Taratibu za mahari katika uislamu

Taratibu za mahari katika uislamu

Download Post hii hapa

Taratibu za mahari katika uislamu

Mahari



Kabla ya mkataba wa ndoa kupitishwa jambo muhimu ni mwanamke kutaja kiasi cha mahari atakacho penda kupokea kama hidaya au zawadi anayopewa kwa amri ya Mwenyezi Mungu (s.w) kutoka kwa anayemuoa. Uhuru wa kutamka kiasi cha mahari uko kwa muolewaji na bila ya mahari hayo kutolewa taslimu au kwa ahadi ya kulipa baadaye, ndoa haiswihi. Msititizo wa mahari unapatikana katika aya zifuatazo:


Na wapeni wanawake mahari yao, hali ya kuwa ni hidaya (aliyowapa Mwenyezi Mungu). (Lakini hao wake zenu) wakikupeni kwa radhi ya nafsi zao kitu katika hayo (mahari) basi kuleni kwafuraha na kunufaika. (4:4).


"...Na (mmehalalishiwa kuwaoa) wanawake wema wa Kiislamu na wanawake wema katika wale waliopewa Kitabu kabla yen u,mtakapowapa mahari yao, kafunga nao ndoa..." (5:5)



Katika aya hizi tunajifunza kuwa kutoa mahari kuwapa wanawake tunaowaoa ni jambo Ia lazima aliloliamrisha Mwenyezi Mungu (s.w), lakini wenye kuolewa kwa hiari yao wenyewe, wakiamua kuyasamehe mahari hayo au kuyapunguza hata baada ya kutaja, hapana ubaya wowote bali ni jambo zuri pia Ienye kuzidisha mapenzi baina ya mume na mke. Pia mume anaweza kukopeshwa mahari na mkewe akaja kumlipa baadaye.



Lakini kulingana na hadithi ya Mtume (s.a.w) mtu akimlaghai mwanamke kuwa atamlipa mahari hapo baadaye iii akubali wafunge naye ndoa na huku ana nia ya kutomlipa, basi hiyo ndoa haitosihi na huyo mwanamume atahesabiwa kuwa anakaa kimada na huyo mwanamke mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w). Mahari ndiyo inayomuhalalishia mume tendo Ia ndoa kwa mkewe kama tunavyojifunza katika hadithi:



Uqbah bin Amir (r. a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: Jambo ?a msingi katika ndoa ni kwamba utimize kwanza kutoa idle kilichofanya sehemu za sin (za mwanamke) kuwa halali (kwako). (Bukhari Muslim).




                   


Download Post hii hapa

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 849

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰5 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana: