Kwenye mada hii tutajifunza shahada mbili,tafsiri ya shahada kstika maisha ya kila siku.
6.2.Shahada Mbili.
“Nashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah”
- Kiutendaji maana yake ni kuahidi kwa dhati utaishi kila kipengele cha maisha yako kwa kumtii Allah (s.w) katika maamrisho na makatazo yake.
- Pia ni kuahidi kuwa hutamtii yeyote isipokuwa Allah (s.w) na kuendesha maisha yote kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah.
“Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah”
- Kiutendaji maana yake ni kuahidi kuishi kwa kufuata mafundisho ya Mtume (s.a.w) na kuacha aliyoyakataza.
Rejea Qur’an (59:7).
- Pia ni kuahidi kufuata mwenendo na tabia za Mtume (s.a.w) kama kiigizo cha maisha yetu yote.
Rejea Qur’an (33:21).
- Shahada haikamiliki kwa kutoa shahada ya kwanza tu ni lazima uongeze na ya pili kwa sababu Mtume (s.a.w) ndiye mwalimu aliyeteuliwa na Allah (s.w) kuufundisha wahyi kwa wanaadamu ili kumtambua na kuweza kumuabudu yeye ipasavyo.
- Ni ile inayoyakinishwa kwa dhati moyoni bila ya chembe ya shaka juu ya kuwepo Allah (s.w) na juu ya Utume wa Muhammad (s.a.w).
Rejea Qur’an (49:14-15).
2.Shahada ya Matamshi (Ulimini).
- Ni lazima shahada baada ya kuyakinishwa moyoni itamkwe dhahiri mbele ya umma wa Kiislamu ili kumtabulisha kwao kwa lengo la kujenga udugu naye na kuwa ummah mmoja.
Rejea Qur’an (9:33), (61:9), (48:28), (49:10), (61:4) na (3:102).
3.Shahada ya Vitendo.
- Shahada ya kweli ni ile baada ya kuyakinishwa moyoni na kutamkwa kwa ulimi hudhihirishwa katika vitendo vya maisha ya kila siku ya muislamu.
- Shahada ya matamshi bila kudhihirishwa katika matendo ni udanganyifu kwa mtoaji na ummah wa Kiislamu, na haikubaliki mbele ya Allah (s.w).
Rejea Qur’an (49:14).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Mahusiano kati ya elimu ya mwongizo na elimu ya mazingira katika uislamu.
Soma Zaidi...Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.
Soma Zaidi...Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.
Soma Zaidi...