafsihi wazinata ‘arshihi wamidaada kalimatihi, (Mara tatu) “metakasika Allah na sifa zote njema ni zake kwa hisabu ya viumbe vyake, na radhi yake (mara tatu kila asubuhi)


16.“Allahumma inny as-aluka 'il-man-naafiaa, wariz-qan twayyiba, wa-'amalan mutaqabbala". “Ee! Allah nakuomba unipe elimu yenye manufaa, na riziki iliyo nzuri na amali (ibada) yenye kukubaliwa.


17." Sub-hanallahi wabihamdihi." (mara mia) Ametakasika Allah na sifa zote njema ni zake.


18.“Laailaha illallahu, wah-dahu laa sharikalahu, lahul-mul-ku walahul-hamdu wahuwa 'alaa kulli shay-in qadiiru" (mara mia) “Hapana Mola ila Allah, mpweke, asiye na mshirika, ni wake ufalme na ni zake sifa njema zote, na yeye yuko juu ya kila kitu.


19.Mwenye kusoma Ayatul-Kurisiyy (2:255) pindi anapoamka atalindwa kutokana na mashetani (majini) mpaka jioni, na atakayesoma jioni atalindwa nayo mpaka asubuhi. Mwenyezi Mungu hakuna Mola ila Yeye, (na) ndiye Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni Vyake (peke yake vyote) vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi. Na nani huyo awezaye kuombea mbele Yake (Allah) bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na (yajayo) nyuma yao; wala (hao viumbe) hawalijui lo lote katika yaliyo katika ilimu Yake (Mwenyezi Mungu) ila kwa alipendalo (Mwenyewe). Enzi yake imeenea mbingu; na ardhi; wala kuvilinda hivyo hakumshindi; na Yeye (peke yake) ndiye aliye juu na ndiye aliye Mkuu. (2:255)


20.Mwenye kuzisoma mara tatu asubuhi na jioni sura zifuatazo zinamtosheleza na kila kitu:


21.Suratul-Ikhlas (112:1-4) Sema, Yeye ni Allah aliye mmoja tu Allah ndiye anayestahiki 475 kukusudiwa (na viumbe vyote). Hakuzaa wala hakuzaliwa. Hakuna hata mmoja anayefanana naye." (112:1-4)


22.Suratul-Falaq (113:1-5) Sema: Ninajikinga kwa Mola wa ulimwengu wote.Na shari ya Alivyoviumba. Na shari ya giza la usiku liingiapo.Na shari ya wale wanaopulizia mafundoni.Na shari ya hasidi anapohusudu. (113:1-5)


23.Suratun-Naas (114:1-6) Sema: Ninajikinga kwa Bwana Mwenye kuwalea watu. Mfalme wa watu. Muabudiwa wa watu. Na shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma. Atiaye wasi wasi nyoyoni mwa watu. (Ambaye ni) katika majini na watu." (114:1-6)


24.Kumswalia Mtume Asubuhi na Jioni Mtume (s.a.w) amesema:Mwenye kuniombea rehema asubuhi mara kumi na jioni mara kumi, nitamuombea shufaa (masamaha) siku ya kiyama.


25.“Allahumma swali'alaa Muhammad wa'alaa aali Muhammad, kamaa swallayta 'alaa Ibraahiima wa'alaa aali Ibraahiim, Innaka hamidun majiidu, allahumma baarik-'alaa Muhammad wa-'alaa aali Muhammad, kamaa barak-ta 'alaa Ibraahiima wa-'alaa aalii Ibraahiima, Innaka hamidunmajiidu." Ee Allah! Mrehemu Muhammad na jamaa zake (wafuasi wake) Muhammad kama ulivyo mrehemu Ibrahiim na jamaa zake (wafuasi wake) Ibrahiim, hakika wewe ni mwenye kusifika mtukufu. Ee Allah! Mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na jamaa zake Ibrahiim, Hakika wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu. Mtume (s.a.w) amesema: "Anayeniswalia mara moja, Allah (s.w) humswalia mara kumi." (Muslimu).


26.Pia Mtume (s.a.w) amesema: “Bahili ni yule ninapotajwa, haniswalii (haniombei rehema na amani kwa Allah)." (Tirmidh) Kumswalia Mtume (s.a.w) kumeamrishwa kwa waumini kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo: “Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Mtume (wanamtakia rehema na amani). Basi, enyi mlioamini mswalieni (muombeeni Mtume) rehema na amani." (33:56)


27.Kuomba Msamaha na Kutubia Amesema Mtume (s.a.w): “Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika mimi ninamtaka msamaha Mwenyezi Mungu na ninatubia kwake katika kila siku zaidi ya mara sabini." (Al-Bukhari).


