Simulizi za Hadithi EP 6 Part 1: Muuaji ni nani?

Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA....

NANI MUUWAJI?

 

Mfalme alipoamka alitaka kumuona kijana wake lakini asimuone. Akauliza habari za kijana yule na akaelezwa kuwa amefariki lakini muuwaji hajulikani, mpaka sasa kuna wauwaji wanne na kila mmoja anadai yeye ndio muuwaji halisi. Mfalme akaamrisha wote waitwe na waje mbele yake na amtafute muuwaji halisi wa kijana wake yeye mwenyewe.

 

Mfalme aliogopa sana asije fanya kosa kama lile alolifanya kwenye kesi ya kifo cha mtoto kwenye ndoo ya maji ambapo mtu asiye na hatia aliuliwa. Walinzi wa mfalme wakamuuliza kwani ni kitu gani kilitokea kuhusu kesi ya mtoto huyu. Akawasimulia kwa ufupi habari hii kuwa alikiwepo mama mmoja aliyekuwa na mtoto anayeanza kusimama dede. Pale ndani palikuwepo na mfanya kazi wao. Mtoto yule alizoeshwa kuogeshwa kwenye ndoo ya maji na mama yake a alikuwa akifurahia sana anapotiwa kwenye ndoo ya maji.

 

Siku moja mama yule alipata safari ya ghafla na kumuacha mtoto wake kwa jirani maana mfanyakazi hakuwepo alikwenda kuchota maji mbali kidogo. Mtoto yule akiwa kwa jirani alitoroka na kyurudi kwao. Na kwa kuwa milango ilikuwa wazi aliingia ndani na kukuta ndoo za maji zipo wazi. Mtoto yule akaingia kwenye ndoo zile na kupitiwa na usingizi. Dada mchota maji alipokuja hakuangalia vizuri kwenye ndoo akajaza maji na kuondoka kwa haraka ili akawahi foleni ya maji.

 

Mtoto mule kwenye ndoo alipiga kelele na kayanywa maji zaidi na hatimaye akapoteza maisha. Akaja dada wa kazi na kujaza ndoo ile kisha akaifung bila ya kuangalia nddani. Akazipandanisha ndoo kama tatu. Mama aliporudi alimtafuta mtoto kwa jirani bila ya mafanikio. Juhudi za kumtafuta ziliendelea ndani ya siku tatu bila hata kufanikiwa. Majirani wakamuonea huruma mwenzao na wakaamua kumpikia apate kula, wengine wakaanza kufua nguo zake na kudeki nyumba maana ndani ya siku tatu hakukuwa kukipikwa wala kufagiliwa wala kudekiwa.

 

Maji yalipobakia ndoo moja wakamkuta mtoto amshakufa kwenye maji. Mama yule kwa hasira alimpeleka mfanyakazi wa hakimu na hatimaye mfanyakazi akauliwa kwa kosa la kumuuwa mtoto kwenye maji na kumficha na ndoo. Kumbe mfanya kazi hana hatia maana ni mama aliyemzoesha mwanae kuingia kwenye ndoo na nikosa la jirani kutomuangalia vizuri mtoto. Kosa la mfanyakazi kuweka maji bila ya uangalifu. Hivyo nahofia kesi hii isijekuwa na mfanano na hii. Basi kwa haraka akaagiza waletwe wat wote wanaohusika mbele yake.

 

Watu wote wakapelekwa kwa mfalme pamoja na maiti wao. Falme akaanza kuuliza mmoja mmoja ataje amemuuwa vipi. Hapo mlevi akasema namna ambavyo tukio limetokea, kisha muuza nyama akaeleza tukio lilivyotokea kwa upande wake kisha tabibu kisha mshona nguo. Baada ya kiusikia maelezo ya kushangaza mfalme akaamuru habari hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na iwekwe kwenye kumbukumbu za kifalme. Kisaha mfalme akauliza je kuna mwenye hadithi inayoshangaza zaidi ya hii ya kijana wangu huyu? Hapo mlevi akasema yeye ana hadithi ya kushangaza zaidi ya hii. Na akaanza kusimulia kama ifuatavyo;-

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Mankaa image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Burudani File: Download PDF Views 484

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 5: Nani ni binti?

Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 6: Hadithi ya Ndoa ya siri

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili muendelezo....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 3: Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi.

Simulizi za HALIF LELA U LELA ni nziri sana tuwe pamoja kusikiliza kisa cha mzee wa pili na mbwa wawili weusi...

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 20: Waliodhulumiwa kufanyiwa suluhisho

Ni mojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 18: Binti wa pili mwimba mashahiri mwenye makovu

Mwendelezo wa hadithi kutoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA......

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 1: Kisa cha mvuvi na jini

Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA ....

Soma Zaidi...