Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa Kuna maambukizi kwenye magoti, kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha maumivu au maambukizi kwenye magoti Kuna dalili za mwanzo ambazo zinajitokeza kama tutakavyoona hapo chini
1. Kuwepo kwa maumivu wakati wa asubuhi au wakati wa baridi.
Kwa kawaida wakati wa asubuhi na wakati wa baridi kunakuwepo na hali ambayo usababisha mwili kusinyaa kwa hiyo kutokana na kusinyaa kwa mwili hivyo hivyo usababisha misuli ya magoti kusinyaa na kusababisha maumivu pale penye maambukizi hasa mtu akitaka kusimama au kutembea kwa hiyo watu wenye maambukizi upata shida sana.
2. Kuwepo kwa maumivu wakati wa kubeba mizigo.
Kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye magoti endapo mtu atabeba mzigo mzito maumivu yote yataishia sehemu Ile iliyoadhirika kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi na hivyo sehemu hiyo inakuwa imeathirka sana.
3. Kuwepo kwa maumivu wakati wa kutembea.
Kwa kawaida Mtu anapotembea kutoka hatua Moja kwenda nyingine usababisha na viungo vyote kubadilisha mwelekeo na kuelekea kwa mtu ambapo anaelekea kwa kufanya hivyo usababisha sehemu Ile yenye maambukizi kuumia kwa sababu ya msuguano kutoka sehemu Moja kwenda nyingine.
4. Maumivu wakati wa kuchuchumaa
Kwa kawaida Mtu anapotaka kuchuchumaa ni lazima kuhusisha na magoti kwa hiyo akitaka kuchuchumaa usababisha maumivu makali kwenye magoti na vile vile kushindwa kuchuchumaa na wengine wanatumia choo za kusimama kwa sababu ya kushindwa kuchuchumaa kwa sababu ya maumivu kwenye sehemu ya maambukizi.
5. Maumivu wakati wa kufanya kazi yoyote ile.
Hii nayo ni dalili Mojawapo inayowapata watu wenye maambukizi kwenye magoti akija kufanya kazi ni lazima kuhisi maumivu kwenye sehemu ya maambukizi na pengine watu wengine ushindwa kufanya hata kazi ndogo kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi.
6. Pia maumivu wakati wa kunyanyua vitu vizito.
Kuna wakati mwingine mtu akija kunyanyua vitu vizito anahisi maumivu makali kwenye sehemu ya maambukizi.
7. Maumivu wakati wa kusimama.
Na pia kama mtu amekaa chini unalalamika sana maumivu akija kuamuka kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye magoti.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za minyoo na sababu zake
Soma Zaidi...maambukizi ya kawaida ya zinaa (STI), Hujulikana Kama Chlamydia. Huenda usijue una Ugonjwa huu kwa sababu watu wengi hawapati dalili au ishara, kama vile maumivu ya sehemu za siri na kutokwa na uchafu kutoka kwa uke au uume. Maambukizi haya huathiri
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi athari za Ugonjwa wa herpes simplex kwa watoto wadogo, tunajua kubwa mama kama ana ugonjwa huu anaweza kumwambikiza mtoto na mtoto akazaliwa na Ugonjwa huu.
Soma Zaidi...post hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa kifaduro ambao hujulikana Kama Pertussis pia inajulikana kama kifaduro ni maambukizi ya bakteria ambayo huingia kwenye pua yako na koo.
Soma Zaidi...Postii hii inshusiana na dalili na ishara za kujikinga au kuzuia malaria kwa Njia mbalimbali.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa kipindupindu.Ni dalili zinzojitokeza kwa magonjwa wa kipindupindu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu Zaidi dalili za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu, ni dalili ambazo zinaweza kujitokeza Kwa mgonjwa,Kwa hiyo baada ya kuona dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospital mara moja Kwa ajili ya matibabu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za UTI upande wa wanaume
Soma Zaidi...Kabla ya kubanwa zaidi na pumu, kuna dalili za awali zinzznza kujitokeza, na hapo ndipo utakapoanza kuchukuwa tahadhari. Makala hii itakwenda kukujulisha zaidi kuhusu dalili hizo.
Soma Zaidi...