28.“Astagh-firu llaha waatuubu ilahi." (mara mia) “Namuomba msamaha Allah na ninatubia kwake."


29.Pia Mtume (s.a.w) amesema: "Yeyote anayesoma maneno yafuatayo, Mwenyezi Mungu atamsamehe hatakama anamakosa ya kukimbia vitani:


30.“Astagh-firu llaahal-'adhiimal-ladhii laaillaha illahuwalhayyul qayyuumu wa-atuubu ilayhi." “Namuomba msamaha Allah, Mtukufu ambaye hapana Mola ila yeye, aliye Hai, aliyesimama kwa dhati yake na ninatubia kwake."


31.Amesema Mtume (s.a.w): "Hakuna mja yeyote yule anayefanya dhambi kisha akatawadha vizuri na akaswali rakaa mbili, kisha akamtaka Mwenyezi Mungu msamaha ila atasamehewa". (Abu Daud na Tirmidh) 12. Dhikri ya kuleta baada ya kupatwa na janga au balaa “Laailaha illa llahul-'adhwiimul-haliimu, laa ilaha illa llahu r a b b u l - ' a r - s h i l ' a d hwi imi , L a a i l a h a i l l a l l a h u rabbussamaawaat warabbul-ardhwi,warabbul-'ar-shilkariimi. “Hapana Mola ila Allah, aliye mtukufu mpole, Hapana Mola ila Allah, Mola wa arshi tukufu, Hapana Mola ila Allah, Mola wa mbingu na ardhi na Mola wa arshi tukufu. “Laailaha illaa-anta Sub-hanaanaka inny kuntuminal Dhw- Dhwaalimiina." Hapana Mola ila Wewe, Utukufu ni wako, hakika mimi ni miongoni mwa waliodhulumu nafsi zao. 13.Unapokutana na adui au mtawala dhalimu “Hasbunallahu wani'imal-wakiilu" “Allah anatutosheleza Naye ni mbora wa kutegemewa.


32.Dua ya Kulipa Deni "Allahummak-finiy bihalaalika'an haraamika wa-agh-niy bifadhw-lika 'amman siwaaka." Ee Allah! Nitosheleze na halali yako na Uniepushe na haramu yako, na Unitosheleze kwa fadhila zako nisiwahitaji wengine asiye wewe.


33.Dua anayoleta yule aliyefikwa na jambo gumu “Allahumma laasah-la illaa maaja-'al-tahu sah-laa, wa anta taj-'alul-haz-na idhaashi-ita sah-laa. Ee Allah hakuna jepesi ila ulilolifanya jepesi, nawe unalifanya gumu kuwa jepesi ukitaka.


34.Dua ya kuomba unapotokewa na jambo usiloliridhia au unaposhindwa kufanya jambo Amesema Mtume (s.a.w) (katika Sahihi Bukhari): "Muumini mwenye nguvu (qawiyyu) ni bora na anapendeza zaidi kwa Allah (s.w) kuliko muumini dhaifu, na wote wanakheri. Fanya pupa kwa kile kitakacho kunufaisha na taka msaada wa Allah wala usichoke, na kikikupata kitu chochote kibaya basi usiseme lau kama ningelifanya kadha na kadhaa yasingenitokea haya, lakini sema: "Qaddarallahu wamaa shaa-af-a'la. “Amepanga Allah na analolitaka anafanya." Hakika Allah analaumu mwenye kukata tamaa, lakini usivunjike moyo, na ukishindwa na jambo kabisa sema: "Has-biya llahu wani-i'mal-wakiilu" "Allah ananitosheleza, Naye ni mbora wa kutegemewa."


35.Dua ya Kumuombea mgonjwa wakati wa kumtembelea “Laa ba-asa twahuurun in-shaa-allahu." “Hakuna neno, (ugonjwa) ni kusafishwa na dhambi anapopenda Allah." (Al-Bukhari) Anasema Mtume wa Allah: "Hapana yeyote Muislamu anayemtembelea mgonjwa ambaye wakati wake wa kufa bado haujafika na anamuombea mara saba. “As-alullaah l-a'dhiima rabal-a'r-shi l-a'dhiimi an-yash-fiyaka. “Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa arshi tukufu akuponyeshe." Isipokuwa Allah humponyesha mgonjwa huyo." (At-Tirmidh na Abu Daud)


36.Dua anayoomba mgonjwa aliyekata tamaa na kupona “Allahumma gh-fir-liy war-hamniy wa-alhiq-niy birrafiiq il-a-a'laa" 481 Ee! Allah, nisamehe na unirehemu na unikutanishe na waja walio katika daraja za juu".


