image

PHP - somo la 28: Maana ya constant kwenye php na kazi zake

Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya constanta pamoja na matumizi yake. Pia utazijuwa sheria za uandishi wa constant

PHP CONSTANTS

 

Je constants ni nini?

Constant ni jina ambalo hupewa thamani fulani ambayo haitabadilika kwenye script za php wakati zinapofanya kazi. Constants na variable hufanana ytofauti mkubwa ni kuwa, constants hazibadiliki lakini variable hubadilika.


 

Ni yapi matumizi yake:

Constant hutumika hasa kwa zile taarifa ambazo haziwezi kubadilika wakati wa code zinapofanya kazi. Kwa mfano tunatumia constant kwa ajili ya database configuration. Au login ambazo hazihitaji database. Ama unaweza kutumia constatnt popote bale kama mbadala wa variable.

 

Kanuni za kuandika constants:

Unapoandika constant ujuwe kuwa haianzi na alama ya dola $ kama ilivyo variable. Unaweza kuanza na herufi au underscode (_). Pia tunapoandika constants tunaanza na neno define likifuatiliwa na mabano ya kufunga na kufunguwa () mfano define() 

 

Pia unaweza kusema kama constat hiyo inaangalia case-sensitivity, yaani kufuata kamaherufi ni kubwa iwe hivyohivyo na kamaherufi ni ndoo iwe hivyohivyo. Yaani hii ipo hivi, wakati wa kujakuitumia constants endapo hapo mwanzo uliiandika kwa herufi kubwa basi hata wakati wa kuitumia uandike hivyohivyo kwa herufi kubwa. Sasa jambo hili unaweza kuliset.

 

Ndani ya mabano kunakaa jina la constant, thamani ya conctanta, na case sensitivity. Hivyo basi kanuni ya kuandika constant inaweza kufupishwa hivi:-

 

define(jina, thamani, case-insensitive)

 

Mfano 1:

define("chakula", "ugali, nyama na soda");

echo chakula;

?>

 

Kama hapo juu jina la constant ni chakula kwa herufi ndogo. Na wakati wa kuitumia nimetumia hivyo hivyo herufi ndogo. Endapo ningetumia herufi kubwa ingeleta error. Sasa endapo unataka isijali herufi ziwe kubwa ama ndogo utaongeza parameta nyingine kwenye mabano kwa ajili ya kueleza case insensitive.


 

Case sensitivity ipo katika namna mbili eidha iwe true au false. Ukiacha bila ya kuipanga basi itakuwa ni case-sensitive ambayo hufuata hefufikubwa ni kubwa na ndogo  i ndogo.

 

Na endapo utaweka true maana yake ni case-insensitivity hapa haitajali herufi kubwa au ndogo

 

Mfano 2:

define("VINYWAJI", "soda, maji, juisi, kahawa", true );

echo vinywaji;

?>

Iyo inatakiwa ikupe matokeo ya 


 

Ila kwa sasa itakupa error kwa sababu kuanzia toleo la 8 la PHP constants ya namna hii imeondolewa yaani huwezi kuwa na case-insinsitivity. Ila kabla ya hapo ilikuwa inafanya kazi.

 

Mfano 3:

Hapa tutaona jinsi ya kutumia constant ili kuunganisha database, MySQL kwakutumia PHP. Tulisha jifunza kwenye mafunzo ya PHP level 2 jinsi ya kuunganisha database kwa kutumia variable. Sasa hapa badala ya kutumia variable tunakwenda kutumia constants.

 

//Tengeneza constanta

defi">...           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 92


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

PHP - somo la 28: Maana ya constant kwenye php na kazi zake
Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya constanta pamoja na matumizi yake. Pia utazijuwa sheria za uandishi wa constant Soma Zaidi...