Afya ya uzazi na ulezi

Rajabu Athuman

AFYA YA UZAZI: BABA, MAMA NA MWANA

AFYA YA UZAZI
AFYA YA UZAZI
UTANGULIZI
SIKU YA KUPATA UJAUZITO
SIKU YA KUPATA UJAUZITO KWA MWENYE SIKU SIDOGO.
MAJIMAJI YA UKENI (CERVICAL MUCUS)
SIFA ZA UTEUTE WA UKENI (CERVICAL MUCUS)
DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO)
FANGASI SEHEMU ZA SIRI
DALILI ZA KUTOKA KWA MIMBA
SABABU ZA KUTOKA KWA MIMBA
HAYA NI HATARI KWA UJAUZITO (MIMBA)
HAYA HAYASABABISHI MIMBA KUTOKA
MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA
SABABU ZA KUKOSA HAMU YA TENDO LANDOA 11
TATIZO LA NGUZU ZA KIUME NA SABABU ZAKE 11
KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA MAPEMA 12
VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA 12
KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO 13UTANGULIZI
Afya ya uzazi huweza kufungamana na mambo mengi sana. Maradhi na mtindo wa maisha wa mtu huweza kuchukuwa nafasi kubwa katika kuzungumzia afya ya uzazi. Wazazi wengi wamekuwa wakilalamika kkuhusu swala na kushika mimba, maradhi ya kizazi pamoja na wanaume kulalamika kutokuwa na nguvu za kutosheleza haja zao. Afya ya uzazi imekuwa ikichukuwa kundi kubwa la watu pindi inapozungumziwa. Kizazi kilicho salama kinategemea ubora wa afya hii pamoja na malezi yaliyo bora kutoka kwa wazazi.


Katika makala hizi tutakwenda kuona mengi katika hayo yanayohusiana na afya ya uzazi kwa wanaume, wanawake pamoja na watoto ambao ndio kwa kiasi kikubwa afya zao. Makala hii imeandikwa kwa kuangalia tafiti za kiafya zilizofanya katika maeneo mbalimbali duniani.


Tunaheshibu na kuthamini afya ya mtu. Katu hatuthubuthu kuandika kitua bila ya marejeo, hivyo basi ukigundua chochote ambacho hakiposawa kwenye makala hii basi wasiliana nami kwa haraka zaidiSIKU YA KUPATA UJAUZITO
Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote. Seli hii hukuwa na kujakuwa mtoto kamili. Kawaida kitendo hiki hufanyika ndani ya masaa 12 toka yai kukomaa na kuletwa kwenye mirija ya falopian. Baada ya mimba kutungwa itabakia pale kwa masaa kama matatu, kisha huanza kusafirishwa na kupelekwa kwenye tumbo la mimba ambapo huku litabakia mpaka mtoto kuzaliwa.


Mwanamke hutoa yai moja kila mwezi kutoka katika ovari moja. Kuna wakati mwanamke huenda akatowa mayai zaidi ya moja, hali hii si kawaida. Yai hili linaweza kuwa hai ndani ya masaa 12 mpaka 24. hutokea pia likaweza kuwa hai mpaka masaa 48. ndani ya muda huu yai ni lazima likutane na mbegu ya kiume ili mimba itungwe. Kipindi hiki kitaalamu kinajulikana kama fertile window.


Mbegu ya mwanaume huweza kudumu kuwa hai ndani ya siku 5, ndani ya siku hizi mbegu hizi huwa zipo hai hivyo zinaweza kurutubisha yai. Mwanaume huto zaidi ya mbegu milioni 300 ejaculation moja. Katika mbegi hizi mbegu moja ndio hutakiwa kuungana na yai.


Siku za mwanamke kuweza kuwa kati ya 21 mpaka 35 inategeme na mwanamke. Kikawaida walio wengi siku zao ni 28. katika siku hizi zipo siku 6 tu ambazo mwanamke anaweza kupata ujauzito. Siku hizi huanzia siku ya 11,12,13,14,15 na 16. katika siku hizi siku ya 14 ndio ambayo huaminika zaidi kuwa yai hutolewa ziku hii. Ni vyema kukutana kimwili katika siku hizi kwa wanaotafuta ujauzito. Sio lazima pia kufululiza inawezekana kuruka ila nivyema kutoikosa siku ya 13 na 14.


Pia kuna dalili kadha za kuijua siku hii kama kuzidi kwa joto la mwanamke siku moja kabla na siku ile ya kutolewa kwa yai. Pia kuongezeka kwa utelezi kwenye shingo ya uzazi. Pia mwanamke anapenda sana kukutana kimwili kukaribia siku hii. Vipo vifaa pia vya kuitambua siku hii. Siku hizi huhesabiwa kutoka kupata hedhi na kuendelea. Pia siku hisi kutofautiana kwa wanawake.SIKU YA KUPATA UJAUZITO KWA MWENYE SIKU SIDOGO.
Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapo ambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo. Sasa ni ipi siku ya kutolewa kwa yai kwa wanawake hawa?. makala ya hapo juu katu haikugusa kipengele hiki.


Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha ongeza 2 mnyuma ndani ya siku mbili zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--


1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa mbili nyuma (9-2=7) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 9 na 7 katika siku zake.
2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku mbili tena nyuma (20-2=18) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 18 mpaka 20


MAJIMAJI YA UKENI (CERVICAL MUCUS)
Kuna mabadiliko yanayotokea kwenye mwili wa mwanamke katika mzunguruko wa siku zake. Cervical mucus ni majimaji yenye sifa tofauti tofauti yanayopatikana kwenye njia ya uzazi yaani uke. Majimaji haya yanabadilika kulingana na siku ama maradhi. Miongoni mwa sifa hizi ni kama kinata, kuteleza, kufutika, ukavu na rangi yake.


Majimaji haya yanasaidia katika kutujulisha siku ambazo ni mujarabu kwa wale ambao wanatafuta ujauzito. Pia majimaji haya ni taarifa kuwa yai lipo karibu ktolewa hivyo ni vyema kujiandaa. Majimaji haya pia yanaweza kutujulisha kama mimba imeingia ama laa. Tofauti na kazi hizi majimaji haya yana kazi zifuatazo:-
1.Kuzuia bakteria na wadudu wengine wasiingie ndani kwenye tumbo la uzazi
2.Kusafirisha mbegu za kiume (sperm) kuelekea ndani
3.Kulainisha njia ya uke na kuwa katika hali iliyo bora zaidi.


Majimaji haya huweza kutofautiana muonekano kutokana na mabadiliko ya siku. Siku hizi huanza kuhesabiwa punde tu baada ya kumalizika kwa hedhi. Ili kuchunguza majimaji haya inahitaji muda na ni vyema kutokukutana kimwili kama unataka kuchunguza mabadiliko haya katika mwezi wote hii husaidia kwani kukutana kimwili kunaweza kuathiri muonekano wa majimaji haya.


Kama unataka kuchunguza kwa baadhi ya siku tu kama kutaka kujua kama yai linakaribia basi unaweza kukaa mkao wowote ambao utafanya uke uwe wazi, kisha tumia kitambaa laini cheupe na kiingize ndani na fanya kama unapangisa kitu kwa ndani ili kuweza kuyapata majimaji haya kwa wingi. Ia unaweza kutumia kidole, baada ya hapo chunguza vyema rangi na muinekano wa majimaji haya kama kuteleza, kunata, kuvutika na uzito.


SIFA ZA UTEUTE WA UKENI (CERVICAL MUCUS)
Baada ya hedhi uke huwa mkavu hivyo majimaji haya yanakuwa ni macgache na si yenye mtelezo wowote. Hayana rangi yeyote na wala huwezi kuyapata kwa wingi. Hii huashiria kuwa muda huu mwanamke hawezi kupata ujauzito.


Siku chache baadaye majimaji yataanza kuonekana yakiwa na muonekano wa kuweza kunatanata, majimaji haya sio mepesi kabisa. Huu ni mwanzo wa kuandaliwa mazingira ya kupevushwa kwa yai.


Baada ya siku chache tu yai linakaribia kutolewa, muda huu majimaji haya yanakuwa mepesi, laini, mengi na yenye rangi nyeupe. Haya maji ni kiashiria kuwa sasa yai lipo njiani kutolewa. Huu ni muda muafaka zaidi kwa wanaotafuta mtoto.


Siku moja ama mbili kabla ya yao kutolewa majimaji haya yanafanana sana na majimaji ya weupe wa yai, yaani kama yale majmaji meupe yanayooekana pindi linapopasuliwa yai. Majimaji haya yanaweza kuvutika kwenye vidole na yanateleza sana. Hii ni ishara kuwa yai limekaribia kutolewa eidha kwa siku moja ama mbili.


Punde baada ya yai kutolewa majimaji haya yanaanza kuwa makavu na kupoteza mtelezo. Ama uke unakauka na kuwa mkavu na kurudi katika hali ya kawaida. Na kama mimba ilitungwa majimaji haya yanakuwa na rangi ya maziwa. Hivyo ni vyema kuchunguza vizuri ili kujuwa kama mimba ilitungwa au laa.


Pia ijulikane kuwa kuna wanawake wengine hawana majimaji haya na pia kuna wengine ambao majimaji haya ni mengi sana zaidi ya kawaida. Hivyo katika kuchunguza hali hizi wanawake wa aina hii ni ngumu sana kwao.
DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO)
Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupotea bila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua. Wapo wengine wanakujakujitambua ujauzito ukiwa na miezi kadhaa. Sasa ni zipi hasa dalili za ujauzito?. huenda swali hili kwa wanawake walio wengi lisiwe na manufaa kwao kwani tajari ni wajuzi wa swala hili. