23. Kuwa mwenye HurumaMuumini hana budi kujipamba na tabia ya kuwahurumia viumbe wenzake. Amuoonee huruma kila mwenye shida na ajitahidi kumsaidia iwezekanavyo. Katika kuonesha umuhimu wa kipengele hiki cha tabia njema Mtume (s.a.w) amesema:“Ambaye hahurumii watu, pia Allah (s.w) hatamuhurumia ”. (Bukhari).
Huruma hudhihiri katika kuwasaidia wenye shida na matatizo kwa mali na kauli njema kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Hamtaweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vitu mnavyovipenda, na chochote mnachokitoa, basi hakika Allah anakijua ”. (3:92).


“Sio wema (tu) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi. Bali wema (hasa) ni (wale) wanaomwamini Allah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, w anawapa mali, juu ya kuwa wanayapenda, jamaa na mayatima na maskini na wasafiri (w alioharibikiwa) na waombao na katika kuwakomboa watumwa...” (2:177


“… Na wafanyie wema wazazi na jamaa na yatima na maskini na semeni na watu kwa wema…” (2:83).
Pamoja na kuonyesha huruma kwa wanaadam wenzetu, Uislamu pia umetutaka tuwe na huruma kwa wanyama. Tunafahishwa katika hadith kuwa mtu mmoja alimuambia Mtume:Ee Mtume w a Allah! Ninapochinja mbuzi ninajaribu kumuonea huruma. Mtume (saw) akasema: “Kama utamuonea huruma , Huruma ya Allah itakuwa juu yako”. (Hakim)
Pia katika hadith nyingine Mtume (saw) amesema:“Mwanamke mkosefu alimuona mbwa akiwa anachungulia kisima, siku ya joto kali na ulimi wake ukiwa umening’inia kuonyesha kiu kali aliyokuwa nayo. Alimuonea huruma na akamtekea maji na chombo chake. Kutokana na kitendo chake hiki (cha kumuhurumia mbwa), alipata uokovu”. (Muslim)
Pia Hadith ifuatayo inatuonyesha kuwa waislam wanatakiwa


wanyooshe mkono wa huruma kwa viumbe vyote vilivyo hai. Mtume (saw) amesema:
“Wahurumie waliomo ardhini, na yule aliyopo mbinguni atawamiminia huruma yake”Kinyume chake kuwa katili kwa wanyama ni kitendo cha dhambi kinachoweza kumuingiza mtu motoni. Mtume (saw) amesema:
Mwanamke alitiwa motoni kwa sababu alimfunga paka bila ya kumlisha au kumwachia huru, ambapo angaliweza kwenda huku na huku na kujilisha kutokana na wadudu , n.k. (Bukhari)
Kutokana na Hadith hizi tujue kuwa Allah (sw) hata turehemu iwapo tutakuwa wakatili kwa wanaadamu wenzetu na viumbe wengine.