Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 18: Hadithi ya fundi cherehani

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.....

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MSHONA NGUO (FUNDI SHERAHANI)

 

 

Jana tulikuwepo kwenye sherehe moja ya wafanyabiashra. Mmoja kati ya wafanyabiashara alikuwa na sherehe yake, nayo ni nadhiri aliyoiweka pindi mambo yakiwa safi atalisha watu bure kwa masaa machache ya siku. Katika sherehe hiyo ilipofanyika chakula kizuri kiliandaliwa. Niliwaza hata kuchukuwa chakula niende nikampatia mkewangu naye apate kuonja vitamu, vilivyoandaliwa na mfanyabiashara.

 

 

Sikuwa na mtoto hivyo chakula kidogo kingemtosha mke wangu kipenzi kutuliza hamu yake. Kama ilivyo ni kawaida hatukupewa viti vya kukalia bali mazulia mazurimazuri yaliyopambwa vyema yalitandikwa. Waungwana na watumwa tukajiweka vyema na kuandaa matumbo yetu kwa kinacholetwa. Mazulia yalitandikwa kwa mpango wa duara na katikati ndipo kulikuwa na meza kuu.

 

 

Zulia lililopo kati lilikuwa ni bora, zuri na lenye thamani kubwa. Kimoyoni nilijisemea “kweli itifaki imezingatiwa”. zulia hilo la meza kuu liliandikwa maneno ya kiarabu yaliyonyooka vyema kama mapambo ya mauwa. Rangi ya manjano ilikolea mithili ya dhahabu ya Moroko. Lilipata kubonyea zulia hili midhili ya godoro, hata nikastaajabu uzito ulioje wa zulia hili. Nilitamani niengeliona wakati linatandikwa. Ila nikajiridhisha badala ya kuliona lipo kwenye vipande vilivyoungwa vyema.

 

 

Muda haukukawia sana mnawishaji akapita na kutoa maelekezo kuwa wawiliwawili ndio mpango wa kula. Nilikuwa na mwenzangu ambaye alikuwa akijishughulisha na shughuli za unyoaji yaani kinyozi. Alikuwa amevaa vyema na mavazi yamemkaa sawiya. Muda wote hakuwacha kutabasamu utadhani amebebeshwa gunia la furaha. Nilitamani sana kuwa kama yeye hasa ilipoona uso wake ulio mkunjufu usio na mikunyo kama anayekula ndimu.

 

 

Nilitamani niwenaye karibu, nipate kujuwa ni manukato gani anatumia, lakini sikufanya hivyo. Wakati haya yote yakiendelea nikathubutu kuchungulia kwa ndani kwa furaha niliona sahani zinaletwa. Sahani za vyakula ziliongozana na waheshimiwa waliopaswa kukaa kwenye zulia la wageni maalumu. Katia msafara huo ilionyesha kweli ni msafara wa wafanya bishara. Kwa mavazi, walipendeza vyema. Wakina ni vijana watatu na mzee wa makamo mwenye ndevu nyeupe na nyeusi..

 

 

Walipofika mlangoni wakasimama kuangalia hadhara, wakati huo wanaongea na mwenyeji wa shughuli. Wakiwa wao wanazungumza huku tayari vyakula vilianzwa kugawiwa. Sinia kubwa liliwekwa mbele yetu. Ndani ya sinia hili kulikuwa na vyakula pamoja na vinywaji. Nyama za kuoka na kupikwa vyema, vyakula vipendwavyo pamoja na michuzi mizito. Mikate iliyopikwa vyema na mchuzi wa kutowea. Juisi ya matunda yaliyochujwa vyema, uzitowake utadhani ni asali mbichi iliyokaa siku 10 ndani ya mtungi. Kwa ukarimu walio nao maji ya kuywa yalikuwa ni maji kutoka Miji mitakatifu.

 

 

Wale wageni badala ya kuzungumza kidogo wakaanza kuelekea kwenye kikalio chao. Sasa kijana mmoja kati ya wale wageni akakunja sura kwa ghafla, kanakwamba amechanganyikiwa badala ya kuona kitu cha ajabu sana. Haya yote yalitokea badala ya yeye kuangalia upande ambao mimi na wenzangu tuliuwa tumekaa. Watu walipatwa na shauku ya kutaka kujuwa nini kimemtokea mbele za watu pale. Yule kijana ikaonekana anataka kuondoka kwenye shughuli ile. Mwenyeji alionekana kumsihi sana asiondoke lakini wapi.

 

 

Kumbe sikuwa mimi tu bali tulikuwa wengi ambao tulikuwa tukifatilia kwa ukaribu tukio lile. Watu walio karibu wakatika kujuwa hasa kwa nini mgeni wetu anataka kuondoka. Hapo mwenyeji wa shuguli akamuomba aeleze kitu ambacho hakukifurahia. Kijana yule akasema kuwa hapa nimeoa mtu ambaye niliapa katika maisha yangi kuwa sitakaa naye sehemu moja, mji mmoja wala nchi mmoja. Kisha akamuonyesha yule kinyozi. Watu wakataka kujuwa hasa ni kitu gani kilitokea kati yao. Kijana akasema kuwa huyo kinyozi ndio sababu ya yeye maisha yake kuwa vululu, kuvunjiaka mguu na mabaya makubwa mengi yalimpata kwa sabbu ya kinyozi. Kisha kijana akaanza kusimulia hasa kilichotokea kati yao:-






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:18:51 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 113


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 10: Mapenzi kwenye mtihani
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 20: Kinyozi maishani mwangu
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 16: Kitabu cha ajabu
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 5: Bonde la uokozi
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza....... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 6: Hadithi ya mwenye kutabiriwa mtoto wa tajiri
Tunapfatilia simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizi hii imetoka ndani ya kitabu cha kwanza karibuni tuendelea kupata skmulizi nyingi za kusisimua ..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 20: Waliodhulumiwa kufanyiwa suluhisho
Ni mojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 6: Hadithi ya ugeni wa dhati
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 7: Taharuki
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 3: Kisa cha mke na kasuku
Simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizii hii inasimulia kisa cha mke na Kahuku wake.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Rafiki wa ukweli
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 4: Sehemu ya pili ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 13: Jaribio kwa Aladini kwa mara ya kwanza
Muendelezo.... Soma Zaidi...