Cheetah


image


Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama cheetah


.Cheetah

 

picHuyu ni katika wanyama jamii ya paka, na anafanana zaidi na mnyama anayeitwa puma. Cheetah ni mnyama mwindaji kama walivyo chui, simba na mbwa mwitu. Ijapokuwa cheetah wanafanana kwa sura na maumbile lakini unaweza kutofautisha mmoja kwa mwingine kwa kutofautisha rangi za kwenye mikia yao. Cheetah ni katika wanyama walio hatarini kwa kuuliwa kwani wapo wachache sana. Wataalamu wa wanyama na watafifi wanaeleza kuwa nchi ya Namibia ndio nchi pekee yenye cheetah wengi zaidi. Inakadiriwa cheetah wanaoishi maeneo haya wanafika 2500. Cheetah anaweza kufika uzito wa kilogramu 39 mpaka 65 (kg 29 - 65).

 

picTafiti zinaonesha kuwa cheetah ndiye mnyama anayekimbia kwa kasi zaidi kuliko wanyama wote wa porini. Cheetah anaweza kukimbia kwa mwendokasi wa kilomita 97 kwa lisaa (97 km/h) na anaweza kuendelea kukimbia kwa mwendokasi huu kwa umbali wa mita 300. Mwili wa cheetah hauna uwezo wa kutoa jasho hivyo anapokimbia kwa umbali huu wa mita 300 bila ya kukpata kiwindwa chake cheetah huachana nae kwa kuhofia mwili wake kupata joto ambalo linaweza kumpelekea kufa.

 

picWanyama hawa wanakaa kwenye makundi ya familia na mara nyingi madume wanapenda kupigana. Wanyama hawa wanapoteza asilimia 10 mpaka 13 ya vile walivyoviwinda kwa simba pamoja na fisi. Tafiti zinaonesha kuwa nusu ya mawindo yao wanafanikiwa kupata chakula. Cheetah ni katika wanyama waliop hatarini sana kwani wana windwa sana na binadamu kwa ajili ya kuuliwa. Mnyama huyu anapenda kuwinda kwenye maeneo yaliyo wazi pasiwe na miti mingia mabayo itamfanya akikose kiwindwa chake kwa urahisi.

 

Cheetah ni katika wanyama ambao wanaweza kuishi muda mrefu bila ya kunywa maji. Kwani anajipatia maji anayohitaji kutoka kwenye mwili wa kiwindwa chake. Pindi anapowinda humnyatio mnyama wake mpaka ukaribu wa mita 10 ndipo humkurupukia na kumkumbiza kwa mwendokasi wa zaidi sana, na hukata tamaa pindi akimkimbiza kwa umbali wa mita 300. 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    2 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    3 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani offline    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Samaki aina ya salmon
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sifa za samaki aina ya salmon Soma Zaidi...

image Yanayoathiri betri yako
Somo hili linakwenda kukuletea mambo yanayo athiri betri lako Soma Zaidi...

image Kufungua program nyingi kwa wakati mmoja
Posti hii inakwenda kukuelekeza njia za kufungua program nyingi kwa wakati mmoja Soma Zaidi...

image Tembo
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama tembo Soma Zaidi...

image Kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao Soma Zaidi...

image Utunzaji wa betri la kifaa chako
Posti hii inakwenda kukupa elimu kuhusu utunzaji wa betri la kifaa chako Soma Zaidi...

image Cheetah
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama cheetah Soma Zaidi...

image Mbu (mosquito)
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mdudu mbu Soma Zaidi...

image CONTACT US
Soma Zaidi...

image OUR PRIVACY POLICIES.
Soma Zaidi...