Muendelezo....
HADITHI YA CAMARALZAMANI PRINCE PEKEE
Inapata mwendo wa safari ya siku 4 kwa farasi kutokea nchi ya Peshia alikuwepo mfalme maarufu sana aliyefahamika kwa jina la Shahzaman. Mfalme huyu alikuwa ni mkarimu sana kwa mawaziriwake na kwa wananchi pia. Huwenda ukarimu ulizidi kwa sababu hakuwa na mtoto hata mmoja. Mfalme alikuwa na kila kitu lakini katika wake zake wanne wato hakuna hata aliyesubutu kupata walau mtoto mmoja. Mfalme aliendelea kutekeleza majukumu yake, laki I kuna muda huwa anakaa na kuwaza kuhusu mtoto ambaye angekuja kurithi madaraka yake. Fikra zake zote huwa hazina majibu sahihi. Wakati mwingine hudhani lamda wake zake ni matasa. Wakati mwingine hugombana na wake zake juu ya kupata mtoto.
Siku moja mfalme alimuita waziriwake mkuu na kumtaka shauri kuhusu swala la kupata mtoto. Waziri hakuwa namaneno mengin sana maana alitambuwa kuwa mfalme wake hakuwa mtu wa kuzunguka anapotaka jambo. Mfalme alipendelea sana mtu kuzungumza naye kwa uwazi na moja kwa moja bila ya kufichaficha maneno. Basi waziri akamshauri mfalme kwa kubwambia “mfalme, swala la kupata mtoto lipo nje ya uwezo wa binadamu ni Mungu pekee ndiye anaweza hivyo, nakushauri uwaite viongozi wa dini, uandae zawadi na sadaka, ili wakufanyie duwa, huwenda Mungu akakuhurumia”. mfalme aliupenda sana ushauri huo na akafanya kama alivyoelezwa. Zawadi mbalimbali aliandaa na sadaka pia.
Ijumaa iliyofuwata kundi kubwa la viongozi wa dini likawasiri. Duwa kubwa ikafanywa na zawadi zikatolewa. Sadaka mbalimbali zilitolewa ikiwemo chakula, dhahabu, vifaa vya nymbani na pesa. Hakika watu walifurahi sana. Huwenda hata Mwenyezi Mungu alifurahi pia, hivyo haukupita mwezi mke mkubwa wa mfalme akapata ujauzito. Furaha ilitawala kwa wananchi, viongozi walioomba duwa na viongozi wa nchi. Furaha zaidi ni kwa mfalme. Hatimaye miezi 9 ikatimia. Ndani ya kasri la Mfalme Shahzaman mtoto wa kiume akazaliwa.
Kwa kuwa malezi ya ujauzito yalikuwa vyema, basi mtoto alikuwa na afya nzuri na mwenye sura nzuri ya utotoni. Jina alilopewa lilikuwa ni Kamaralzamani yaani mwezi wa nchi. Viongozi walioomba duwa wakampa jina la uani kama badrudin. Mtoto huyu alilelewa katika maisha ya furaha sanna kwa kuwa alikuwa ni wa pekee na ni wa kiume pia. Kila alipokuwa maisha yake yote yalikuwa yakifuatiliwa kila hatuwa. Walimu wake walikuwa ni bora zaidi kuliko walimu wa watoto wa mawaziri.usiku asingeweza kung’atwa hata na upepe kama ungeliuwa unag’ata. Alikuwa akilindwa muda wote.
Kamaral zamani au Badrudin kama walivyomuita wengine, licha ya kuwa anapendwa na watu kwa upekee wake na kuwa ni mtoto wa mfalme, lakini pia alikuwa na sura nzuri sana. Mabinti watoto wa mawaziri walikuwa wakimfananisha uzuri wake kama mwezi yaani aling’aa sana. Haikuwa kawaida kwa mtoto wa kiume kuwa mzuri kiasi kile lakini ilitokea hivyo kwa kamaralzamani. Maisha yalikwenda vyema hata kamaralzamani alipoingia umri wa kubalehe. Mabinti hawakuweza kupata kile walichotarajia kutoka kwa kamaralzamani, ijapokuwa walijiweka karibu sana naye.
