Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo mgonjwa wa ngiri anaweza kuzipata, kwa hiyo baada ya kusoma na kuelewa dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospitali mapema kwa ajili ya kupata matibabu.
1​​​​​​. Kwanza kabisa tunajua kuwa ugonjwa wa ngiri utokea pale ambapo misuli au kuta za tishu mwilini ambazo ushikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kubwa na uwazi na kufanya viungo hivyo kutoshikilia vizuri katika sehemu inayostahili hali ambayo Usababisha mtu kuhisi maumivu na pengine kuwepo kwa uwazi katika sehemu mbalimbali za mwili hali ambayo Usababisha nyama kuota na kuelekea kwenye sehemu hizo za uwazi.
2.Kuna Dalili mbalimbali ambazo ujitokeza iwapo mtu amepata tatizo hili na dalili hizi utofautiana kutoka kwa mtu mmoja na mwingine kwa sababu ugonjwa huu ushika sehemu tofauti kama vile kwenye kifua, kwenye kitovu na kwenye mshipa wa ngiri na pengine kwa sababu ya upasuaji kwa hiyo Dalili utofautiana kulingana na Ugonjwa umeshika sehemu ipi.
3. Mtu mwenye tatizo la ngiri anaweza kubanwa na tumbo hasa chini ya kitovu wakati wa baridi na pengine pale anapokuwa ameshiba au amekula vitu vitamu, hiyo huwa ni dalili ya ngiri ya kitovu kwa walio wengi.
4. Kupinga mingurumo tumboni.
Kwa kawaida ngiri nyingi ili kutokea uanzia kwenye tumbo ambapo sehemu ya utumbo inaota kuelekea kwenye uwazi fulani inawezekana kwenye kifua au na sehemu mbalimbali za mwili ambapo ngiri inaweza kutokea kwa hiyo hali hii usababisha mingurumo kutokea kwenye tumbo.
5. Kuhisi una haja kubwa na ukifika chooni unatoa gesi tu, kwa hiyo kama kuna tatizo hili la ngiri tumbo ukaa na gesi sana ,hii ni kwa sababu ya hali ya tumbo kutokuwa kwenye hali yake ya kawaida.
6. Kukaa siku kadhaa bila kupata haja kubwa , inawezekana kwa siku kama mbili au zaidi bila kuwepo kwa choo, au ukibatiwa kupata choo ni kidogo sana na huwa kama choo ya mbuzi.
7. Pengine Mgonjwa anakwenda haja mara kwa mara, hasa anakuwa anahisi haja kubwa na akienda uko ni gesi na choo kidogo hali hiyo usumbua sana na kufikia kiasi cha mgonjwa kukaa karibu na choo na hatoi kitu cha maana.
8. Kupotea kwa nuru ya macho.
Mara nyingine kuna wagonjwa ambao nuru za macho upotea, ila hali hii utokea kwa mara chache sana na sio kupotea kwa nuru ni tatizo la ngiri kwa hiyo mgonjwa anapaswa kupima kwanza ili kujua tatizo ni nini.
9. Maumivu makubwa ya mgongo na kiuno.
Kuna wagonjwa wengine wanahisi kuwa na maumivu makali ya mgongo na kiuno na pengine hali inaweza kufikia kiasi kwamba Mgonjwa anashindwa kutembea, kwa hiyo ni vizuri kupima haraka na kugundua tatizo ni lipi.
10. Makende kuwa kwenye sehemu moja.
Kuna wakati mwingine makende yote yanakuwa kwenye sehemu moja kwa hiyo ni vizuri kujua Dalili hii ili kuweza kutibu na pengine mgonjwa anahisi maumivu makali sana kwenye sehemu za siri hasa kwa wanaume.
11.Pamoja na kujua Dalili zote za ngiri ni vizuri kabisa kujua kuwa sio Dalili zote ni za kuwepo kwa ngiri kwa hiyo vipimo ni lazima na kuwaona wataalamu wa afya ni jambo la muhimu sana ili kuweza kugundua kuwae ni tatizo gani kwa sababu kuna Magonjwa mbalimbali ambayo yana Dalili kama hizi.
12.Pia tunapaswa kutoa wito kwa jamii kuwa ugonjwa wa ngiri upo na unatibika kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa kwa jamii ili kuepuka hali ya kuwaficha wagonjwa wakiwa na umani kuwa ni magonjwa ya zinaa na kuona kuwa ni aibu kwa familia na kuwatibu wagonjwa ki mila hali inayosababisha kuongezeka kwa maumivu na tatizo kubwa kubwa zaidi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Zijuwe sababu kuu zinazokufanya ukahisi maumivu makali ya tumbo kwa chini upande wa kushoto
Soma Zaidi...Saratani ya uke ni Saratani adimu inayotokea kwenye uke wako mrija wa misuli unaounganisha uterasi na sehemu zako za siri. Saratani ya uke mara nyingi hutokea katika seli zilizo kwenye uso wa uke wako, ambao wakati mwingine huitwa njia ya uzazi. Wan
Soma Zaidi...Maumivu ya matiti yanaweza kuanzia kidogo hadi makali. Inaweza kukuathiri siku chache tu kwa mwezi, kwa mfano kabla tu ya kipindi chako, au inaweza kudumu kwa siku saba au zaidi kila mwezi. Maumivu ya matiti yanaweza kukuathiri kabla tu ya kipindi chako
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za kuonyesha kuwa Kuna maambukizi kwenye kitovu hasa hasa chini ya kitovu.
Soma Zaidi...Makala hii itaeleza dalili za ukimwi, dalili za VVU, magonjwa nyemelezi na matumizi ya ARV
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, hizi ni njia ambazo zinapaswa kufuatwa ili kutokomeza kabisa maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mlo kwa wagonjwa wa figo wanaochujwa damu, ni wagonjwa ambao figo zao zimeharibika na zimeshindwa kufanya kazi au pengine kuna uchafu mwingi mwilini ambao uchujwa kwa hiyo kuna vyakula muhimu ambavyo wagonjwa wa figo wanapaswa kutu
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza baadhi ya njia za kuzuia kiungulia
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Aina za kansa, Kansa ni Aina ya ugonjwa unaosababishwa na kuzaliana kwa seli ambazo sio za kawaida.
Soma Zaidi...Virusi vya Ebola ni virusi vinavyohusiana vinavyosababisha Homa za hemorrhagic magonjwa yanayoambatana na kutokwa na damu nyingi (kuvuja damu), viungo kushindwa kufanya kazi na, mara nyingi, kifo. Virusi vya Ebola na virusi huishi kwa wanyama, na wanad
Soma Zaidi...