Posti hii inahusu zaidi saratani zinazowashambulia watoto. Hizi ni aina mbalimbali za saratani ambazo upenda kuwasumbua watoto ambao ni chini ya umri wa miaka mitano na uleta madhara katika kipindi cha makuzi yao.
Saratani zinazowashambulia watoto.
1.Kwanza kabisa tunajua kuwa saratani ni Ugonjwa ambao utokea kwa sababu ya kuwepo kwa seli zisizohitajika zinaweza kutokea katika sehemu yoyote ile ya mwili . Kwa watoto Sababu za kuwepo kwa tatizo la saratani hazijathibitishwa bado ila kuna vitu ambavyo vinaweza kuchangia kama vile uvutaji wa sigara wakati wa ujauzito, pombe kali na mtindo wa maisha wa Mama kwa a ujumla wakati wa ujauzito unaweza kusababisha kuwepo kwa saratani kwa watoto. Kwa hiyo watoto wanashambuliwa na saratani zifuatazo.
2.Kuna saratani ya damu.
Aina hizi ya saratani utokea pale ambapo mtoto anakuwa anaishiwa na damu mara kwa mara inawezekana kupitia sehemu yoyote kama vile puani au inawezekana isipite sehemu yoyote ila mnaongeza damu ila baada ya siku chache mtoto anaishiawa damu, aina hii ya saratani kama haijafahamika mapema inaweza kumchukua mtoto mara moja kwa hiyo baada ya tatizo hili kutokea wazazi au walezi wanapaswa kuwasiliana na wataalamu zaidi wanaohusika na Magonjwa ya saratani.
3. Saratani ya macho.
Pia ni mojawapo ya saratani inayowapata watoto unakuta jicho la mtoto linakuwa na uvimbe mdogo na kuwasha na kadiri mda unavyokwenda unakuta uvimbe unaongezeka na mtoto anashindwa kuona na kwa wakati mwingine unakuta jicho limetokezea kwa nje na kumfanya mtoto kuangaika kwa sababu ya kuwepo kwa maumivu makali kwenye jicho. Kwa hiyo wazazi na walezi baada ya kuona tatizo kama hili mnapaswa kumpeleka mtoto hospitalini mapema ili kupunguza ukali wa tatizo.
4. Kuna saratani ya mifupa.
Pia na hii ni aina ya saratani ambayo ushambulia mifupa kwa na kabisa mtoto uanza kusikia maumivu anapotembea na pia kadri siku zinavyoenda anashindwa kutembea kabisa kwa sababu mifupa uanza kusagika na kwa hiyo ukimgusa sehemu yoyote ile anaanza kulia kwa hiyo mtoto anaweza kuishi kwa kulala maisha yake yote na kushindwa kuendelea kukua katika hatua za makuzi ya mtoto.
5. Kuna saratani ya ubongo na ngozi.
Aina hii tena ya saratani uwapata watoto chini ya miaka mitano kwa sababu unakuta watoto wanakuwa kama zezeta na wanashindwa kukua katika hatua za mtoto na pengine mtoto hawezi kukaa na kusimamia viungo na pia macho yao huwa yanaangalia makengeza na pengine mtoto anashindwa kuwa na balance. Hali utokea kwa sababu ya kukosa mawasiliano kati ya ubungo na misuli.
6. Pia kwenye ngozi ya mtoto panakuwepo na ma upele ambayo hayaeleweki na hata yakitibiwa mara hali inajirudia kuna wakati mwingine ngozi ya mtoto inaweza kubadilika kwa namna moja ama nyingine, pengine ngozi inaweza kuwa nyeupe au pengine nyeusi zaidi na kwa wakati mwingine kuwa na rangi ya mabaka mabaka kwa hiyo ngozi ubadilika Mara nyingi kwa hiyo baada ya kuona hali kama hizi ni wazi kubwa hiyo ni kansa ya ngozi.
7. Kwa hiyo kwa akina Mama wanapaswa kujua kuwa saratani kwa kawaida yake ikionyesha Dalili za mwanzoni na mtoto akapelekwa hospitali na tatizo likagunduliwa mapema anaweza kupona na kurudia kwenye hali ya kawaida kwa hiyo pindi mama akiona dalili hambazo hazieleweki kwa watoto anapaswa kufuata matibabu mara moja ili kuepuka madhara zaidi. Ila kwa walio wengi wanasubiri tatizo likiwa kubwa ndio wanakuja na kusema kweli tiba inakuwa ni shida na kupona kwa mtoto itakuwa bahati.
