picha

utaratibu wa lishe kwa Mjamzito, Vyakula anavyopasa kula mjamzito

Ni vyakula gani anapasa kula mjamzito, na utaratibu mzima wa lishe kwa wajawazito

utaratibu wa lishe kwa Mjamzito, Vyakula anavyopasa kula mjamzito



LISHE SALAMA KWA MJAMZITO:




Kwa ufupi ni kuwa mjamzito na anayenyonyesha wanatakiwa wapewe lishe kamili iliyokuwa na virutubisho vyote. Haata hivyo ni vyema kuzingatia nukuu za hapo chini. Wanaonyonyesha na wajawazito wanahitaji kupata vyakula vyenye viinilishe vya kutosha ili kuwezesha ukuaji wa mtoto tumboni , utengenezwaji wa maziwa na kwa ajili ya afya zao wenyewe.



Vyakula vya protini vinahitajika kwa mkiwango kikubwa ili kuwezesha mwili wa mama kujenga misuli vizuri , tishu katika mwili wake na mwili wa mtoto aliye tumboni. Utengenezwaji wa maziwa , usafirishwaji wa damu na ukuaji wa viungo vya mama na mtoto unahitaji protini. Hivyo wamama hawa wapewe protini kwa wingi.vyakula vya protini ni kama:-
A.Nyama
B.Mayai
C.Maharagwe
D.Samaki
E.Maziwa
F.Pia kwenye nafaka na baadhi ya mboga za majani na matunda.



Vyakila vya folic asid na vitamini B vinahitajika kwa ajili ya kuwezesha kupunguza tatizo la kushindwa kujifunguwa kwa njia ya kawaida. Vyakula vya madini ya kashiam(calcium) ni muhimu kwa ukuwji wa mifupa ya mtoto aliye tumboni na kuimarika mwili wa mama pia. Kwani mjamzito asipopewa madini haya mtoto atatumia madini yaliyomo kwa mama na kumfanya mama awe na mifupa dhaifu katika kipindi hiki.



Madini ya chuma ni muhimu katika utengenezwaji wa damu, halikadhalika mtoto anahitaji madini haya ili ayatumie katika wiki ya kwanza ya kuzaliwa. Madini ya zink ni muhimu katika kuwezesha kujifunguwa.(progression of labour) na ukuaji salama wa mtoto aliyoko tumboni.



Wamama wajawazito wapewe vyakula vyenye kambakamba (dietary fiber}. Hivi vitamuwezesha kutopata tatizo la kukosa choo.



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views 2519

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Je, mwanamke anapataje Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi PID?

Posti hii inaelezea namna mwanamke anavyoweza kupata Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi.

Soma Zaidi...
Mabadiliko kwenye uke wa Mama pale anapobeba mimba.

Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye uke wa Mama pale anapobeba tu mimba, Mama anapobeba mimba Kuna mabadiliko Katika uke wa Mama kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...
Namna za kujilinda na fangasi ukeni

Posti hii inahusu zaidi namna ya kuepuka fangasi za ukeni, ni njia ambazo usaidia kuepuka madhara ya fangasi za ukeni.

Soma Zaidi...
Faida za kula yai lililopikwa kwa mama mjamzito

Yai lililopikwa ni chanzo kizuri cha protini, vitamini, na madini muhimu kwa mama mjamzito. Husaidia katika ukuaji wa mtoto tumboni, afya ya mama, na kuimarisha kinga ya mwili.

Soma Zaidi...
Zifahamu fibroids (uvimbe kwenye via vya uzazi)

Posti hii inahusu zaidi fibroids au uvimbe kwenye via vya uzazi hasa hasa utokea kwenye tumbo la uzazi ambapo kwa kitaalamu huitwa uterusi, uvimbe huu ulitokea watu wengine huwa hawawezi kutambua Dalili zake mapema kwa hiyo leo tunapaswa kujua Dalili zake

Soma Zaidi...