Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine.
1. Eda ya kuachwa mwanamke ni twahara tatu au miezi mitatu kwa wasiopata hedhi.
2. Eda ya mke mwenye mimba, huisha atakapojifungua.
3. Eda ya mke aliyefiwa ni miezi minne na siku kumi (siku 130).
Hekima ya Kukaa Eda
- Ni kuwapa wawili (mume na mke) fursa na muda, huenda wakasuluhishana na kurejeana na kuendelea na maisha ya ndoa yao.
Rejea Qur’an (65:1)
- Ni kuthibitisha uhalali wa mtoto wa mume wa mwanzo asijepewa mume atakayefuatia.