Rangi za matunda
Fida za matunda huanzia kwenye rangi zake, je unajuwa kama rangi ya matunda inaeleza jambo?
RANGI ZA MATUNDA
Unaweza kujiuliza ni kwa nini matunda yana rangi mbalimbali? Hili swali Mwenyezi mungu aliyeumba kila kitu ndiye anajuwa saidi. Ila kwa ufupi utambuwe kuwa rangi katika matunda ni dalili ya ishara flani. Katika post hii tutaona baadhi ya rangi katika matunda. Mwisho wa post hii utaweza kutambua nini kimo katika tunda utakaloliona kwa kuangalia rang.
1.rangi nyekundu
Rangi nyekundu kwenye matunda hutokana na nyembenchembe ziitwazo lycopene. Hizi ni antoxidant ambazo husaidia katika kulinda mwili dhidi ya sumu za vyakula. Sumu hizi mara nyingi huweza kuharibu seli ndani ya miili yetu. Pia sumu hizi husababisha mtu kuzeeka haraka. Chembechembe hizi pia husaidia katika kuzuia uharibifu wa seli mwilini. Huimarisha mfumo mzima wa kinga mwilini. Na pia husaidi akatika kulinda au kupunguza adhari za magonjwa ya moyo na saratani.matunda yenye rangi hii ni pamoja na tomato, matikiti, pilipili n.k
2.rangi ya njano.
Rangi ya njano kwenye matunda husababishwa na chembechembe ziitwazo beta-carotene, hizi pia ni antoxidant. Chembechembe hizi husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini. Mwili huweza kubadili beta-carotene, kuwa vitamini A. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimu sana katika afya ya mtu. Kupamabana mna maradhi mablimbali nna kuimarisha afya ya macho. Kupambana na wadudu wanaosababisha vidonda vya tumbo. Huimarisha afya ya ngizi na maeneo mengune yenye utando laini.miongoni mwa matunda yenye rangi hii ni viazi, karoti, maembe n.k
3.rangi ya kijani.
Rangi ya kijani husaidia kutambuwa uwepe wa vitamini Ana C. Kama inavyotambulika mboga za majani zina rangi hii. Vitamini A na C huweza kupatikana kwa wingi kwenye rangi hii. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimi katika kudhibiti mfumo mzima wa kinga mwilini. Upungufu wowote wa vitamini hivi viwili uanaweza kusababisha madhara makubwa mwilini.
4.rangi ya bluu na violet
Rangi hii hutambulisha uwepo wa anthocyanin ambayo ni antioxidat. Itambulike kuwa antioxidant zina uwezo mkubwa wa kupambana na sumu mbalimbali ndani ya mwili. Sumu hizi zinasababishwa ba vyakula tunavyokula kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivi vyenye rangi hii huwa vina vitamini C kwa kiasi kikubwa. Pia vyakula hivi vina kambakamba ambazo ni muhimu sana katika afya ya mtu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake
Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake
Soma Zaidi...Lishe salama kwa mjamzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu lishe salama kwa mjamzito
Soma Zaidi...Zijue Faida ya kula tunda la tango.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida za kula tango japokuwa watu wengi hulipuuzia Ila Lina Faida kubwa Sana mwilini.
Soma Zaidi...Papai lililo iva ni salama kwa mama mjamzito au halifai
Papai ni moja kati ya matunda yenye vitamini C na virutubisho vinginevyo. Lakini papai pia ni moja kati ya vyakula ambavyo mjamzito anatakiwa awe makini navyo.
Soma Zaidi...Faida za kula Embe
Embe ni katika matunda atamu na yenye faida kubwa kiafya, soma makala hii hadi mwisho
Soma Zaidi...Namna ya kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba.
Posti hii inahusu namna au njia za kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba ya homoni imbalance kwa wanawake.
Soma Zaidi...