8.Kwa hiyo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla inapaswa kupewa elimu kuhusu kuwepo kwa saratani kwa watoto na kuwaambia Dalili zake na pia wajue madhara yatokanayo na tatizo hili na pia akina Mama wakati wa ujauzito wanapaswa kufuata mashariti yote na kuachat na ulevi pamoja na uvutaji wa sigara, na kutumia vitu visivyofaa wakati wa ujauzito ili kuepuka matatizo ya saratani kwa watoto.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1002
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Nina vidonda kwenye uume wangu, je ni dalili ya nini?
Soma Zaidi...
Uume ukiwa unaingia na ukiwa ndani nahic maumivu Kama uke unawaka Moto tafadhali nishauri
Je unasumbuliwa namaumivi wakati wa nlishiriki tendo la ndoa ama baada. Huwenda post hii ikakusaidia. Soma Zaidi...
Je dalili ya kuuma tumbo huanza baada ya wiki ngapi Toka mwanamke apate ujauzito?
Maumivu ya tumbo ni moja katika dalili za ujauzito. Maumivu wanawake wengi hushindwa kujuwa kuwa ni ujauzito ama laa. Na hii ni kwa sababu kwa wanawake wengi maumivu ya tumbo ama changu ni jalivya kawaida kwao. Soma Zaidi...
Madhara ya kufanya tendo la ndoa na mwanamke akiwa katika siku zake.
Tendo la ndoa wakati wa siku za hedhi ni halia mbayo jamii nying zinakataza. Katika vitabu vya dini pia haviruhusu, hata ki saikolojia utaona kuwa sio jambo jema. Hata hivyo hapa ninakuletea madhara yake kiafya Soma Zaidi...
Dalili za tezi dume na sababu za kutokea kwa tezi dume.
dalili za ugonjwa wa tezi dume, na sababu za kutokea kwa tezi dume, maana ya tezi dume na athari zake Soma Zaidi...
Mwanamke anatema mate mara kwa mara je inaweza kuwa ni ujauzito?
Ni kweli kuwa kutema mate mara kwa mara inaweza kuwa ni dlili za ujauzito. Lakini itambulije kuwa pekee sio kithibitishi cha ujauzito. Soma Zaidi...
MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA
Maumivu wakati wa tendo la ndoa kitaalamu huitwa dyspareunia. Soma Zaidi...
je mtu kam anaona dalili za mimb ila akapima nakipim hakijamuonyesha kam ana mimb am hana je kuna uwezekan wakuw anayo
Dalili za mimba pekee haziwezi kuthibitisha uwepo wa mimba. Bila vipimo kwa. Muda sahihi huwezi kuwa. Na uhakika. Je na wewe unasumbuliwa na dalili za mimba na ukapona hakuna mimba? Makala hii ni kwa ajili yako. Swali Soma Zaidi...
Dalili na sababu za Kukosa hedhi
Post hii inaongelea kuhusiana na Kukosa hedhi ambapo kitaalamu hujulikana Kama Amenorrhea ni kutokuwepo kwa hedhi - hedhi moja au zaidi ya kukosa. Wanawake ambao wamekosa angalau hedhi tatu mfululizo wana amenorrhea, kama vile wasichana ambao hawajaanz Soma Zaidi...
Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa
Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoabkunaweza kuashiria kuwa kuna majeraha yametokea huwenda ni michubuko ilitokea ndio ikavujisha damu. Lakini kwa nini hali kama hii itokee. Posti hii itakwwnda mujibu swali hili. Soma Zaidi...
Sababu za kutangulia kwa kitovu wakati Mtoto anazaliwa
Posti hii inahusu zaidi sababu za kutangulia kwa kitovu wakati wa mtoto anapozaliwa. Soma Zaidi...
Sababu za kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.
Post hii inahusu zaidi sababu za kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, kuna wakati mtoto anapozaliwa anaweza kuvunjika kwenye sehemu mbalimbali kwa sababu zifuatazo. Soma Zaidi...