Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 10: Ndoa ya binti mfalme na Sinbad

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo......

NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME.

 

Siku hazikuenda kipolepole hatimaye wiki ikafika na harusi ikafanyika. Sherehe kubwa isiyo na kifani ilifanyika na hata wafalme wa jirani walihudhuria. Niliozeshwa binti yule na kukabidhiwa nyumba ndani ya ikulu. Nilipata kukabidhiwa na mali na mambo mengine kadhaa. Sherehe za kimila pia zikafanyika kwa ajili ya kukabidhiwa cheo cha mfalme ajae yaani baada ya kufa mfalme huyu nitakuwa mfalme mpya. Yote haya yalifanyika japo sikuwa na furaha nayo.

 

Ni miezi miwili sasa imefika na mishaanza kuzoea mazingira ya kulinda muda wote na kuzungukwa na watu. Nilitembelea uwanja wa kujifunzia farasi nikakuta watu wanaendesha farasi bila ya kuweka kiti chha farasi. Basi nikatumia taaluma nilonayo na kuwatengezea viti vya farasi. Jambo hili lilifanya nipendwe sana na watu na mawaziri kwa kuleta kitu kipya zaidi. Mapenzi ya mfalme na mimi yalizidi kuongezeka siku hadi siku. Watu walikuwa wakinikubali sana hasa ninapokuwa nawasimulia hadithi za kuhusu baghadad na safari za majini na mikasa iliyowahi kunikuta.

 

Ni miezi mitano sasa toka kumuoa binti mfalme. Binti mfalme alinipa habari za furaha kuwa ana ujauzito. Nilizipeleka habari zile kwa babamkwe na mama mkwe. Kwa hakika siwezi kusimulia namna ambavyo furahayao ilivyokuwa. Habari ziliwafikia mawaziri na watu wengine. Wote walikuwa wakiniupongeza. Binti mfalme alizidi kuniona mimi ni mtu muhimu sana kwenye maisha yake kwa kumfanya awe mama mtarajiwa wa familia ya mifalme.

 

Hatimaye miezi ya kujifunguwa ya binti mfalme imefikia na sasa amepelekwa kwa wakunga. Nikiwa nipo mlangoni kusubiria habari za furaha nilishitushwa na kilio kikubwa sana kilichotoka ndani. “Innaa lillahi wa innaa ilaihi rajiun” niliposikia maneno haya yakisemwa nikajua mtoto wangu amefariki dunia. Nilianza kulia sana, na muda si mrefu mkunga mmoja akatokea nje na kuniambia kuwa binti mfalme amefariki dunia na mtoto wake amepona. Nililia zaidi na kutamani ardhi inifukie.

 

Furaha za kupata mtoto sikuweza kuzipata kamwe nikikumbuka kuwa nakwenda kuzikwa na me wangu. Mila haikuwacha kufuata mkonowake sasa mwili wa marehemu ukawa unaanza kuandaliwa na nikamuona baba mkwe akija kwa unyonge na kunipa maelekezo na kunipatia nguo mpya na kuniambia hizi zitakuwa ndio sanda yako. Sina la kukusaidia lamba nitakuongezea mkate wa nane. Maana huwa aliye hai anapozikwa na mwenza anapewa kichupa cha maji na mkate mikate 7 hivyo nitakupendelea kukupa mikate nane.

 

Maneno haya yaliendelea kuniumiza hasa pale watu walipokuja kunihani na kuniaga kwa mara ya mwisho. Sasa ndipo nikaanza kujuta kukubali kutembea majini safari hii. Nilitamani hata ningekuwa kama wale wenzangu nilowaaza kule wanachinjwa maana taabu nitakayoiona na kuzikwa nikiwa hai ni kubwa. Basi likaandaliwa jeneza moja kubwa sana na mimi na mke wangu tukaingizwa na kubebwa kuelekea mazikoni. Walikwenda kwa muda wa masaa 2 na nusu kisha wakaanza kupandisha juu kwa mwendo wa nusu saa. Nikawasikia wanazungumza kuwa wamefika tayari.






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 09:39:52 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 107


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 21: Kinyozi mwenyewe
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 13: Sehemu ya sita ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa safari ya Sinbad iliyopo ndani ya kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 8: Simulizi ya chongo wa tatu mtoto wa mfalme
Muendelezo wa hadithi ya mtoto wa mfalme mwenye chongo katika hadithi ya HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 11: Vidole gumba vilikatwa
Kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA kina simulizi nyingi nzuri na za kusisimua, muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 14: Jaribio la pili kwa Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 19: Mfalme na waziri wake
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 15: Mji uliogeuzwa mawe
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Taharuki kwa mfalme
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 12: Dirisha moja kwanini????
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hadithi ya Nurdini Mtoto wa Waziri
Hii ni hadithi ya kitabu cha tatu cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 22: Kaka wa kwanza wa kinyozi
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 2: Sultani mtoa buradani kufariki
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili..... Soma Zaidi...