37.Dua ya kuomba mvua “Allahumma asqinaa ghaythan mughiithan mariian mariia'a, naafia'an ghayradhwaarrin, a'ajilanghayra aajilin. Ee! Allah tunyesheleze mvua yenye kuokoa, nyingi, yenye kustawisha, yenye manufaa isiyodhuru.


38.Dua ya kuleta wakati unapovuma upepo Allahumma inniy as-aluka khayrahaa wa-au'udhubika minsharrihaa. Ee, Allah! Ninakuomba unipe kheri ya upepo huu na uniepushe na shari yake.


39.Dua ya kuleta wakati mvua inanyesha “Allahumma Swayyiban naafia'n “Ee Allah ijaalie iwe mvua yenye manufaa."


40.Dua ya kuleta baada ya mvua kunyesha Mutwir-haa bifadh-lillahi warah-matihi. Tumepata mvua kwa msaada na rehema ya Allah."


41..Dua ya kusema unapoanza kula Unapoanza kula hunabudi kusema: “Bismillaahi" “Kwa jina la Allah" Na ukisahau kusema hivyo wakati wa kuanza, ukikumbuka wakati unaendelea kula sema: “Bismillahi fiy awwalihi wa-aakhirihi" “Kwa jina la Allah katika mwanzo wake na mwisho wake" 24.Dua ya kushukuru baada ya kula “Al-hamdulillahilladhii atw-a'maniy hadhaa warazaqaniyhi min ghayri hawlin minniy walaa quwwatin" “Shukurani zote anastahiki Allah ambaye amenilisha chakula hiki bila ya uwezo wala nguvu yoyote kutoka kwangu."


42.Dua ya mgeni kumuombea mwenyeji aliye mlisha chakula “Allahumma baarik-lahum fiymaa razaq-tahum, wagh-fir lahum war-hamhum." 483 Ee Allah, wape baraka kwa hicho ulicho wapa,wasamehe na warehemu."


43.Dua ya kuleta baada ya kupiga chafya Unapopiga chafya hunabudi kusema: “Al-hamdulillaahi" “Sifa zote anastahiki Allah." Kisha ndugu zako Waislamu watasema: “Yar-hamuka llahu." “Allah akurehemu." Kisha utajibu kwa kusema: "Yah-diykumullahu wayusw-lihi baalakum." "Allah akuongozeni na kuwasahilishia mambo yenu." Kama anaeambiwa ni mwanamke “Utasema yar-hamuki llahu”


44.Dua ya kuwaombea maharusi (waliooana) “Baarakallahulaka,wabaaraka a'layka,wajamaa'baynakumaa fiy khayrin" “Allah akubariki wewe na yeye (mkeo/mumeo) na awaunganishe katika kheri."


45.Dua ya kuleta unapoanza kufanya tendo la ndoa “Bi smi l lahi A l lahumma jannib-nashshay - twaana wajannibish-shytwaana maarazaq-tanaa". “Kwa jina la Allah, Ee Allah muweke shetani mbali nasi na muweke shetani mbali na hicho ulichoturuzuku."
Pata kitabu Chetu Bofya hapa






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2996


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

DUA ZA KUONDOA WASIWASI
DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah. Soma Zaidi...

Namna ambazo Allah hujibu dua ya mwenye kuomba.
Post hii inakwenda kukufundisha namna ama staili ambazo Allah hujibu dua za watu. Soma Zaidi...

Matamshi ambayo ukimwambia Allah kwenye dua yako basi hujibiwa kwa haraka dua hiyo
Post hii inakwenda kukufundisha matamshi ambayo mtu akiyatamka Allah hujibu dua hiyo kwa urahisi. Soma Zaidi...

Al-Arba-uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 5: kujiepusha na uzushi katika dini
Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini Soma Zaidi...

Dua 10 ambazo ni muhimu kuziomba kwa kila siku.
Posti hii inakwenda kukupa orodha ya dua 10 ambazo unaweza kuziomba kila siku. Soma Zaidi...

DUA ZA SWALA
DUA ZA SWALA 1. Soma Zaidi...

Maswali juu ya Sunnah na hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

SWALA YA MTUME (s.a.w)
SWALA YA MTUME Kumswalia Mtume (s. Soma Zaidi...

Dua Sehemu ya 02
Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa. Soma Zaidi...

darasa la dua
Soma Zaidi...

Faida za swala ya Mtume
Hapa utajifunza fadhila za kumswalia Mtume (s.a.w) Soma Zaidi...

HADITHI YA 34 YEYOTE ATAKAYEONA KITENDO KIOVU AKIONDOE KWA MKONO WAKE
Soma Zaidi...