Posti hii inahusu zaidi maelekezo muhimu kwa mama au mlezi wa mtoto mgonjwa. Ni maelekezo muhimu hasa wakati wa kutoa dawa kwa mtoto.
Maelekezo muhimu kwa Mama au mlezi wa mtoto mgonjwa.
1.Kwanza kabisa watoto wadogo wanapaswa kuwa karibu sana na walezi wao ili waweze kupata huduma muhimu na za msingi kwa hiyo mtoto akiwa mgonjwa na akaleta hospitalini Mama au mlezi wanapaswa kupewa maelekezo yafuatayo ili kuweza kuwafanya wampatie Mtoto dawa sahihi na kwa wakati wake.
2. Kwanza mama au mlezi wanapaswa kujua dozi na dawa ipi mtoto anapaswa kupewa, na pia wanapaswa kuambiwa wazi sababu ya kupewa dawa hizo, kwa hiyo akina mama wakiwa wanaenda hospitalini ni muhimu kuuliza sababu ya kupewa dawa, mtoto anapaswa kupata dozi ipi na kwa mda gani kwa hiyo ni haki kuuliza na kupewa jibu.
3. Pia Mama anapaswa kuonyeshwa kwa vitendo namna ya kumpatia mtoto dawa na pia ikiwezekana anaweza nkujarubisha akiwa anaangaliwa na kama mtoto hajapewa dawa dozi ya kwanza inaweza kutolewa ili kumfanya Mama aweze kupata uzoefu wakati wa kutoa dawa.
4. Na kama dawa ni zaidi ya moja ni lazima kuziweka alama ili zisije kuchanganywa na pia mama anapaswa kujua kuwa lazima dawa zitolewe kwa mtoto mpaka ziishe hata kama mtoto amepona kwa hiyo ni lazima kumalizia dawa zote ili kuepuka hali ambayo siyo nzuri ikitokea dawa haijaisha.
5.Kwa hiyo ni vizuri kwa akina mama na walezi wa watoto kubwa makini pindi mnapokuwa hospitalini hakikisha kuwa dawa unazopewa unajua wazi matumizi yake na unaweza kujisimamia mwenyewe na kumpatia mtoto kwa mda mwafaka na akapona kwa hiyo kama hauwezi au haujui matumizi uliza kwa sababu unayo haki ya kupata matibabu kwa wakati na kwa mda wake
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Nina swali langu:-je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba?
Soma Zaidi...Kutoka na majimaji ka uchache kwa mwanamke sio jambo lakishangaa sana. Damu hii inawezapiabkikbatana damu na maumivu makali.
Soma Zaidi...Yai lililopikwa ni chanzo kizuri cha protini, vitamini, na madini muhimu kwa mama mjamzito. Husaidia katika ukuaji wa mtoto tumboni, afya ya mama, na kuimarisha kinga ya mwili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kutokwa na majimaji kwenye uume, ni tatizo ambalo uwakumba baadhi ya wanaume kwa sababu mbalimbali na pia Ugonjwa huu unatibika hasa kwa wale wanaowahi kupata matibabu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu changamoto za ujauzito na dalili zake endelevu
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na mathara yanayosababisha Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukupa dalili ambazo zinaonyesha kuwa mimba ni ya mapacha. Dalili hizi zitahitajika kuthibitishwa na kipimo cha daktari ili kujuwa kuwa ni kweli.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za mimba kutoka, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mimba zote ambazo utaka kutoka kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...