Kutokea Kweli Matukio yaliyotabiriwa katika Qur-an

Kutokea Kweli Matukio yaliyotabiriwa katika Qur-an

(vi)Kutokea Kweli Matukio yaliyotabiriwa katika Qur-an:



Ushahidi mwingine unaonesha kuwa Qur-an ni neno la Allah (s.w) ni kutokea mambo kama yalivyotabiriwa hapo awali na Qur-an. Katika mwanzo wa kushuka Qur-an kuna mambo mbali mbali ambayo Mtume (s.a.w) aliahidiwa pamoja na Waislamu kuwa yatatokea hapo baadaye. Pamoja na kuonekana kwa watu kutokuwa na uwezekano kutokea hayo yaliyotabiriwa kulingana na hali halisi iliyokuwapo wakati huo ukweli ni kwamba yalitokea. Kwa mfano, katika siku za mwanzo za Utume, Mtume (s.a.w) na Waislamu waliahidiwa na Allah (s.w) kuwa pamoja na ugumu uliokuwa ukiwakabili na pamoja na udhaifu wa mali na uwezo waliokuwa nao, hali yao itazidi kuwa nzuri siku hadi siku na baadaye watafarijika na kuwa juu ya maadui zao. Ahadi hizi tunazikuta katika aya zifuatazo:


Na bila shaka wakati ujao utakuwa ni bora kwako kuliko uliotangulia,na Mola wako atakupa mpaka uridhike. (93:4-5)


Na kwa hakika baada ya dhiki (huja) faraja. Hakika baada ya dhiki (huja) faraja. (94:5-6)
Tukiangalia maisha ya Mtume na maswahaba wake, ahadi zote hizi zilitimia. Waislamu waliongezeka siku hadi siku na Uislamu ulisimama na kuwa juu ya Dini zote (njia zote za maisha) katika kipindi kifupi cha miaka 23 tu.Mfano wa pili wa utabiri wa Qur-an uliotokea kweli baada ya kipindi kifupi tu ni ule uliotolewa katika suratur-Ruum katika aya zifuatazo:



Warumi wameshindwa katika nchi iliyo karibu (na nchi ya Bara Arabu, nayo ni Sham) nao baada ya kushindwa kwao watashinda, katika miaka michache: Amri hii ni ya Allah kabla (yake) na baada (yake) na siku hiyo Waislamu watafurahi kwa nusra ya Allah (Atakayowapa wao. Nayo ni kuwashinda Makuraishi siku hiyo) (Allah) Humnusuru amtakaye; naye ni Mwenye Nguvu; Mwenye Rehma. Hii ni ahadi ya Allah, Allah havunji ahadi yake lakini watu wengi hawajui. (30:2-6)



Katika mwaka wa sita au saba wa Utume, palikuja habari Makka kuwa Warumi ambao ni watu wa Kitabu (Ahlal-Kitab) wameshindwa vita na Waajemi ambao walikuwa ni washirikina kama washirikina wa Makka. Tukio hili liliwafurahisha sana washirikina wa Makka na kuwaambia Waislamu: "Wakristo, watu wa Kitabu kama nyinyi, wameshindwa na washirikina wenzetu, na hii ni ishara kuwa na sisi hivi karibuni tutakushindeni." Ndipo Qur-an ikatangaza katika aya hizi bishara mbili; bishara ya kwanza ni kuwa katika muda wa miaka tisa Waajemi watashindwa na Warumi na ya pili ni kuwa Waislamu siku hiyo nao watafurahi na kuwacheka Washirikina wa Makka, yaani makafiri wa Makka nao watashindwa vibaya sana na Waislamu. Hivi ndivyo ilivyotokea, kwani katika mwaka 624 A.D. Warumi waliwashinda Waajemi na mwaka huo huo Waislamu 313 walishinda jeshi la makafiri wa Makka lililokuwa na askari 1000 katika vita vya Badr, kwa hiyo ahadi ya Allah(s.w) aliyoitoa katika Qur-an ilitimia. Je hii haithibitishi kuwa Qur-an ni maneno ya Allah (s.w), Mjuzi wa yote yaliyopita na yajayo?



Hebu tuangalia tena mfano mwingine unaoonesha kutokea kweli ahadi alizozitangaza Allah(s.w) katika Qur-an. Katika suratul-Fat-h tunafahamishwa:


Bila shaka Tumekwisha kupa kushinda kuliko dhahiri. (48:1)
Katika mwaka wa 6 A.H. Mtume (s.a.w) na baadhi ya Maswahaba wake walitoka kwenda Makka kufanya Umra (Hija ndogo) lakini walipokaribia kuingia Makka makafiri waliwakatalia kata kata wasiende kufanya ibada hiyo.



Waislamu walikasirika sana mpaka kukaribia kupigana ndipo Allah (s.w) akawateremshia utulivu na wakakubaliana kufanya mkataba wa (Hudaibiya), kisha Allah (s.w) akawaahidi kupata ushindi baada ya muda mfupi. Ndivyo ilivyotokea.



Baada ya miaka miwili tu, na baada ya makafiri wenyewe kuvunja ule mkataba wa amani, Waislamu waliuteka mji wa Makka na kuwa mwisho wa kuabudiwa miungu mingine pamoja na Allah(s.w) katika Nyumba Takatifu (Al-Kaaba) na katika muda mfupi huo watu wengi walisilimu. Je, kutimia kwa bishara hii ambayo iko wazi mno katika historia, haioneshi kuwa haikutolewa na yeyote ila ni yule mwenye elimu ya hakika juu ya yote yaliyopita na yajayo?




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 906

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰3 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰4 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

HUKUMU ZA QALQALA

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al qadir

Asbab nuzul surat al qadi. Hii ni sura ya 97 katika mpangilio wa mashaf. Surat al qadir imeteremshwa Madina na ina aya 5.

Soma Zaidi...
MAANA NA HUKUMU YA TAJWIDI

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
mafunzo ya TAJWID na imani ya dini ya kiislamu

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Quran na sayansi

3; Mchujo wa maji dhaliliKatika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha yakuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalilina pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran??

Soma Zaidi...
Saratul-humaza

Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...