Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Saumu (Funga).
Umuhimu wa swaumu (Funga) katika Uislamu.
Funga ya mwezi wa Ramadhani ni nguzo ya nne katika Uislamu.
Funga ya mwezi wa Ramadhani ni faradhi kwa waislamu wote na ni miongoni mwa nguzo za Uislamu baada ya shahada, swala na zakat.
Rejea Quran (2:183).
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni utambulisho wa Uislamu wa mtu.
Mtu akiacha nguzo hii kwa makusudi ni sababu na ishara tosha ya kutoka katika Uislamu.
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni utambulisho wa Ucha-Mungu wa mtu.
Funga ya Ramadhani na sunnah zingine ni kielelezo cha Ucha-Mungu wa muislamu zikitekelezwa vilivyo.
Rejea Quran (2:183).
Kutofunga mwezi wa Ramadhani makusudi hupelekea kukosa msamaha.
Muislamu asipofunga mwezi wa Ramadhani makusudi basi, hukosa msamaha, na rehma na hustahiki adhabu za Mwenyezi Mungu (s.w).
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni faradhi (amri) kwa waislamu wote isipokuwa wenye udhuru.
Rejea Quran (2:183).
Umeionaje Makala hii.. ?
Mtume amemfundisha kuwa watoto wafundishwe kuswali wakiwa na miaka saba na waadhibiwe wakiacha wakiwa na miaka 10
Soma Zaidi...Post hiibitakugundisha hekima ya kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja katika sheria za kiislamu.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mambo haya yanaweza kuharibu funga ya mtu ama kupunguza malipo ya funga.
Soma Zaidi...