picha

Utoaji wa zaka katika Dhahabu, fedha ama silva na pesa

Utoaji wa zaka katika Dhahabu, fedha ama silva na pesa

(iii) Dhahabu (gold), fedha (silver) na fedha taslimu (cash)



Miongoni mwa vitu vinavyopendwa na wanaadam ni dhahabu na fedha. Ni vitu hivi walimwengu katika kipindi kirefu cha historia huvitumia kama kipimo cha thamani ya vitu mbali mbali, na ndio vimetumika kama kipimo cha utajiri. Kwa hiyo vimestahiki zaidi kutolewa Zakat:



“... Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari ya adhabu iumizayo” (9:34).


Aya hii inatuthibitishia kuwa kutoa katika njia ya Allah kutokana na dhahabu na fedha (silver) ni lazima kwa Muislamu. Pia fedha taslimu (Bank money or cash) ziko katika mkumbo huu.



Nisaab ya dhahabu, fedha na fedha taslimu na viwango vya Zakat Nisaab ya dhahabu na fedha imeelezwa katika Hadith ifuatayo:



Ali (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Hapana Zakat kutoka kwa Farasi au Punda. Kwa hiyo chukua Zakat ya fedha (silver), dirham moja kwa kila dirham arobaini (1/40). Hapana Zakat kwa dirham 190. Zinapofika dirham 200, basi kuna dirham 5 za Zakat” (Tirmidh, Abu Da ud).



Kutokana na Hadith, kiwango cha Zakat ya dhahabu, fedha (silver) ni Dirham moja. Dirham ni fedha zilizotumika katika baadhi ya nchi za kiarabu tangu wakati wa Mtume Muhammad (s.a.w) hadi hivi sasa. Pia katika Hadith hii tunafahamishwa kuwa Nisaab ya fedha (silver) ambayo ni sawa na nisaab ya dhahabu na fedha taslim ni dirham 200. Tukitumia kipimo cha uzito Nisaab ya fedha ni gram 577.5 au tola 52.5. Nisaab ya dhahabu ni gramu 82.5 au tola 7.5. Muda wa kutoa Zakat ya fedha, dhahabu na fedha taslim ni baada ya kupindukia mwaka mmoja. Kwa hiyo dhahabu, fedha na fedha taslim zitakapowekwa akiba kwa kipindi cha mwaka mzima zikiwa zimefikia thamani ya dirham 200 au zaidi zitatolewa Zakat kwa kiwango cha 1/40 au 2.5%.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: General Main: Post File: Download PDF Views 1927

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

fadhila za sura kwenye quran

FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.

Soma Zaidi...
Lengo la swala

Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake.

Soma Zaidi...