Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo kitovuni na dalili zake
SABABU ZA MAUMIVU YA TUMBO KITOMVUNI NA DALILI ZAKE
1.Kuwepo na uvimbe kwenye njia ya chakula (digestive track) kitaalamu hufahamika kama gastroenteritis. Hali hii inaweza kusababishwa na virusi, bakteria ama parasite. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu na yanaweza kuwa ni makali sana. Mara nyingi maumivu haya yanapoa yenyyewe bila hata kuhitaji matibabau ha huondoka ndani ya siku chache. Ila ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
Dalili zakeTofauti na kuwa mgonjwa atakuwa anaumwa na tumbo kwenye kitomvu, lakini tumbo hili litafungamana na dalili zifuatazo:-1.Kuharisha2.Kichefuchefu3.Kutapika4.Homa5.Kutokwa na jasho sana
2.Kuvimba kwa appendix. Maumivu ya tumbo kwenye kitomfu yanaweza kuashiria ugonjwa wa appendix, kitaalamu hufahamika kama appendicitis. Kama utahisi maumivu makali ya tumo kitomvuni kisha ghafla yanahamia upande wa kulia wa tumbo kwa chini, huashiria tatizo hili. Tofauti na kuwepo kwa maumivu haya pia mgonjwa ataona dalili flani.
Dalili za ugonjwa wa appendix1.Kujaa kwa tumbo na kukaza kama mtu aliye vimbiwa2.Kichefuchefu3.Kutapika4.Kuhisi maumivu ambayo huwa yakiongezeka kila unapokohoa ama unapojongea.5.Mvurugiko wa tumbo kama kukosa choo au kuharisha6.Homa7.Kukosa hamu ya kula.
Ugonjwa huu ni katika magonjwa ambayo yanahitajika kutibiwa mapema na haraka sana. Endapo mgo jwa atachelewa kutibiwa appendix inaweza kupasuka, na endapo itapasuka inaweza kuhatarisha maisha.
3.Vidonda vya tumboYes maumivu ya tumbo kitomvuni yanaweza kuwa yamesababishwa na vidonda vya tumbo, huwenda vipo kwenye tumbo la chakula ama sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayotambulika kama duodenum. Tofauti na maumivu ya tumbo kwenye kitomvu pia mgonjwa ataona dalili zifuatazo
Dalili za vidonda vya tumbo:1.mvurugiko wa tumbo2.Kuhisi tumbo kujaa na kucheua3.Kichefuchefu4.Kutapika5.Kukosa hamu ya kula6.Kutoa hewa kwa mdomoni kwa sauti
4.Matatizo kwenye kongoshoHuu ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa kongosho kitaalamu huitwa Pancreatitis. Maradhi haya yanaweza kuja ghafla sana bila ya kuonyesha ishara za awali. Pia zinapoonyesha dalili zake huwa ni kama:-
Dalili za maradhi ya kongosho1.Kichefuchefu2.Kutapika3.Homa4.Mapigo ya moyo kuongezeka
5.Kuwa na ngriri ya heniaUgonjwa huu huwapata wanaume, na hutokea pale ambapo baadhi ya tishu za tumboni zinapoingia kwenye misuli ya tumboni karibu na kitomvu. Kwa watu wazima upasuaji hufanyika ili kutibu tatizo.
6.Kama kuna kizuizi katika utumbo kinachozuia chakula kutembea. Tatizo hili likichelewa kutibiwalinaweza kuwa hatari zaidi. Tatizo hili huweza kusababishwa na:-1.Mashambulizi ya bakteria2.Henia3.Uvimbe4.Kama kulitokea shida wakati wa kufanyiwa upasuaji.
Dalili1.Kichefuchefu2.Kutapika3.Tumbo kujaa4.Kupunguwa maji5.Kukosa hamu ya kula6.Kukoa choo7.Homa8.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
7.Matatizo katika mishipa mikuu ya damu kwenye tumbo (aortic aneurysm). hili ni tatizo la kiafya linalosababishwa na kudhoofu na kutanuka kwa kuta za mishipa mikuu ya damu. Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mtu kama mishipa ya damu itapasuka na kupelekea damu kuingia tumboni, hii inaweza kupelekea maumivu makli. Maumivu haya yanaweza kuathiri na viungo vingine.
Dalili nyingine:-1.Kupata pumzi kwa tabu2.Kushuka kwa presha ya damu3.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo4.Kuzimia5.Udhoifu wa ghafla upande mmoja wa mwili
8.Kama kutakuwa na shida wakati wa mzunguko wa damu katika tumbo (mesenteric ischemia). hii hutokea endapodamu inayotembea kwenye utumbo mdogo itapata usumbufu, kwa mfano ikiganda. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu makali ya tumbo. Maumivu haya huandamana na dalili kama:-1.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo2.Kuona damu kwenye choo
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Ugonjwa wa mdomo unaounguaΓΒ ni neno la kimatibabu kwa ajili ya kuwaka moto mara kwa mara mdomoni bila sababu dhahiri. Usumbufu huo unaweza kuathiri ulimi wako, ufizi, midomo, ndani ya mashavu yako, paa la mdomo wako au maeneo yaliyoenea ya mdomo wako wot
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi visababishi mbalimbali vya ugonjwa wa vericose veini, ni visababishi mbalimbali ambavyo utokea kwenye mtindo wa maisha kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Post yetu ya Leo inaenda kutufundisha kuhusiana na uvimbe wa korodani moja au ambayo kitaalamu huitwa EPIDIDYMITIS. EPIDIDYMITIS ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa kiume wa uzazi. Epididymis ni mrija (tube) uliyoko nyuma ya korodani ambayo mbegu za kiume
Soma Zaidi...Kuna ukimwi na HIV na kila kimoja kina dalili zake na muda wa kuonyesha hizo dalili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maumivu ya kiuno na dalili zake, ni maumivu ambayo utokea kwenye kiuno na kusababisha madhara mbalimbali katika mwili,
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa matibabu kwenye nyonga na kiuno hayatafanyika.
Soma Zaidi...Uchovu wa joto ni hali ambayo dalili zake zinaweza kujumuisha kutokwa na jasho kubwa na mapigo ya haraka, ambayo ni matokeo ya joto la mwili wako. Ni mojawapo ya magonjwa matatu yanayohusiana na joto, huku tumbo la joto likiwa kali zaidi na Kihar
Soma Zaidi...