Mbu (mosquito)
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mdudu mbu
MBU (MOSQUITO)
Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik. Mbu anafahamika kwa kuwa ndiye msambazaji mkubwa wa malaria pamoja na matende na ngiri maji. Chakula cha mbu ni maji, bakteria pamoja na damu. Mbu dume huweza kumjua mwanamke kwa kutumia sauti ya mbawa. Mbu ni katika wadudu wadogo lakini wana maajabu makubwa. Katika mkala hii tutaangalia kwa ufupi mambo matano kuhusu mbu.
Tofauti na kuwa mbu ni mdogo lakini anaweza kunyonya damu iliyokuwa nzito kuliko mwili wake. Yaani sawa na mtu mwenye uzito wa kilo 70 kula chakula chenye uzito wa kili 100. mara mbu anaponyonya damu mwili wake huchukuwa mpaka siku tatu kuweza kuimeng’enya damu ile na kuimaliza. Baada ya hapo mbu atakwenda kunyonya damu tena. Itambulike kuwa chakula cha mbu ni bakteria, maji pamoja na damu. Mbu jike hula damu pindi anapotaka kutaga. Wataalamu wanaeleza kuwa kuna aina 2000 za mbu.
picKabla ya mbu kutaga mayai yake anaanza kupima ardhi kama ina majimaji pamoja na joto la kutosha kwa maisha ya mayai yake. Mbu hutaga mayai juu ya maji, ardhi, miti na nyasi pamoja na maeneo mengine yaliyo na majimaji. Pia mbu anaweza kutaga yai lake hata pakiwa na maji kiasi cha tone moja tu. Nayai ya mbu ni chakula kwa samaki pamoja na watutu wengine hivyo mbu huwa makini sana wakati wa kutaga mayai yake.
Tofauti na wadudu wengine na ndege mbu anaweza kulizuia yai lake tumboni kulitaga pindia anapohofia usalama wa yai lake. Kuku na ndege wengine yai linapofikia kutagwa hana namna lazima akalitage, lakini hii ni tofauti kwa mbu. Yai la mbu linaweza kukaa kwa muda wa miaka miwili bila ya kufa na ndo maana ni vigumu kutokomeza kabisa mbu.
Yai la mbu lina rangi ya njano, tangi hii ni rahisi kulifanya yai hili lionewe na maadui walao mayai ya mbu. Hivyo ifikapo usiku yai la mbu hubadilika rangi na kuwa jeusi. Hali hii husaidia kuliepusha yai la mbu kuliwa na maadua. Pia yai la mbu halizami ndani ya maji, na linaweza kuelea hewani, njia zote hizi husaidia ulinzi wa yai hili lisidhuriwe.
Ijapokuwa mbu anakula binadamu lakini na yeye ni chakula kwa viumbe vingine kama popo. Hivyo popo hutusaidia katika mapambano dhidi ya wadudu hawa hatari. mbu pia anaweza kujuwa wati mtu yupo kwa kutumia pumzi anayopumua mwanadamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Ndege kwenye ulimbo
Wahenga wanaelewa, enzi hizo unaambiwa ndege akinasa basi unakumbuka macho juu asije akayoke. Hukuchinib. hujali kama kuna mjimba ama nini
Soma Zaidi...Maumivu ya Chini ya Tumbo kwa Mwanamke: Sababu na Tiba
​Maumivu ya chini ya tumbo (nyonga) ni hali inayowapata wanawake wengi katika vipindi tofauti vya maisha yao. Maumivu haya yanaweza kuwa ya ghafla (kali) au ya muda mrefu (sugu), na yanaweza kusababishwa na mifumo mbalimbali mwilini ikiwemo mfumo wa uzazi, mkojo, au mmeng'enyo wa chakula. Makala hii inaangazia sababu kuu za maumivu haya na jinsi ya kukabiliana nayo.
Soma Zaidi...Kitabu Cha
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Kukosa Subira na Uvumilivu: Jinsi ya Kubadilisha Tabia na Kujenga Ustahimilivu wa Kudumu
Kukosa subira na uvumilivu ni changamoto inayowaathiri wengi katika ulimwengu wa sasa wa kasi na teknolojia. Makala hii ya kina inachambua kisaikolojia vyanzo vya tabia hii, madhara yake katika afya ya akili na uhusiano, na inatoa mbinu za kivitendo kulingana na sayansi ya tabia (behavioral science) ili kujenga uvumilivu wa kudumu. Pata mwongozo kamili wa jinsi ya kubadilisha mtazamo wako na kufikia utulivu wa ndani.
Soma Zaidi...TUNAKUTAKIENI RANADHANI MUBARAKA
Wikibongo inawatakia waislamu wote heri ya mfungo wa ramadhaji
Soma Zaidi...