Qur-an, vile vile inatufunza mahusiano tunayotakiwa tuwe nayo ili kuondoa chuki na uadui na kupandikiza mapenzi miongoni mwa wanajamii kama tunavyojifunza katika sura zifuatazo:
Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu. Na (ameagiza) kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee, (naye yuko) pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa hishima (kabisa). Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa (njia ya kuwaonea) huruma na useme: "Mola wangu! Warehemu (wazee wangu) kama walivyonilea katika utoto." Mola wenu anajua sana yaliyo nyoyoni mwenu. Kama mkiwa wema (kwa wazee wenu daima; lakini mara moja mbili hivi mkapotea, basi atakusameheni) kwani Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wenye kurejea (kwake). (17:23-25)
Na umpe jamaa (yako) haki yake, na maskini na msafiri aliyeharibikiwa, wala usitawanye (mali yako) kwa ubadhirifu. Hakika watumiao kwa ubadhirifu ni ndugu wa mashetani (wanamfuata Shetani). Na Shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake. (1 7:26-2 7)
Na kama unajipurukusha nao (sasa hivi kwa kuwa huna kitu) lakini unatafuta rehema ya Mola wako (riziki) unayoitumai, basi sema nao maneno laini (ya kuwapa waadi ya kuwa ukipata utawapa). Wala usifanye mkono wako (kama) uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa (ukifanya hivyo) na kufilisika (ukiukunjua ovyo ovyo). (17:28-29)
Hakika Mola wako humkunjulia rikizi amtakaye na humdhikishia (amtakaye). Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona; (anajua yupi anayestahiki utajiri na yupi anayestahiki ufakiri). (17:30)
"Wala msiwaue watoto wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi ndio tunaowaruzuku wao na nyinyi (pia). Kwa yakini kuwauwa ni khatia kubwa. Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo (zinaa) ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa). (17:31-32)
Wala msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha (kuuliwa) isipokuwa kwa haki. Na mwenye kuuawa kwa kudhulumiwa, basi tumempa nguvu mrithi wake. Basi (mrithi ) asifanye fujo katika kuua (kwa ajili ya huyo mtu wake aliyeuliwa). Hakika yeye atasaidiwa (na sharia maadam anayo haki). (17:33)
Wala msiyakaribie (msiyaguse) mali ya yatima, isipokuwa kwa njia iliyo bora mpaka afike baleghe yake (huyo yatima akabidhiwe mwenyewe). Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa (Siku ya Kiama). Na timizeni kipimo mpimapo; na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na bora mwishoni (kwake). (17:34-35)
Wala usifuate usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo; hivyo vyote vitaulizwa. Wala usitembee (usende) katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala huwezi kufikia urefu wa milima. (Basi unajivuna nini). (1 7:36-3 7)
Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza mbele ya Mola wako.(1 7:38)
Haya ni katika yale aliyokufunulia Mola wako katika hikima (zake). Wala usimueke pamoja na Mwenyezi Mungu, Mungu mwengine, usije kutupwa katika Jahanamu hali ya kuwa mwenye kulaumiwa (na) mwenye kufukuzwa (huku na huku). (1 7:39)
Aya hizi zinatufundisha kuwa ili tuweze kuishi vizuri katika jamii hatuna budi kushikamana na maamrisho kadhaa yaliyoainishwa na kujiepusha na makatazo kadhaa.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 685
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 Kitau cha Fiqh
DUA YA 1 - 10
1. Soma Zaidi...
Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Soma Zaidi...
vigawanyo vya elimu
Soma Zaidi...
Kuongea na Allah (s.w) nyuma ya Pazia
Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s. Soma Zaidi...
SHIRK
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...
NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)
Zifuatazo ni njia nyingi za kumjua Mwenyezi Mungu (EDK form 2:dhana ya elimu katika uislamu) Soma Zaidi...
Nguzo za imani
Zifuatazo Ni nguzo za imani
(EDK form 2: elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Sifa za Allah Mwenyezi Mungu
Soma Zaidi...
Kuamini mitume wa mwenyezi Mungu
Nguzo za Imani
(EDK form 2:. Dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...
Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)
Nguzo za Imani
(EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Sifa za waumini zilizotajwa katika surat ash-Shuura
“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele). Soma Zaidi...
Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat
"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi. Soma Zaidi...