(vii)Mpangilio wa Qur-an:Ukiuchunguza msahafu kwa kina utagundua kuwa si kitabu cha kawaida kama vile wanavyo vitunga wanaadamu. Qur-an pamoja na aya zake kufumwa na maneno ya Kiarabu, pametumika ujuzi usio na mfano katika uchaguzi na mpangilio wa maneno. Maneno yamechaguliwa na kupangiliwa kwa kiasi kwamba huwianisha habari zote zilizoelezwa ndani ya Kitabu na kuufikisha ujumbe kwa wepesi. Mifano michache ifuatayo itatupa picha ya mpangilio wa ajabu wa Qur-an:Kwanza, kutokana na uchunguzi uliofanyika kwa kutumia kompyuta imedhihirika kuwa sura zile zilizoanza na herufi kama Qaf ( )zina idadi kubwa zaidi ya herufi hiyo ukilinganisha na herufi nyingine katika sura hizo.Pili, Kuna sura 114 katika msahafu na kila sura imeanza kwa "Bismillahir-Rahmaanir-Rahiim" isipokuwa Suratut Tawba. Hi huifanya idadi ya "Bismillahir-Rahmaanir-Rahiim" kuwa 113. Lakini katika Suratun-Naml kuna "Bismillahir-Rahmaanir-Rahiim" iliyoletwa katikati ya sura.


Imetoka kwa Suleimani, nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu,Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu." (2 7:30) Hivyo huifanya idadi ya "Bismillahir-Rahmaanir-Rahiim" kuwa 114 sawa na idadi ya sura zote katika msahafu. Je, hii imetokea kwa bahati tu au ni mpangilio wa Mjuzi, Mwenye Hikma.Tatu, kutokana na uchunguzi imedhihirika kuwa maneno mbali mbali katika Qur-an yamerudiwa kwa kuzingatia idadi maalum. Kwa mfano neno "Sema" () limerudiwa mara 332 katika msahafu na neno "Alisema" () limerudiwa mara hizo hizo 332. Pia katika Qur-an zimetajwa "Mbingu Saba" ( ) na maneno haya yamerudiwa mara saba tu katika
msahafu mzima. Kuna miezi kumi na mbili katika mwaka mmoja na neno "Shahr"( )lenye maana ya mwezi limetajwa mara 12 katika Qur-an. Neno "Yaum" ( )katika Qur-an limetajwa mara 365 sawa na idadi ya siku za mwaka mmoja katika mwendo wa jua!Nne, Qur-an inapofananisha jambo fulani na lingine, idadi ya utajo wa mambo hayo kitabuni humo pia huwiana. Kwa mfano katika sura ya 3 aya 59 Qur-an inasema: Bila shaka hali ya Issa mbele ya Allah ni kama ile ya Adam.Alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia kuwa na akawa. (3:59).Adam(a.s) ametajwa mara 25 katika Qur-an. Issa(a.s) vile vile ametajwa mara 25 katika Qur-an. Zaidi ya hivyo katika sura 3:59, Adam ametajwa kwa mara ya saba vivyo hivyo Issa nae ametajwa kwa mara ya saba katika aya hiyo.Adam(a.s) ametajwa katika aya zifuatazo:
2:31, 2:33, 2:34, 2:35, 2:37, 3:33, 3:59 (mara ya saba), 5:27, 7:11, 7:26, 7:31, 7:35, 7:35, 7:172, .17:61, 17:70, 18:50, 19:58, 20:115, 20:116, 20:117, 20:120, 20:121, 36:60.Issa(a.s) ametajwa katika aya zifuatazo:
2:87, 2:136, 2:253, 3:45, 3:52, 3:55, 3:59 (mara ya saba), 3:84, 4:157, 4:163, 4:171, 5:46, 5:78, 5:110, 5:112, 5:114, 5:116, 6:85, 19:34, 33:7, 42:13, 43:63, 57:27, 61:6 na 61:14.


Mfano mwingine ni ule wa sura ya 7 aya ya 176. Qur-an inawalinganisha watu wanaofuata matamanio ya nafsi zao kinyume na aya za Mwenyezi Mungu, kuwa hao ni sawa na mbwa (Kalb).


"Hali yao ni sawa na ile ya mbwa:


Tamko:"Wale wanaokanusha aya zetu( ) limerejewa mara 5 katika Qur-an, na neno "mbwa"() limetajwa mara 5:
Tamko:"Wale wanaokadhibisha aya zetu limetajwa katika aya zifuatazo:7:176 (mara ya kwanza),7:177,21:77, 25:36 na 62:5 (mara ya tano).


Neno mbwa (kalb) limetajwa katika aya zifuatazo: 7:176 (mara ya kwanza), 18:18, 18:22
Aidha Qur-an inaposema jambo au kitu hiki si kama kile idadi ya mambo au vitu hivyo haiwiani katika kutajwa kwake ndani ya Qur-an.2
Kutokana na mifano hii michache ni muhali mwanaadamu kuweza kuandika kitabu chenye mfumo wa maneno, aya na sura mithili ya Qur-an.