Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
MAWAKALA WA MARADHI (PAHOGEN)
Hawa tumesema ndio mawakala wakubwa wa kuambukiza maradhi. Hawa husababisha maradhi haya ya kuambukiza. Wapo aina nyingi lakini tunaweza kuwagawanya katika bakteria, virus, fungi, protozoa na parasites.
1.Bakteria
Hawa ni vijidudu vidogo sana ambavyo haviwezi kuonekana kwa macho maavu bila ya kutumia hadubini (microscope). Vidudu hivi vina seli moja tu. Wapo bakteria ambao hawasababishi maradhi na wapo a,mbao husababisha maradhi. Bakteria karibia dunia nzima wamejaa na hata sehemu ambazo zana mabarafu bakteria pia wapo. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kuna aina zisizopungua 300 za bakteria ambao wanaishi kwenye mdomo wa binadamu. Ila karibia bakteria hawa wote hawana madhara kwetu kwa upande mwengine wengi wao ni msaada na ni faida kwetu.
Mfano mzuri ni kuwa kwenye utumbo mdogo kuna bakteria ambao wanatengeneza vitamini ambavyo ni msaada kwa afya zetu. Pia ijulikane bakteria wengine wana madhara makubwa wakiwa ndani ya miili yetu kwa mfano baktria aina ya tuberculosis hawa husababisha kifua kikuu. Tetanus hawa huleta tetenasi. 2.VIRUSI
Virusi ni vidogo zaidi kuliko hata bakteria. Virusi ni vijidudu vidogo sana ambavyo vyenyewe vina genetic material na protein coat. Genetic material ni chembechembe zinazowafanya waweze kuzaliana. Virusi vinaweza kushi tu kama vipo ndani ya kiumbe hai. Vyenyewe vinaweza kuzaliana kwa kutumia seli za kiumbe hai ambapowamo. Maradhi ya Ukimwi, mafua ni baadhi tu ya maradhi ya virusi.
3.FUNGI
Hawa huwa tumezoea kuwaita fangasi hawa wanakula kwenye seli za kiumbe hai. Mfano mzuri ni uyoga huu ni katika jamii ya viumbe hawa wanaokula kutokana na seli au kiumbe kilichokufa. Kama bakteria hata wadudu hawa wapo wanasababisha maradhi na wengine hawasababishi. Fangasi wa miguuni ni mfano mzuri wa maradhi ya wasudu hawa. Mfano mwengine ni wale wa sehemu za siri wanaopelekea kuchubua kwa koreodani kwa wanaume na madahra menginey wa wanawake.
4.PROTOZOA
Hawa pia ni vijidudu vidogo visivyoonekana kwa macho makavu. Hawa pia wana seli moja tu katika miili yao. Ila hawa ni wakubwa kuliko bakteia. Hawa wanasababishwa magonjwa ambayo yanaongoza kuuwa watu wengi sana dunianii. Kwa mfano malaria husababishwa na vijidudu hivi. Kwaribia watu milioni moja kila mwaka wanakufa kwa malaria katika nchi zilizopo kwenye uoto wa tropic.
5.PARASIT
5.Hawa ni wadudu wanaokula kiumbe hai. Mfano mzuri ni chawa, kupe, mbu na wengineo wenye mfano huu. Wadudu hawa wanajipatia chakula kwa kunyonyo viinilishe kwenye mwili wa kiumbe hai. Hawa wanaweza kuwa nche ya mwili kama chawa au ndani ya mwili kama minyoo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Simulizi yetu ya leo tutajifunza kuhusu faida za kiafya za kufunga kwa mtazamo wa kitabibu, kama anavyoeleza daktari. Tutaangalia namna kufunga kunavyoathiri na kusaidia viungo na mifumo mbalimbali ya mwili. Somo letu la leo litahusuโฆ faida za kiafya za kufunga katika figo, moyo, ini, mfumo wa kinga, kisukari, presha ya damu na mmengโenyo wa chakula.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kuzinuwa faida za kufunga kitaalamu. Hapa hatutaangalia mtazamo wa dini yeyote
Soma Zaidi...Endapo tezi dume haitatibiwa ama itachlewa kutibiwa basi mtu anaweza kupata madhara. katika post hii utakwenda kuyajuwa madhara ya tezi dume kwenye Mwili
Soma Zaidi...