Posti hii inahusu zaidi mzio na Dalili zake ni Dalili ambazo ujitokeza kwa mtu mwenye mzio, kuna wakati watu wengine ushindwa kutambua kuwa ni mzio au la, lakini leo tunaenda kujua Dalili za mzio kama ifuatavyo.
Mzio (aleji) na Dalili zake.
Mzio usababishwa na vitu mbalimbali kama vile vumbi, kuumwa na wadudu, baadhi ya vyakula, kemikali au madawa fulani, mzio utokea kwa mtu mmoja na mwingine na kila mtu ana mzio wake kwa mfano mtu mmoja anaweza kuwa na Mzio wa vumbi mwingine hana kwa hiyo utofautiana kutoka kwa mtu mmoja na mwingine, na dawa za kutuliza mzio zipo ambazo ni citrizen, pilitin na anti histamine na Mzio ukizidi mwone daktari kwa msaada zaidi.
1. Dalili mojawapo ambayo ilinyesha kubwa ni mzio ni wekundu usoni, mwasho, au upele hayo yanaweza kutokea kwa mtu kwa sababu pengine ametumia dawa fulani ambayo haipatani na mwili wake au chakula fulani kama vile nyama,au amesikia harufu fulani ya maua hali hii umfanya kubwa na vitu vilivyotakiwa hapo juu.
2. Dalili nyingine ni kama vile kuvimba midomo hasa hasa hali hii utokea kwa sababu ya vyakula na kuvimba kinywa na koo, kumeza kwa shida ukiona mgonjwa wako ana dalili kama hizi moja kwa moja anapaswa kupata matibabu yanayofaa ili kuepuka kusababisha madhara makubwa zaidi.
3. Kupumua kwa shida
Aina hii ya mzio uwakumba sana watu mzio wa vumbi, harufu ya maua na vitu vingine ambavyo vinahusiana na kunusa, iwapo mtu amepatwa na Mzio huu uwa na Dalili kama za Asthma kwa hiyo ni vizuri kumpeleka hospitalini ili kuweza kuepuka madhara zaidi, hasa kama ni kwa mtoto hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa hiyo matibabu yanapaswa kutolewa mapema iwezekanavyo.
4. Kuvimba mikono na miguu.
Hii ni Dalili mojawapo ya mzio ambao utokea kwa mtu inawezekana ikawa ni kwa sababu ya dawa au kwa sababu ya vitu vingine kama vile vumbi kwa hiyo kama mgonjwa yuko hospitalini anaumwa dalili hii ukajitokeza anapaswa kufuata ushauri wa daktari au abadilishe dawa au mazingira.
5. Kichefuchefu au maumivu ya tumbo.
Mgonjwa pengine anahisi kichefuchefu kwa sababu pengine mzio unakuwa imeingilia mmeng'enyo wa chakula, kwa hiyo pengine tumbo linaweza kuuma kichefuchefu na hata kutapika kwa mgonjwa kwa hiyo tunapaswa kujua Dalili hizi na kuzifanyia kazi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi ya tishu ya matiti ambayo husababisha maumivu ya matiti, uvimbe, joto na uwekundu. Pia unaweza kuwa na Homa na baridi. Ugonjwa huu huwapata zaidi wanawake wanaonyonyesha ingawa wakati mwingine hali hi
Soma Zaidi...Nimonia ni Hali ya kuvimba pafu inayoathiri hasa vifuko vya hewa viitwavyo Alveoli, husababishwa na Maambukizi ya virusi
Soma Zaidi...UKIMWI (acquired immunodeficiency syndrome) ni hali ya kudumu, inayoweza kutishia maisha inayosababishwa na virusi vya ukimwi (VVU) Kwa kuharibu mfumo wako wa kinga, VVU huingilia uwezo wa mwili wako wa kupambana na viumbe vinavyosababisha magonjwa. Inawe
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa kusinyaa kwa Misuli. Ni maradhi yanayopelekea uzalishwaji hafifu wa misuli, hivyo kupelekea misuli kukosa protini, kushunwa kukuwa na kusinyaa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa Kuna maambukizi kwenye magoti, kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha maumivu au maambukizi kwenye magoti Kuna dalili za mwanzo ambazo zinajitokeza kama tutakavyoona hapo chini
Soma Zaidi...Makala hii itazungumzia dalili za Malaria, athari za kuchelewa kutibu malaria, na matibabu ya malaria
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za fangasi uken, hizi ni baadhi ya dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la fangasi uken.
Soma Zaidi...