picha

Dalili za kifua kikuu kwa watoto.

Posti hii inahusu zaidi dalili za kifua kikuu kwa watoto,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto pindi wanapopata Maambukizi ya kifua kikuu.

Dalili za kifua kikuu kwa watoto.

1.Kifua kikuu ni Ugonjwa unaowashambulia Watu wazima na watoto kwa hiyo Dalili uweza kupelekea a ila mtu mzima anaweza kujieleza wazi jinsi anavyojisikia kuliko mtoto kwa hiyo ili kujua Dalili za kifua kikuu kwa watoto tunapaswa kuangalia yafuatayo kwa watoto.

 

2. Mtoto kukosa raha au kulia lia.

Hii ni mojawapo ya Dalili ya kifua kikuu kwa watoto kwa sababu mtoto anakuwa anajisikia vibaya na hawezi kusema kwa hiyo ataonekana hana raha na kuanza kulia lia ingawa hii inaweza kuwa ni Dalili ya hata Magonjwa mengine lakini dalili hii ikiambatana na Dalili nyingine za kifua kikuu kama tutakavyoona ni kifua kikuu mtoto anapaswa kupelekwa hospitalini kwa uangalizi zaidi.

 

3.Kupungua uzito, au kutokuongezeka uzito.

Dalili nyingine ya kifua kikuu ni kupungua uzito kwa mtoto , tunajua wazi kubwa mtoto anapaswa kuongezeka uzito kila mwezi kama afya yake ni nzuri na hana ugonjwa ukiona uzito wa mtoto umeanza kupungua na hata kila mwezi haongezeki uzito hiyo ni Dalili ya kifua kikuu kwa mtoto kwa hiyo uchunguzi ni lazima.

 

4.Kikohozi kwa mda mrefu bila kupona.

Kuna kipindi ambapo watoto wanapata kikohozi lakini kikidumu kwa mda mrefu bila kupona na pakiwepo na dalili nyingine za kifua kikuu lazima mtoto apelekwe hospitali ili aweze kupimwa na kupata matibabu zaidi.

 

5.Homa kwa wiki mbili na zaidi.

Kuwepo kwa homa kwa wiki mbili na zaidi ni mojawapo ya Dalili ya kifua kikuu kwa mtoto kwa hiyo mama au mlezi baada ya kuona dalili kama hizi ya kuwepo kwa homa ambazo hazishi kwa mtoto ni lazima kumpeleka kwa mtoto kwa uangalizi zaidi.

 

6.Mtoto kudumaa au kutoonyesha maendeleo yoyote katika ukuaji na kubaki katika hali hiyo ikiongezea na kukonda 

Hii ni Dalili kubwa ya kifua kikuu ambapo mtoto uonekana kama mwenye mambukizi ya virus vya ukimwi na kukua hakui kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa ni Dalili mojawapo ya kifua kikuu kwa mtoto kwa hiyo matibabu ni lazima.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 3188

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

MALARIA NI NINI? NI WATU WANGAPI WANAKUFA KWA MALARIA DUNIANI

Malaria ni katika maradhi yanayosumbua sana na kusababisha maradhi ya watu wengi sana duniani.

Soma Zaidi...
Aina za saratani ( cancer)

Posti hii inahusu zaidi Aina za kansa, Kansa ni Aina ya ugonjwa unaosababishwa na kuzaliana kwa seli ambazo sio za kawaida.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa pepopunda kwa watoto

Pepopunda ni ugonjwa hatari wa kutishia maisha unaosababishwa na sumu inayojulikana Kama tetanospasmin inayotolewa kwenye majeraha yaliyoambukizwa. Bakteria ya pepopunda huingia kwenye mwili wa mtoto mchanga kupitia kisiki cha kitovu ambacho kimekatwa na

Soma Zaidi...
tatizo la kushindwa kujaza misuli ya mwilini na kusinyaa kwa misuli mwilini

Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa kusinyaa kwa Misuli. Ni maradhi yanayopelekea uzalishwaji hafifu wa misuli, hivyo kupelekea misuli kukosa protini, kushunwa kukuwa na kusinyaa.

Soma Zaidi...
Koo langu limekauka yaweza kuwa ni muadhirika?

kuwashwa na koo ni katika dalili za kuwa na maambukizi mwilini. Kuwa na maambukizi haimaanishi ni HIV ama UKIMWI laa hili ni neno pana. Hapa nitakujuza kwa ufupi kuhusu swali hilo la muulizaji kuwa anawashwa na koo.

Soma Zaidi...
Sababu za mdomo kuwa mchungu

Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu.

Soma Zaidi...
Fahamu Dalili zinazotokana na kuzama kwenye majj kwa watoto.

Kuzama hufafanuliwa kama mchakato unaosababisha upungufu mkubwa wa kupumua kutokana na kuzamishwa kwenye chombo cha kuogelea (kioevu). Kuzama hurejelea tukio ambalo njia ya hewa ya mtoto huzamishwa kwenye kioevu, na kusababisha kuharibika kwa kupumua.

Soma Zaidi...
Nini husababisha ugonjwa wa kifua na maumivu ya kifua?

Posti hii inazungumzia sababu zinazopelekea kuumwa na kifua.

Soma Zaidi...
Nini kinasababisha kizunguzungu?

Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za kizunguzungu zinazotekea katika mwili wa binadamu

Soma Zaidi...
FIKRA POTOFY KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO

FIKRA POTOFY KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Vidonda vya tumbo huja na maoni mengi potofu.

Soma Zaidi...