imageimage Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi.
Ni ufunuo kutoka kwa Allah (s.w) kwenda kwa wanaadamu (mitume) kupitia Malaika wake Jibril (a.s). Wahyi umegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni Qurani na Hadithi. Wahyi umekuwa ukimjia Mtume na mitume wengine walotangulia kupitia malaika jibril. Lakini zipo njia nyingine ambazo wahyi unaweza kuwajia wanadamu. Njia hizo ni;-
1.Il-hamu
2.Kusemeshwa na Allah (s.w) nyuma ya pazia.
3.Kupitia malaika.
4.Ndoto za kweli.
4.Maandishi.

Qur’an ni maneno ya Allah (s.w) yaliyoteremshwa kwa Mtume (s.a.w) kwa njia ya wahyi kupitia Malaika Jibril (a.s) ili kuwa mwongozo kamili wa maisha ya wanaadamu. Qurani imekuwa ikitambulika kwa majina mengi sana yakiwemo;-
Al-Qur’an – Chenye kuunganishwa pamoja au chenye kusomwa.
Kalamullah – Maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Al-Mas-haf – Mkusanyiko wa kurasa nyingi (Kitabu kikubwa).
Al-Kitabu – Kitabu Pekee (The Unique Book) Kimuundo, Kimaudhui,
Kiusahihi, n.k.
Al-Furqaan – Kipambanuzi baina ya haki na batili.
Adh-Dhikru – Mawaidha au Ukumbusho.
At-Tanziil – Kiteremsho (Mshuko), Wahyi kutoka kwa aliye juu.
Al-Hukmu – Kitabu pekee kinachostahiki kumhukumu binaadamu.
Al-Hikma – Kitabu pekee chenye hikima isiyo na kikomo (Kitabu cha Hikima).
Ash-Shifau – Ponyo au dawa pekee ya kuponya nafsi, nyoyo, uasi, ukafiri, n.k.
Ar-Rahma – Rehema kwa wanaadamu.
Al-Khayr – Kheri pekee, Qur’an ndio chanzo cha kheri zote.
Ar-Ruuhu – Roho ya maisha, asiyeishi kwa mujibu wa Qur’an ni maiti.
Al-Bayaana – Chenye kuweka wazi, kubainisha kila kitu kwa uwazi, n.k.
An-Nuur – Nuru peke ya kumuangazia binaadamu katika njia sahihi ya maisha.
Al-Burhan – Hoja zilizo wazi, zenye kueleweka kwa kila mwenye akili.
Al-Haqq – Kitabu cha Haki, kinachotoka kwa Mola wa Haki kwa ajili ya Kusimamia haki.
Ahsanul-Hadith – Simulizi, maelezo, hadith nzuri kuliko zote.
Al-Hudaa – Mwongozo pekee sahihi wa maisha ya mwanaadamu.

Qur’an ni Kitabu chenye aya 6,236, zilizo katika sura 114 na kimegawanywa katika Juzuu (mafungu) 30. Pia inatupasa tujuwe kuwa qurani kabla ya kumfikia mtume ilipitia hatuwa kuu mbili a,bazo ni;-
Qur’an imeshuka katika hatua kuu mbili;
1.Imeshuka jumla kutoka Lawhim-Mahfuudh (Ubao uliohifadhiwa katika Arshi) hadi Mbingu ya Dunia.
2.Kushuka kidogo kidogo duniani kuja kwa Mtume (s.a.w) kupitia Malaika Jibril (a.s) kwa muda wa miaka 23. Rejea Qur’an (85:21-22), (81:19-20)

Mtume (s.a.w) alianza kushukiwa na wahyi wa kwanza wa Qur’an mwaka 610 A.D akiwa na umri wa miaka 40 katika pango la ‘Jabal Hiraa’. Qur’an ilianza kushushwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Usiku wenye cheo wa “Lailatul – Qadri”. Rejea Qur’an (97:1-5) na (2:185). Ilianza kushuka kwa aya 5 za mwanzo katika suratu Alaq (96:1-5).