Muendelezo....
HADITHI YA KAKA WA KWANZA WA KINYOZI
Kaka yangu alikuwa ni mshona charakani maarufu sana. Alipokuwa amekaa ofisii kwake siku moja akiwa anaangalia dirishani kwa bahati nzuri alimuona mwanamke mzuri sana. Mwanamke yule alikuwa akizugumza na mwenziwe. Kwa muda kadhaa kaka yangu alikuwa akimwangalia yule mwanamke. Kumbe na yule mwanamke alikuwa akimwangalia kaka kwa kujiiba. Basi yule mwanamke alipomaliza mazungumzo yake akamwangalia kaka kisha akamkonyeza na kupotelea mtaani. Muda wote ule kaka yangu hakweza kufanya kazi kwa ufanisi kwakumuwaza.
Bila ya kutambua mambo yalivo, kaka yangu alianza kumpenda yule mwanamke bilia kujuwa kumbe yule mwanamke alikuwa ni mke wa mtu. Siku ilofata kaka alipokuwa akishona alikuwa nmambo na akili yake yote ipo dirishani kuangalia kama atamwona yule mwanamke. Mara yule mwanamke akaja akiwa ameongozana na kijakazi chake. Kijakazi wake alikuwa ni binti wa makamo mwenye sura nzuri. Uzuri wake kamwe haukumfikia mwanmke yule.
Yule mwanamke alizogea jirani na kwa kaka anaposhona, kisha akawa anazungumza na baadhi ya wanawake wenzie. Wakati huo kaka aliacha kushona kabisa, kwa kumuangalia mwanamke yule. Wakati huo yule mwanamke alikuwa akimwangalia kaka kwa kujiiba huku akimkonyeza, na kumuoneshea ishara kwa vidole. Haukupita muda yule mwanamke akaondoka zake. Kaka alichanganyikiwa na kuacha kushona kabisa. Aliondoka na kweda nyumbani kulala ili apunguze mawazo.
Loo! Usingizi haukumpata hata kidogo, kwa mawazo na hisia aliendelea kuumia tu kitandani. Hatimaye usiku ukaingia na asubuhi ikang’ara tena. Kaka hakuweza kupata hata lepe la usingizi wala kugusa chakula. Mapema asubuhi kaka aliwahi kufungua ofisi na kuanza kusubiri wateja, angalau apate japo pesa ya kumuwezesha kupata chakula. Mteje wa kwanza kuja alikuwa ni yule kijakazi wa yule mwanamke. Kaka alijuwa kuwa kutakuwa na habari za furaha.
Kijakazi alikuja na vipande saba vya vitambaa kisha akamwambia kaka kuwa bosi wangu anataka umshonee magauni 7, na itakuwa vyema kama yakikamilika leo hii. Kaka alifunga ofisi ili kuzuia wateja wengine wasije. Hapo akajifungia na kuanza kushona. Nguvu ya mapenzi ilimteka vilivyo, bila kujali njaa aliyo nayo. Kwa kuwa kaka ni mtu wa maneno mengi akaanza kueleza hisia zake kwa huyu kijakazi ili azifikishe kwa mwanamke yule.
Kwa uwongo kijakazi akasema kuwa hata bosi wake yaani yule mwanamke ameshindwa kulala kwa kumuwaza yeye. Ukweli ni kuwa kulikuwa na agend ya siri kwa mwanamke huyu na kijakazi wake. Mpaka kufika jioni kaka alishamakiza kushona nguo zote na tayari akamkabidhi kijakazi. Kaka akaendelea eti ufungua ofisi na kusubiri kama kutakuwa na wateja. Loo aliambukia mtu mmoja aliyetaka kuwekewa kiraka kwenye kanzu yake. Kaka aliambukia pesa kidogo ya kununua matunda.
Ukweli ni kuwa yule mwanamke alimueleza mume wake kuwa kuna mshona nguo anamtaka. Hivyo mwanamke yule akapanga njama ili wamchune. Walipanga njama hii na mipango ilipotimia mwanmke yule akapanaga akutane na kaka mule ofisini kwake. Mbinu yao ni kuwa baada ya wawli kukutana wanataingia kundi la watu na kuja kumfumania. Matokeo yake ni kuchukuwa kila kilichopo ndani. Baada ya mipango kukamilika yote wakaagana na kundi la vijana mabarobaro na mipango ikatekelezwa.
Ilikuwa ni siku ya baada ya juwa kuzama, kaka aliagana na mwanamke yule kukutana pale ofisisni. Siku hiyo kaka alikwenda saluni kushevu nywele zake na kuchonga ndevu zake na kuzilinganisha sawasawia. Baada ya kusubiri kidogo, kaka akaanza kupata harufu ya manukato, kamwe hajapatapo kuivuta harufu hii kwa uzuri ulioje. Zura illiyo ya kuvutia ikaanza kuonekana ikichomoza kupitia mlango wa nyuma wa ofisi ya kaka kama walivyoagana. Kwa furaha kaka akaenda kumpokea kwa madaha na tayari kuazimia kufanya walilokusudia.
Haukupita muda ndipo mlango ukagongwa kwa nguvu, hata kabla ya kufungua mlango ukavunjwa. Loo ni kundi la vijana likidai kumfumania kaka na mke wa mtu. Kaka alijitetea lakini wapi, walimpiga sana maeneo mengi ya mwiili wake na wakampiga kichwani. Kaka akapoteza fahamu. Walichukuwa kila kilichop ofisini. Kisha wakamtia kaka kwenye kari la kuburuta kwa wanyama na kwenda kumtupa mbali sana. Kaka aliathiriaka kwenye kichwa na kupoteza kumbukumbu na akilli yake haiposawa kuanzia siku hiyo.
Basi nilitoka na kwenda kumtafuta kwa siri na kwenda kumchukuwa. Haya ndiyo yaliomkuta kaka yangu wa kwanza, kutokana na maneneo yake mengi na kutokuwa na weledi mwema wa dini. Sasa ngoja nikusimulie kilichomkuta kaka yangu wa pili ambaye ni kipofu na jinsi alivyoupata upofu katika mazingira ya utata.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:22:08 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 130
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 14: Simulizi ya binti wa kwanza na mbwa
Tuendeleee kuburudika na simulizii zetu nzuri kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 10: Jumba la Aladini
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 9: Hadithi ya deni la mapenzi
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 8 Part 3: Kijana mchonganishi
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 2: Sehemu ya safari ya kwanza ya sinbad
Muendelezo wa stori ya safari ya Sinbad ambayo ipo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 8: Harusi ya aladini kufanyika na binti wa mfalme
Muendelezo...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 14: Wageni
Simulizii hii ni nzuri na ni mojawapo ya hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 13: Jaribio kwa Aladini kwa mara ya kwanza
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 27: Kaka wa sita wa kinyozi
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 11: Kisa cha Kalid na Jalid
Tuendelee kusikiliza na kusoma visa, hadithi, na simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza tuwe pamoja mpka mwisho...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 13: Sehemu ya sita ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa safari ya Sinbad iliyopo ndani ya kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 10: Ndoa ya binti mfalme na Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo...... Soma Zaidi...