Hapa utajifunza vyakula hatari kwa mgonjwa wa kisukari, pia utajifunza vyakula salama anavyotakiwa ale mgonjwa wa kisukari, Pia ujajifunza njia za kujikinga na kisukari
VYAKULA SALAMA NA HATARI KWA MWENYE KISUKARI
Kisuari ni hali ya mwili kushindwa kudhibiti kiwango cha sukari hivyo kuachia sukari yote kuishia kwenye damu bila ya kuingia kwenye seli ili kutumika maeneo mbalimbali ya mwili. Na hutokea endapo uzalishwaji wa homoni ya insulini utakuwa katika shida. Eidha hutokea kwa sababu homoni ya insulini inayozalishwa si yenye kutosheleza ama mwili wenyewe unashindwa kuitumiahomoni ya insulini. Homoni ya insulin ndio ambayo hudhibiti kiwango cha sukari.
Vipi kisukari hutokea?
Mwili unahitaji sukari kwa ajili ya kuzalisha nishati yaani nguvu. Mwili pia unahifadhi sukari kwa matumizi ya baadaye. Endapo sukari mwilini itakuwa ni nyingi basi homoni ya insulini huzaliwa kwa wingi ili kupunguza sukari iliyozidi n akuihifadhi kwa matumizi yaa baadaye. Na endapo sukari itakuwa ni kidogo mwilili homoni ya insulini huzuiliwa hivyo mwili hutumua sukari iliyohifadhiwa. Kwa kufanya hivi kiwango cha sukari hudhibitiwa.
Sasa endapo kutatokea shida yeyote katika matumizi ya homoni ya insulini mwili utashindwa kuhifadhi sukari pia kuitumia sukari. Hivyo sukari itabakia kwenye damu bila ya kwenda kokote kwa matumizi. Hali hii ikitokea ndipo mtu huambiwa ana kisukari. Kisukari kinaweza kuwa ni kwa muda mfupi kama kwa baadhi ya wajawazito. Pia kinaweza kuwa ni cha kudumu, na hapa tunazungumzia type1 na type 2.
Mtu mwenye kisukari anatakiwa kuwa makini sana katika matumizi ya vyakula na vinywaji. Vinginevyo anaweza kuingia kwenye matatizo makubw aya kiafya. Je unavijuwa vyakula salama kwa nmwemye kisukari? Na je unavijuwa vyakula hatari kwa mwenye kisukari? Endelea na makala hii hadi mwisho:-
VYAKULA SALAMA KWA MWENYE KISUKARI
1. Samaki hasa wale wenye fati kwa wingi kama samlon na sardines
2. Mbogamboga za majani
3. Palachichi
4. Mayai
5. Mbegu za chia
6. Maharagwe
7. Kitunguu thaumu
8. Nyama yandege wafugwao kama kuku
9. Kahawa
10. Vinywaji visivyowekwa sukari
11. Jusi za mbogamboga
12. Usikoboe mahindi, mchele, na mtama
13. Matunda kwa uchache
VYAKULA HATARI KWA MWENYE KISUKARI
1. Nafaka zilizokobolewa
2. Nafaka zilizoongezwa sukari
3. Mikate yenye sukari
4. Nafaka zisizo na kini
5. Mboga zenye chumvi nyingi
6. Mboga zilizoongezwa maziwa
7. Vinywaji vyote vya sukari usitumie mpaka kiwango chako cha sukari kiwe kipo katika udhibiti hata asali epukana nayo kwanza
8. Juisi zilizowekwa sukari ama zenye utamu kama za matunda
9. Vinywaji vya energy (energy drink)
10. Nyama ya kuoka
11. Nyama zenye mafuta mengi
12. Nyama ya ngurue
13. Maziwa fresh
14. Samaki wa kuoka
15. Soda
Njia za kujikinga na kisukari
1. Dhibiti uzito wako. Hakikisha huna uzito w akupitiliza
2. Fanya mazoezi mara kwa mara
3. Kula mlo kamili
4. Punguza misongo ya mawazo
5. Kunywa maji kwa wingi
6. Wacha kuvuta sigara
7. Punguza ama wacha unywaji wa pombe
8. Punguza ulaji wa sukari kwa wingi
9. Pendelea kunywa kahawa
10. Tumia dawa za asili kiasi uwezavyo
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu vyakula ambavyo vinasaidia kupunguza uzito, ni baadhi ya vyakula ambavyo unaweza kutumia ili kuweza kuweka kwenye hali ya kawaida.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hivi ni vyakula hatari kwa watu wenye maradhi ya moyo. Vyakula hivi si salama kwa afya ya moyo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya hatari kwa mjamzito hasa mimba changa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za majani ya mstafeli,ni majani ambayo utibu magonjwa mbalimbali hasa saratani, kwa hiyo tunapaswa kuyatumia ili tuweze kupata matibabu ya kansa mbalimbali.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea za kula nanasi na umuhimu wake kiafya
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukuletea kazi za vitamini B, pia tutajwenda kuona makundi ya vitamini B na kazi za kila kundi. Pia makala hii inakwenda kukufundisha vyanzo na vyakula vya vitamini B. Utajifunza pia kazi kuu za vitamini B kwa ujumla wake.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza faida na matumizi ya asali mwilini.
Soma Zaidi...