Nitajuwaje kama mjamzito amekaribia kujifunguwa, ni dalili gani anaonyesha, dalili za uchungu wa kujifunguwa

Ni ndoto za wanawake wengi siku moja abebe ujauzito, azae mtoto kisha aitwe mama. Haswa hata wanaume hupendelea hivyo. Ila mwanamke anapofikia kujifunguwa hapa ndipo kizaazaa huonekana. Sasa makala hii itakwenda kukueleza dalili za kujifunguwa.
Daliili za kukaribia kujifunguwa kwa siku kadhaa
1.Maumivu ya nyonga kuongezeka
2.Uchovu kuongezeka
3.Kutoa damu yenye utelezi
4.Viungo kuachia
5.Njia ya kuzalia kutanuka zaidi.
6.Maumivu ya tumbo kuongezeka.
7.Maumivu ya tumbi na kutungwa.
8.Kuharisha
9.Maumivu ya mgongo kuongezeka
Dalili za kujifunguwa kwa masaa machache:
1.Mikazo ya tumbo inayotokea katika muda maalumu
2.Kutokwa na damu yenye utelezi
3.Kutokwa na utelezi kwa wingi
4.Njia kuachia zaidi
5.Mtoto kushuka karibu na njia ya kutokea.
Uchungu wa kujifunguwa:
Uchungu wa kujifunguwa hauwezi kuelezeka kwa maandishi machache haya. Hata hivyo kuna machache naweza kukueleza ijapokuwa huwenda usiwe uhalisia. Kujifunguwa kunapitia hatuwa kuu tatu ambazo ni kama ifuatavyo:-
1.Katika hatuwa ya kwanza
cevix (mlango wa mimba) hulegea na kufumguka kwa sentimita 10. hata hivyo kulegea kwa cevix kunaweza kuanza siku chache nyma, kidogo kidogo. Majimaji yanayotoka ukeni huongezeka baada ya kupasuka kwa utando uliomzunguka mtoto. Katika hatuwa hii mikazo ya tumbo la kujifunguwa yanaweza kuwa makali sana ndani ya sekunde 30 mpaka 60 kisha yanakata kwa dakika kama 4 ama 5 kisha huanza tena kama hivi.
Katika hatuwa hii maumivu yanaweza kuwa makali sana kiasi cha kuwa kama vile hayakati. Hapa mtoto anaanza kusogea kwenye njia ya kuzalia. Wakati huu atakuwa ana sukumana na njia ya haja kubwa na hapa mwanamke anaweza kujisikia kuenda haja kubwa. Baadhi ya wanawake walio mara ya kwanza kupata ujauzito wanaweza kwenda chooni na hatimaye anazalia chooni. Kumbuka mikazo ya tumbo haupoi hata kwa dawa za kukata maumivu.
2.Hatua hii ya pili
Hatuwa hii huanzia toka pale mlango wa kuzalia unapofunguka hadi mwisho (sentimita 10) mpaka mtoto atakapozaliwa. Mikazo ya tumbo katika hatuwa hii inazidi na kuwa katika mpangilio maalumu kwa kuachana. Kila mkazo unapokuwa mkubwa hapa mwanamke atajihisi kusukuma mtoto. Hapa mwanamke atahisi moto kwenye uke wake wakati mtoto anashuka ama atahisi kutanuka kwa uke wake hasa pale kichwa cha mtoto kinapoanza kutoka.
Kipindi hiki mama mamzito atakuwa anapewa maelekezo kuhuku kusukuma mtoto ili kuwezehsa kuzaa kwa haraka. Kuna mengi ambayo daktari ama anayezalisha atatakiwa kuyafanya hapa ili kuwezesha kujifunguwa kwa salama. Mtoto ataanza kutokeza kichwa kisha shingo ikifuatiwa na mabega na baadaye mwili kumalizia. Katika hatuwa hii wahudumu wa afya huwa makini zaidi maana ndio hatuwa yenye hatari sana. Hatuwa hii kwa wanawake ambao ndio ujauzito wao wa kwanza inaweza kuchukuwa lisaa limoja mpaka masaa mawili (1 - 2)
3.Hatuwa ya tatu
Hatuwa hii huanza pale mwanamke atakapojifunguwa. Hatua hii huhu huhusisha kutowa placent, ama kondo la uzazi. Hatuwa hii inaweza kuchukuwa mpaka dakika 30. upotevu wa damu hapa utaendelea kuwepo ijaokuwa si mkubwa. Mikazo ya tumbo la uzazi itasaidia kupunguza upotevu wa damu. Kitukibaya zaidi katika hatuwa hii ni endapo damu itatoka kwa wingi.
Hali hii inaweza kupelekea tatizo lijulikanalo kama postpartum haemorrhage na kupelekea upungufu wa damu na uchovu. Hivyo wakunga na wahudumu wataendelea kuwa makini sana katika hatuwa hii. Katika hatuwa hii ndipo mtoto atatenganishwa na placenter.
NINI UFANYE UKIWA KATIKA UCHUNGU WA KUJIFUNGUA KATIKA
1.Kunywa maji ama juisi kwa wingi ama chai
2.Unaweza pia kula kitu kitamu cha kufyonza kama utaruhusiwa. Hii ni kwa ajili ya kukuongezea nguvu
3.Badilisha mikao kuaa, kulala, ubavuubavu, chalichali, kusimama na kukaa na kadhalika)
4.Kama utaweza kuoga maji ya moto fanya hivyo kabla ya kuingia leba
5.Mwambie msimamizi wako kama ataruhusiwa kuingia akufanyie maseji mgongoni ana akusuguesugue
6.Jitahidi kurilax kati ya mikazo ya tumbo usisukume mtoto mpaka uambiwe kufanya hivyo
7.Unaweza kuomba dawa za maumivu kama utaruhusiwa.
8.Usione aibu hata kidogo ukiwa katika leba. Hao unaowaonea aibu wameshaona kila kitu kwako na kwa watu wengine. Kama unataka kulia lia sana, tambuwa kuwa kila kitakachokutokea hapo ni siri na katu hakuna atakayehadithia, hata hivyo kila kitu ni kawaida sana katika leba.
9.Fuata maelekezo kama utakavyoambiwa na wahudumu wako. Kosa lolote utakalofanya kumbuka linaweza kuhatarisha maisha yako na ya mtoto wako.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
ukiwa na ujauzito unaweza kuona mabadiliko mengi katika mwili wako yakiwemo kutokwa na majimaji. je majimaji haya yana dalili gani kwenye ujauzito?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinafanya wajawazito kupata ugonjwa wa Bawasili, kwa sababu tatizo hili linawapa wakina mama wajawazito, kwa hiyo tutaona kwa nini wajawazito wanapatwa na tatizo hili sana.
Soma Zaidi...SIKU YA KUPATA UJAUZITO Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapo ambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuziba kwa mrija wa kizazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapian tube, ni sababu ambazo ufanya mirija ya follapian tube kuziba.
Soma Zaidi...Kuunda na kujaa kwa matiti ni miongoni mwa dalili za ujauzito lakini pia ni dalili za kukaribia hedhi kwa baadhi ya wanawake. Posti hii itakwenda kufafanuabutofauti wa dalili hizi na kipi ni sahihibkatibya hedhi ama ujauzito.
Soma Zaidi...