HAdithi hii itakufundisha namna ambavyo mwanadamu anapitia hatuwa mbalumbali tumboni mwa mama yake
Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa:
“Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake).
Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema.
Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye ‘amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa motoni akaingia motoni.
Na mmoja wenu hufanya ‘amalii za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah))
[Al-Bukhaariy na Muslim]
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika hadithi hii utakwenda kujifunza nguzo za uislamu
Soma Zaidi...DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 1.
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صل?...
Soma Zaidi...DUA Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua.
Soma Zaidi...