image

Kwa nini lengo la kutoa zaka halifikiwi na watoaji zaka?

Kwa nini Lengo la Zakat na Sadaqat Halijafikiwa katika Jamii yetu?

Kwa nini lengo la kutoa zaka halifikiwi na watoaji zaka?

Kwa nini Lengo la Zakat na Sadaqat Halijafikiwa katika Jamii yetu?Tumejifunza kuwa jamii yenye kudumisha nguzo ya Zakat na kutilia mkazo suala la kutoa mali na huduma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jamii yenye kuendelea kiuchumi na yenye kuishi kwa furaha na amanai ya kweli ya kibinafsi na kijamii. Jamii ya Mtume (s.a.w) na ile ya Makhalifa waongofu ni mfano wa wazi ulio mbele yetu. Jamii yetu hivi leo, pamoja na mahimizo ya utoaji wa Zakat na Sadaqat katika majukwaa mbali mbali bado hatuyapati matunda ya Zakat katika jamii. Miongoni mwa sababu zinazowafanya Waislamu wasipate matunda yanayotarajiwa kutokana na utoaji wa Zakat na Sadaqat ni:(i)Wengi miongoni mwa Waislamu Hawatekelezi Nguzo ya ZakatWengi miongoni mwa Waislamu wenye uwezo wa kutoa zakat hawaitekelezi nguzo ya zakat na hawajihimizi kutoa misaada midogo na mikubwa kwa wale wanaohitajia.
Kwa sababu ya kutotoa Zakat na Sadaqat kwa wale wenye uwezo miongoni mwa Waislamu, kumeipelekea jamii ya Waislamu kuwa duni na dhalili mbele aya Makafiri na Washirikina.(ii)Wengi Watoa Zakat na Sadaqat Hawatekelezi Masharti ya UtoajiMiongoni mwa matajiri wachache wanaojitahidi kutekeleza nguzo ya Zakat na utoaji mali kwa ajili ya kuwasaidia wanaohitajia, hawazingatii masharti ya utoaji.Baadhi ya matajiri hutoa mali zao kwa ria na hufuatilia kwa masimbulizi. Utoaji wa namna hii umefutiwa baraka na hauwezi kumnufaisha mwenye kutoa wala jamii. Ubaya wa kutoa mali au msaada wowote kwa ria na kwa masimbulizi umedhihirishwa wazi katika aya ifu atayo:Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na udhia; kama yule anayetoa mali yake kwa kuwaonesha watu, wala hamwamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho. Basi hali yake ni kama hali ya jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha ikalifikia (jabali hili) mvua kubwa (likasukuma udongo wote huo) na ikaliacha tupu. Basi haw atakuw a na uw ezo (wa kupata) chochote katika walivyovichuma; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri”. (2:264)Kuna baadhi ya miongoni mwa Waislamu matajiri wanaotoa Zakat bila ya kuzingatia wale wanaostahiki (Rejea Qur-an, 9:60). Badala yake huenda na kapu la fedha msikitini na kumgawia kila mtu atakayekuwa tayari kupokea. Ugawanyaji huu wa Zakat hupelekea kupewa wasiostahiki na kuwakosesha wanaostahiki na kuwabakisha katika dhiki yao. Utoaji wa namna hii huibakisha jamii ya Waislamu katika dhiki na katika uadui na uhasama. Kuna baadhi ya Waislamu pamoja na kutoa Zakat na Sadaqat, hawazingatii mipaka ya halali na haramu katika uchumi wao. Wengine huchuma kwa njia za haramu ambazo hazinufaishi jamii bali huiingiza jamii katika matatizo ya rushwa, riba, kamari, wizi, ujambazi na udhalimu wa kila namna.(iii) Zakat haikusanywi na Kugawanywa Kijamii
Tumejifunza kuwa utoaji na ugawaji wa Zakat, ili unufaishe jamii hauna budi kusimamiwa na jamii. Lazima jamii ya Kiislamu iwe na watu maalum wanaopita kwa kila Muislamu mwenye uwezo wa kutoa zakat, na kuipokea Zakat yake kisha kuikabidhi kwa Mtunzaji wa Baitil-Mali (Mhazini), kisha kuigawa kwa wanaostahiki.
Sehemu kubwa ya jamii ya Waislamu hivi leo, haifuati utaratibu huu wa ukusanyaji na ugawaji wa Zakat na sadaqat bali kila mwenye kutoa Zakat huigawanya mwenyewe kwa wale wanaostahiki walio machoni mwake. Kuacha Zakat mikononi mwa watoaji binafsi, kuna hasara kubwa zifuatazo:Kwanza; hapitiwi na mhimizo wa makusudi juu ya utoaji wa Zaka, kiasi kwamba wenye kustahiki kutoa Zakat hujisahau na hatimaye kuacha kutoa Zakat kabisa.Pili; kwa kutokuwa na utaratibu wa ugawaji, sehemu kubwa ya Zakat hupewa wasiostahiki na wale wanaostahiki hubaki na dhiki yao.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 541


Download our Apps
πŸ‘‰1 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰2 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Njia haramu za uchumi
Soma Zaidi...

Jinsi ya kutekeleza funga za sunnah
Hapa utajifunza muda wa kutia jia katika funga za sunnah. Pia utajifunza kuhusu uhuru ulio nao Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

mambo yanayofungua swaumu
post hii ijakwenda kukufundisha mambo yanayoharibu funga Soma Zaidi...

Vipi utapata uchamungu kupitia funga
Vipi lengo la funga litafikiwa na kumfanya mfungaji awe mchamungu. Soma Zaidi...

Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za Kirumi hapo zamani
(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu. Soma Zaidi...

Watu wanaolazimika kufunga mwezi wa Ramadhani
Hapa utajifunza watu ambao wanalazimika kufunga mwezi wa Ramadhani. Soma Zaidi...

Swala ya jamaa na mnamna ya kuswali swala ya jamaa, nyumbni, msikitini na kwa wanawake
Soma Zaidi...

Sharti za kusihi kwa funga
Soma Zaidi...

Ni ipi hukumu ya muislamu anayekula mwezi wa Ramadhani bila ya sababu ya kisheria
Endapo muislamu hatafunga mwezi wa Ramadhani bila ya ruhusa je atatakiwa afanye nini. Je ataweza kuilipa funga hiyo? Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...