Dalili za mimba, na m,imba changa
DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO)
Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupotea bila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua. Wapo wengine wanakujakujitambua ujauzito ukiwa na miezi kadhaa. Sasa ni zipi hasa dalili za ujauzito?. huenda swali hili kwa wanawake walio wengi lisiwe na manufaa kwao kwani tajari ni wajuzi wa swala hili. Halikadhalika wanaume wengi wanaujuzi pia. Kwani wengi wanaelewa kuwa dalili ya ujauzito ni kukosekana kwa siku za mwanamke yaani hedhi kwa vipindi zaidi ya kipoja. Lakini itambulike kuwa hii sio dalili pekee, kwani siku zinaweza kukosekana na isiwe mimba. Katika makala hii tutakwenda kuonesha kwa utani dalili kadhaa za ujauzito.
Kabla ya kiziona dalili hizo ningependa kutumia muda kidogo kueleza tatizo la kukosa kwa hedhi. Hedhi ni muhimu kwa kila mwanmke ambaye amefikia umri wa kupata ujauzito. Afya ya mwanmke huyu huwa salama kama hedhi yake ipo salama. Kwa kawaida hedhi huweza kukatika yaani kukata kutoka kabisa pindi umri wa mwanamke unapokuwa mkubwa yaani kuanzia miaka ya 45 na kuendelea. Katika kipindi hiki mwanamke huyu kupata tatizo la kutokupata siku zake ni la kawaida sana, ama siku zake kutokuwa na mpangilio maalumu.
Kwa wanawake walio wadogo kukata kwa hedhi kuna sababi nyingi sana. Watu wengi wamezoea kuwa lamda kupata ujauzito ndio sababu ya kutokupata siku zake. Hii sio swa kabisa. Kukata kwa siku za mwanamke kunaweza kusababishwa na maradhi kama kisukari na baadhi ya maradhi yanayoipata ovari ya mwanamke. Ovari ndio sehemu pekee ya mwanamke ambayo mayai huzaliwa. Hivyo sehemu hii ndio ambayo inatoa homoni ambazo huchochea upatikanaji wa hedhi ama huzuia hedhi isipatikane kutokana na kupata ujauzito. Pia matumizi ya njia za uzazi wa mpango huweza kusababisha tatizo hili la kutokuona siku zake mwanamke. Matumizi ya vyakula, hali ya hewa na madawa ni katika visababishi vikuu vya kutokupata hedhi kwa muda sahihi.
Baada ya kugusia kidogo kipengele hiko sasa tukaone baadhi ya dalili za ujauzito. Kwa hali ya kawaida dalili hizi huweza kuwa tofauti kwa mwanamke mmoja hadi mwingine. Ijapokuwa hali ni kama hii pia zipo dalili ambazo huwapata karibia wanawake wote:-
1.Kuonekana kwa damu iliyo chache. Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa asilimia 25% (yaani robo) ya wanawake wote wanaopata ujauzito hutokwa na damu kidogo, na rangi ya damu hii haikuiva kama ile ya hedhi. Damu hii hutokea siku 6 mpaka 12 baada ya kutungwa kwa mimba. Ila kwa wanawake walio wengi huiona damu hii kwenye wiki 12 za mwanzo za ujauzito.
2.Kujaa au kuuma kwa chuchu; mwanzoni mwa wiki ya 1 mpaka ya 2 ya ujauzito mwanamke anaweza kuona kuwa matiti yake yanajaa ama kuwa mazito tofauti na kawaida. Wanawake wengine chuchu za matiti yao zinakuwa ngumu na huwa zinajaa. Wanawake wengine wanaona chuchu ama maziwa yao huwa kama na maumivu wakiyaminya.
3.Uchovu isio wa kawaida; karibia wanawake wote wanaopata ujauzito huhisi uchovu usio wa kawaida. Mara nyingi dalili hii hutokea mwanzoni mwa wiki ya kwanza toka kupata kwa ujauzito. Na hii ni kutokana na kuwa mwili unazalisha homoni za kuweza kuufanya mwili uweze kulea ujauzito, upatikanaji nwa maziwa kwa ajili ya mtoto ajae. Pia kwa kuwa mwili wa mama unaongeza kuwango cha usukumaji wa damu, hivyo uchovu kutokea ni hali ya kawaida.
4.Mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya ujaozito, mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya ghafla ya kichwa. Na hii ni kutokana kuwa mwili umeongeza kazi ya uzalishaji wa homoni, hivyo ongezeko hili linaweza kusababisha maumivu ya kishwa. Hali si kwa siku nyingi hali hii itapotea.
5.Kutapika; kwa kawaida hii hali huwapata wanawake wenye ujauzito kuanzia wiki ya pili mpaka wiki ya nane. Kitaalamu hali hii hutambulika kama โmorning sicknessโ. na huenda hali hii ikaendelea katika kipindi chote cha ujauzito.
6.Kukojoa mara kwa mara; hali hii hutokea kwa sababu mwili huzalisha homoni iitwayo human chorionic gonadotropin ambayo hii huongeza damu kupita maeneo ya chini yaani kuzunguka sehemu za siri, hivyo hali hii hupelekea mwanamke kwenda kukojoa mara kwa mara.
7.Kutokupenda baadhi ya vitu ama vyakula. Hii hutokea kwa ghafla mwanamke anachukia baadhi ya vitu ama hususani vyakula bila ya sababu yotyote.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 1009
Sponsored links
๐1
Madrasa kiganjani
๐2
Simulizi za Hadithi Audio
๐3
Kitabu cha Afya
๐4
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
๐5
kitabu cha Simulizi
๐6
Kitau cha Fiqh
Tatizo la kutanuka kwa tezi dume.
Posti hii inahusu zaidi tatizo la kutanuka kwa tezi dume, ni tatizo ambalo linawakumba wanaume wengi kwa wakati huu kwa sababu ya kuwepo kwa maaambukizi kwenye tezi ambayo Usababishwa na vitu mbalimbali kama tulivyoona. Soma Zaidi...
Madhara ya kupungua kwa homoni ya projestron
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa homoni ya projestron ikipungua mwilini na pia kuweza kutambua dalili za kupungua kwa homoni hii ya progesterone. Soma Zaidi...
Mwanamke anatema mate mara kwa mara je inaweza kuwa ni ujauzito?
Ni kweli kuwa kutema mate mara kwa mara inaweza kuwa ni dlili za ujauzito. Lakini itambulije kuwa pekee sio kithibitishi cha ujauzito. Soma Zaidi...
Njia huanza kufunguka mda gani kabla ya kujifungua
Mtoto huweza kuzaliwa ndani ya miezi 6 na unaweza kupona. Na huyu mdoe mtoto njiti. Na anaweza kuzliwa kwa njia ya kawaida. Hakuna ushahidi unaiinyesha kuwa njiti hukabiliwanamatatizo ya kitalima kwenye ukubwa wako. Soma Zaidi...
Sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke
Post hii inahusu zaidi sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke, kuna kipindi ambacho mwanamke hushindwa kushika mimba kuna sababu mbalimbali mojawapo ni kama zifuatazo Soma Zaidi...
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa kondo la nyuma
Kondo la nyuma ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamziti,kondo la nyuma husaidia katika kazi mbalimbali katika ukuaji wa mtoto. Soma Zaidi...
Imani potofu kwa mwanamke mwenye mimba
Posti hii inahusu zaidi imani potofu kwa mwanamke mwenye mimba, ni Imani ambazo zimekuwepo kwenye jamii kuhusu wanawake wenye mimba. Soma Zaidi...
Ukifanya mapenzi siku hatari na ukameza P2 unaweza pata mimba?
Je umeshawahi kujiukiza kuwa, dawa ya P2 ni kweli inaweza kuzuia mimba, ukifanya mapenzi siku hatari? Soma Zaidi...
Njia za kuzuia ugumba
Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia ugumba, ni njia ambazo utumiwa na wapenzi ambao wameshindwa kupata watoto hasa kwa wale ambao wamezaliwa wakiwa na uwezo wa kupata watoto lakini kwa sababu tofauti tofauti wanashindwa kupata watoto kwa hiyo njia zifu Soma Zaidi...
Njia za kuondoa fangasi sehemu za siri
Makala hii itakujuza baadhi ya njia utakaoweza kuzifuata ili kukabiliana na fangasi sehemu za siri kwa wanaume Soma Zaidi...