Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Mtumwa wa mfalme na mawaziri

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Mtumwa wa mfalme na mawaziri

Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha tatu.....

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

MTUMWA WA AJABU

 

 

 

Kama wasemavyo waliokula chumvi nyingi kuwa muomba mungu hachoki, basi waziri Faridi aliendelea kuomba Mungu hata siku moja akapata taarifa kuwa kuna watumwa wametokea nchi za Uajemi. Hapo waziri alitabasamu kwani alifahamu sasa anakwenda kupata alilolitaka. Kwani alitambuwa kuwa maeneo hayo ndipo watumwa wenye sifa hizo wanapatikana. Basi alifika akauta kuna mabinti wasiopungua 150. waziri aliwaangalia vyema sana huku akagunduwa kuwa kuna wwengine walikuwa wakitabasamu. Alitambuwa kuwa hawa hawafai maana wanadiriki kuuza tabasamu lao bila ya sababu.

 

 

 

Kwa mara ya kwanza waziri akachaguwa walio wazuri kuliko wote. Aliamii kuwa mfalme angeanza kuangalia uzuri hata kabla ya kumthaminisha mtumwa wake. Katika mchujo huu akapata mabinti 21. kisha akaanza kuangalia sauti zao, nywele zao, nyusi na rangi za macho yao. Katika mchujo juu akabahatika kupata 12. kisha akaangalia vigezo vya elimu ya dini na dunia, hapa kabahatika kupata 5. kisha akaangalia hati za uanishi, na ufasaha wa kuzungumza hapa akabahatika kupata 3. sasa akaangalia kama wanafahamu kuburudisha hadhira na kumbrusisha mwanaume. Hapa ndipo akampata binti mmoja aliyefahamika kwa jina la An-neese.

 

 

 

Hakika binti huyu alikuwa mzuri aliyepitiliza vigzo vya sultani. Maana urefu wake haukuwa wa kuchuchumia, hakuhitaji kupaka mafuta ndipo kulainisha ngozi yake. Siku zote alitumia vyakula asili kuweza kuweka mwili wake katika afya na urembo. Hakuwa ni mkwaro wa sauti, mach meupe makubwa, yaliyopambwa na nyuzi nyeysi sana zilizotengeneza umbo la mwezi mwandamo. Nywele nyefu na ngumu zenye afya. Alitambuwa kusoma hati za lugha kadhaa zilizokuwa zikitumia maeneo yale kama kiarabu, kihindi, kiroam (latini) na baaadhi ya lugha za hispatia na fursi.

 

 

 

Waziri alikabidhi pesa palepale. Hapo muuzaji wa watumwa akampa ushauri waziri kuwa, “kwa ;leo usimpeleke kwa mfalme maana ametoka mbali,hivyo kwa uchovu alio nao, uzuri wake utajificha kidogo. Hivyo nakushauri, nenda naye kwanko kwa kiasi cha wiki na atakapozoea hali ya hewa uzurio wake utazidi mara dufu na hapo itakuwa vyema kumpeleka kwa mfalme. Waziri alikubwali ushauri huu japo kwa shingo upande akihofia mwanaye Nurdini.

 

 

 

Waziri siku hiyo alikuwa akirurahia na kuamini sasa amempata wazri Masoud. Ila alihitaji iwe ni mshangao hivyo hakuthubuti kumwambia yeyote kuwa amempata mtumwa wa mfalme. Basi siku hiyo wazir wakati anakwenda na mtumwa wake kwake kwa ushauri wa muuzaji alimueleza kila kitu kuwa awe mbali sana na Nurdin maana ataweza kumuharibia kwani hajawahi kuacha sketi ya mtumwa wala mfanyakazi aliyeletwa nyumbani.yule binti mtumwa akaahidi kuwa hatakuwa na mahusiano na Nurdini kabisa. Basi alipofika nyumbani akamueleza mke wake kila kitu na kumtaka ampatie mtumwa yule kila anachohitaji ili baada ya wiki kupita ampeleke kwaMfalme.

 

 

 

Binti mtumwa akatengewa eneo lake mwenyewe kwa ajili ya malazi na makazi. Mabinti wengine waliandaliwa kwa ajili ya kumpatia kila alichohitaji kuhakikisha kuwa anazea hali ya hewa na uzuri wake unaboreka. Hata hivyo baadhi ya vibinti vifanyakaz wa waziri walikuwa wakichukizwa na uwepowa mtumwa ambaye alikuwa ni kama malkia. Mtumwa ambaye alikuwa akifanyiwa kazi. Hakika mambo haya yalikuwa yakiwachokesha. Walikuwa wana kazi ya kumpikia, kumsugua anapokwenda kuoga, kumpamba na kumfanyia mambo mengine zaidi.

 

 

 

Mambo yote haya yalikuwa yakitokea bila ya Nurdini kutambuwa uwepo wa binti yule. Mambo haya yalifanywa kwa siri ili aibu kubwa isijempata Waziri. Waziri aliamini kuwa kama atamueleza Nurdini kuwa asijekwenda kumuona yule binti basi huenda Nurdini ndio angekwenda kwa makusudi, kwa ajili ya kuridhisha udadisi wake. Basi mambo yakawa kama hivyo haimaye siku mbili zikaisha na ya tatu ikaingia. Uzri wa binti ulikuwa ukiongezeka kila siku zinapozidi. Mawazo ya kubadili maamuzi ya waziri yalikuwa yakimjia. Na hata me wake wivu ulianza kumkamata ijapokuwa hakuweza kudhihirisha.

 

 

Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Mankaa image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Burudani File: Download PDF Views 283

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 2: Kisa cha kinyozi msiri..
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 2: Kisa cha kinyozi msiri..

Karibuni tuendelee kusimuliana stori za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza, stori nzuri sana na za kuvutia zimeandaliwa kwaajili ya kujifunza na kujiburudisha pia.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 17: Ufupisho wa ALIFU LELA U LELA KITABU CHA KWANZA
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 17: Ufupisho wa ALIFU LELA U LELA KITABU CHA KWANZA

Huu ni ufupisho mfupi kuhusiana na kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA...

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 18: Binti wa pili mwimba mashahiri mwenye makovu
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 18: Binti wa pili mwimba mashahiri mwenye makovu

Mwendelezo wa hadithi kutoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA......

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 20: Waliodhulumiwa kufanyiwa suluhisho
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 20: Waliodhulumiwa kufanyiwa suluhisho

Ni mojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...