Siku moja mfalme akamuita waziri wake na kumwambia kuna “ninataka kujivuwa madaraka ya ufalme na kumpatia kamaralzamani, je unaonaje jambo hili”. waziri alikaa kimya kwa muda huku akifikiri jibu sahihi. Kisha akasema “ni wazo zuri ewe mfalme, ila mimi sikubaliani nalo kwa saababu kuu tatu, kwanza wewe bado una nguvu na uwezo wa kuliongoza taifa bado unao na ni mkubwa. Pili Kamaralzamani bado ni mdogo,hajajuwa siasa wala hajawahi kuongoza. Tatu unaonaje kwanza Kamaralzamani angeoa hii ingemletea heshima kubwa hata kabla ya kuwa mfalme.”. hoja hizi alizikubali mfalme, hivyo akatamani aanze na kumuozesha mwanaye kwanza. Pia Kamaralzamani aanze kuhudhuria vikao vya kiuongozi pamoja na mawaziri, ashiriki kwenye majukumu na kutowa maamuzi.
Basi siku ilifata mfalme akamuita mtoto wake Kamaralzaman na kumwambia “mwanangu tambuwa kuwa wewe ndio mtoto wangu wa pekee, nakupendasana kijana changu. Ninataka kuwanzia kesho uhudhurie vikao vya mabaraza yote ya mawaziri, na ushiriki katika kutoa maamuzi.” kijana alionekana kupenda sana wazo hili, kanakwamba alikuwa anaisubiria siku kama hii toka zamani. Ukweli ni kuwa kijana alikuwa ana akili sana na mwenye busara. “nimekubali baba, na nitatii kwa umakini na katu sintokuangusha katika hili” yalikuwa ni maneno ya Kamaral zamani.swa hilo ni moja ila pia kuna jingine. Ni lipi hilo babi. Mfalme alikaa kimya kwa muda.
Baada ya kupiga kutwi ya maji mfalme akatamka “mwanangu, natambuwa sasa umeshaingia utu uzima, ninataka nikupatie mke, je unalionaje jambo hili”? kamaral zamani alinyamaza kwa muda kana kwamba ana mzingo mzito wa mawazo. “baba wazo lako nimelisikia ila kwa sasa sijatamani kutekeleza hilo jambo. Huwenda baada ya muda nitakuwa na wazo hili, ila kwa sasa naomba unipe muda nifikirie.” yalikuwa ni majibu ambayo mfalme hakupendezewa nayo.
Basi mfalme akakutana tena na waziri wake na kumueleza yaliyotokea. Waziri akaendelea kumsisitiza mfalme awe na subira. Kwani alishakuwa na subira sana toka hana mtoto mpaka akapata. Waziri alimsisitiza ampe mwaka mzima ili aendelee kuwa na subira. Lengo la waziri ni kuwa mpaka mwaka kufika binti yake atakuwa tayari kuolewa na ataweza kutengeneza mazingira ya kuwakutanisha wawili hawa. Mfalme hakuelewa mawazo ya waziri. Mfalme alikubaliana na ushauri ule.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa
Tarehe 2024-09-10 15:06:18 Topic: Simulizi za Hadithi
Main: Masomo
File: Download PDF
Share On
Facebook
or
Whatsapp
Views 206
Sponsored links
👉1
Simulizi za Hadithi Audio
👉2
Kitau cha Fiqh
👉3
kitabu cha Simulizi
👉4
Kitabu cha Afya
👉5
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6
Madrasa kiganjani
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 2: Aladini kwenye pango la utajiri
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 10: Ndoa ya binti mfalme na Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 16: Usaliti
Hadithi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi sana na zinavutia na zinasomwa na kusikilizwa kwa wakubwa na wadogo na hii simulizi inatoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 1: Kisa cha mvuvi na jini
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA .... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 3: Mlevi asimuliwa hadithi
Muendelezo wa simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 27: Kaka wa sita wa kinyozi
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini akiwa hatiani
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 15: Mji uliogeuzwa mawe
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 6: Hadithi ya Ndoa ya siri
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 11: Ndani mwa junba la Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...