AINA ZA MINYOO: tapeworm, livefluke, roundworm, hookworm, flatworm

AINA ZA MINYOO Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa.

AINA ZA MINYOO: tapeworm, livefluke, roundworm, hookworm, flatworm

AINA ZA MINYOO

AINA ZA MINYOO
Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa. Aina hizi ni Minyoo wanaotambulika kama flatworm, roundworm na thory-headed worm. Majina ya minyoo hawa yanafanana na maumbile yako kama tutakavyoona hapo chini. Wengi katika hawa minyoo wanaweza kuonekana kwa macho



1.Minyoo inayotambulika kama Tapeworm
Hawa ni katika aina za flatworm, minyoo hawa wanaumbo lililo bataa yaani flati. Unaweza kuwapata minyoo hawa kwa kunywa maji ambayo yana mayai ya minyoo hawa au lava. Pia unaweza kuwapata. Minyoo hawa kwenye chakula ambacho hakikupikwa ama hakikuiva vizuri.kama nyama hasa ya ngurue. Karibia nyama za wanyama wote zina wadudu hawa.

Minyoo hawa wanaonekana kama pingili zilizoungana na kutengeneza cheni ndefu. Minyoo hawa wanaweza kuwa warefu mpaka kufikia futi 80 na wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu mpaka miaka 30.



2.minyoo inayotambulika kama flukes
Hawa pia ni katika aina za minyoo waitwao flatworm. Mwanadamu anaweza kuwapata minyoo hawa kupitia maji yasiyo salama,kupitia mboga ambazo hukuwa ndani ya maji.pia kwa kula samaki ambaye ana minyoo hawa. Pia inatokea ukaosha mboga, tunda kwa kutumia maji ambayo yana minyoo hawa.

Minyoo hawa wanapoingia mwilini wanaelekea kwanye utumbo mdogo na huko ndipo huishi, pia maeneo mengine wanapoishi ni kwenye damu, na tishu za mwili kama ini. Kuna aina nyingi za aina hii ya minyoo, lakini ukubwa wao hawazidi nchi kadhaa.



3.minyoo wanaotambulika kama Hookworm
Hawa ni minyoo aina ya roundworm. Minyoo hawa wanaweza kusambazwa kwa kupitia kinyesina udongo. Hasa kwa wale wanaokula udongo ni rahisi sana kupata aina hii ya minyoo. Njia nyingine nyepesi kwa kupata minyoo hawa ni kwa kutembea miguu peku kwenye udongo ambao una mayai au lava wa aina hii ya minyoo. Malava haya yanaweza kuingia kwenye ngozi yako.

Minyoo hawa wanaishi kwenye utumbo mwembamba, na kwa kuwa kichwani kwao kuna kama miimba ilofanana na ndiwano, wanaitumia kujitundika kwenye utumbo mdogo. Ukubwa wao hauzidi nusu nchi.



4.minyoo wanaotambulika kama pinworms (threadworms)
Hawa ni katika minyoo wadogo sana na maranyingi hawana madhara. Minyoo hawa ni maarufu sana kwa watoto, walezi wa watoto wadogo na maeneo yeye watoto wadogo wengi unweza kuwapata sana hawa. Wana rangi nyeupe na ukubwa wao hauzindi nusu nchi.



Minyoo hawa unawapata kwa kuyala mayai yao kutoka kwa mtu mwenye minyoo hii. Mayai ya minyoo hawa hayawezi kuonekana kwa macho. Pindi unapokula mayai haya yanakwenda kukaa kwenye utumbo mdogo mpaka kutotolewa. Wakati wa usiku minyoo wanawake wanakwenye chini kwenye puru na kutaga mayai kwenye mikunjo ya puru. Kama mtu atajikuna sehemu ya puru mayai yale yanabakia mkononi zaidi ya masaa kadhaa.



Ikitokea mtu huyu ameshika kitu bila ya kunawa mayai yele yanabaki pale. Kama mtu mwingine akapashika pale na akala kitu bila ya kunawa anaweza akayala mayai yale na kupata minyoo. Pia minyoo hii unaweza kuipata kwa kuvuta hewa yenye mayai ya minyoo hii.



Minyoo hii haina athari zaidi kwa afya lakini mwenye minyoo hii atahisi kuwashwa kwenye puru, ama kuzungukia sehemu ya haja kuwa, wakati mwingine maumivu yatumbo. Wakati mwingine ngozi inawasha sana. Minyoo hawa pia kwa wanawake wanaweza kuhama kutoka kwenye puru na kuelekea kwenye uke wa mwanamke na kuingia ndani. Huenda hali hii ikapelekea kupata UTI na matatizo mengine ya kiaya.



Kupambana na minyoo hawa hakikisha unaosha mikono unapoamka, unapotaka kula chochote, kuingia kwenye choo safi na usipende kushikshika vitu hasa maeneo ya vyoo vya watu wengi. Minyoo hawa ni rahisi kutibika tofauti na minyoo wengine.



5.minyoo wanaotambulika kama trichinosis worm
Minyoo hawa ni katika minyoo ambao wanapatikana kutoka kwa wanyama. Mtu anaweza kuwapata minyoo hawa kwa kula nyama ambayo haukuiva vyema, ama kwa kula nyama mbichi. Malava ya minyoo hawa yanakwenda kwenye utumbo mdogo, na huko huweza kuingia kwenye mirija ya damu na kuenda maeneo mengine ya mwili, kwenye misuli na tishu za mwili.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 2038

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Dua za Mitume na Manabii    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

Dalili za ugonjwa wa Donda koo

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa Donda Koo ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea viitwavyo kwa kitaalamu corynebacterium diphtheria, ugonjwa huu ushambulia Koo na unaweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa, mate na

Soma Zaidi...
Dalili za kuvunjika kwa nyonga

Kuvunjika kwa nyonga ni jeraha kubwa, na matatizo ambayo yanaweza kuhatarisha maisha. Hatari ya kupasuka kwa nyonga huongezeka na umri.

Soma Zaidi...
Walio kwenye hatari ya kupata Maambukizi kwenye mifupa

Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata Maambukizi kwenye mifupa,

Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa vericose veini

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa vericose veini

Soma Zaidi...
Dalili za jeraha la kawaida kwenye ubongo

Posti hii inahusu zaidi dalili la jeraha la kawaida kwenye ubongo, jeraha la kawaida utokea kwa sababu mbalimbali kama vile kupata ajali na kugongwa na kitu chochote kichwani,

Soma Zaidi...
Dalili za fangasi kwenye mapafu

Posti hii inaonyesha dalili za fangasi kwenye mapafu.

Soma Zaidi...
Dalili za mawe kwenye kibofu Cha mkono

Mawe ya kibofu ni mkusanyiko mgumu wa madini kwenye kibofu chako. Mawe kwenye kibofu hukua wakati mkojo kwenye kibofu chako unapokolea, na kusababisha madini katika mkojo wako kung'aa.

Soma Zaidi...
Dalili za Ugonjwa wa mapafu.

posti hii inahusu dalili za ugonjwa wa mapafu.ambapo kitaalamu hujulikana Kama Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu yako. Majimaji mengi kw

Soma Zaidi...