Simulizi za Hadithi EP 6 Part 17: Siri ya wageni yafichuka

Muendelezo........

SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA

Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana. Tulikuwa ni marafiki sana tukiwa katika umri wa miaka 7 mapka 18. baba yako alikuwa ni mchamungu toka alipokuwa mdogo. Alipata malezi mema sana. Na mimi nilivutiwa nikawa nirafiki yangu sana. Tulikuwa tukifanya ibada pamoja na karibia mambo yetu yote. Wakati nilipohama Misri kuja Yemeni niliweka ahadi na baba yako kuwa nikipata mtoto wa kike ataolewa na mtoto wake na akiwa wa kiume atauoa wako, na tulimuomba Mungu atutofaitishie watoto wetu, yaani akiwa wangu wakike wake wa kiume ama wake wa kike wangu awe wa kiume.

 

 

 

Miaka mingi ilipita hata tukasahau ahadi zetu. Mimi nilichelewa kupata mtoto na hata yeye. Hata hivi miaka yapata 17 iliyopita nikajiwa na wageni wa ajabu, kisha akataja kisha kama kile kilichomtokea baba. Kisha akaenelea kusema. Wageni wale walikuwa si watu wa kawaida. Ni wajumbe waliotumwa kuja kutukumbusha ahadi zetu na kutupatia habari njema za kaupa watoto. Siku ya mwisho walipoondoka wageni wale walinieleza kuwa mtoto wako atao;ewa na mtoto wa rafiki yako kaam ahadi. Atakuja mwenyewe, na utamjuaje wakaniachia pete hii iliyokufikia. Walinieleza kuwa pete hii ikifika mikononi mwako katu haitaondoka.

 

 

 

Wakanieleza kuwa sifa zako utakuwa ni muuza viatu. Hivyo binti yangu anayemsaidia kazi mke wangu nilimuagiza aje kwako kuuliza viatu kama walivyonieleza wageni wale sifa za viatu. Nikamueleza kama utamuona mtu aliyebadilika utambue huyo ni mtu ninaye mtafuta. Mwambie aje kwangu. Sasa nilikuwa na ugomvi na matajiri wenzangu waliotaka kumuoa binti yangu, niliwakatalia sana, na ndipo wakapanga njama ya mumuua.

 

 

 

Bila ya kutambua wakamuua yule mfanyakazi wangu wakidhani ndiye binti yangu. Baada ya tukio lile kutokea na pete kupotea bikajua kuwa pete imesafika kwa mwenyewe, maana wageni wale walinieleza katu ete isingeweza kuibiwa, ila itamfikia mwenyewe. Baada ya kumaliza kuzungumza akaniambia kuwa nisiendelee tena kuwatafuta wageni wale katu sitawaona. Akamuita binti wake nije nimuone.

 

 

 

Akaja binti mmoja akafunua sura yake. Nilihisi kama nimepigwa shoti kwenye mwili wangu. Ghafla joto likapanda, nilistaajabu kabisha kuona kuwa kumbe duniani kuana mabinti warembo kiasi kile. Nilijisemea kuwa wale waliotaka kumuoa hawakukosea katu. Kwa kweli binti alikuwa ni mzuri sana. Kisha mzee akasema “mwanangu nitakuozesha binti yangu bure ila kwa sharti kuwa uwe ni kama mwanangu”

 

 

 

Nilikubali na ndipo nikaozeshwa. Nilimuoa mke wangu nikiwa sina mkono mmoja. Bada ya harusi niliishi na mke wangu kwa muda wa miaka 5. kumbe kulikuwa na watu wananifanyia uaduni. Na ndipo wakanifanyia uchawi nikapata jini hili lililokuwa likinisumbua. Tulipata sifa zako ndipo tukaja Baghadad kupata matibabu. Ha hii ndio hadithi ya kukatwa mkono wangu.

 

 

 

Baada ya tabibu kusimulia hadithi hii akamuelekea Sulatani na kumuuliza “Je! Sultani hadithi hii haiwezi kuwa nzito kama kifo cha mtoa burudani?” mfalme akajibu angalau ila bado. Kama haitahadithiwa hadithi nyingine iatakayoshinda hii, wote mtapoteza vichwa vyenu. Basi hapo Mshona nguo akaja mbele na kusema “ Mtukufu nitasimulia kisa kilichomtokea huyu marehemu jana,kitakuwa ni cha kushangaza zaidi kuliko hadithi za wenzangu waliotangulia kusimulia. Akaanza kusimulia kama ifuatavyo:-

 

 

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Mankaa image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Burudani File: Download PDF Views 341

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 20: Waliodhulumiwa kufanyiwa suluhisho

Ni mojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 3: Simulizi ya kuingia kwa wageni

Simulizii hii ya kuwasili kwa wageni inapatikana ndani kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... moja kwa moja tusikilize kisa hichi....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 1: Muuaji ni nani?

Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 10: Mapenzi kwenye mtihani

Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 8: Hadithi ya kisiwa cha uokozi

Simulizi hii ipo ndani ya kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...