Kwa nini Funga imefaradhishwa Mwezi wa RamadhaniJapo tumefahamishwa katika Qur-an kuwa, faradhi ya funga ni kwa umma zote hatufahamu umma zilizotangulia zilifaradhishiwa kufunga miezi gani au wakati gani wa mwaka. Umma huu umefaradhishiwa kufunga katika mwezi wa Ramadhani kwa sababu ndio mwezi ilipoanza kushuka Qur-an kama tunavyofahamishwa katika aya ifu atayo:


“(Mw ezi huo mliofaradhishw a kufunga) ni mw ezi w a Ramadhani ambao ndani yake imeshuka hii Qur-an ili iwe uongozi kwa watu na hoja zilizowazi


za uongozi na upambanuzi. Atakayeshuhudia mwezi huu miongoni mwenu na afunge ....” (2:185).
Hivyo, Waislamu wameamrishwa kufunga katika mwezi wa Ramadhani ili pamoja na kutekeleza amri hii wafikie lengo lililoku su diwa, vile vle iwe ni kumbukumbu ya kushuka Qur-an, Mwongozo wa Allah (s.w) wa mwisho kwa wanaadamu. Ni kwa msingi huu kusoma Qur-an kwa wingi katika mwezi huu kumesisitizwa zaidi. Qur-an ilianza kumshukia Mtume (.s.a.w) alipokuwa Jabal-Hira, usiku wa manane katika usiku mmoja wa Mwezi wa Ramadhani. Usiku huo mtakatifu ni “Lailatul’qadri” (Usiku Wenye Cheo) kama tunavyojifunza katika Suratul-Qadr.


Hakika Tumeiteremsha (Qur’an) katika usiku w a Laylatul Qadri. Na jambo gani litakalokujulisha ni nini huo usiku wa Laylatul Qadri? Huo usiku wa heshima ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na roho katika (usiku) huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo. Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri(97:1-5)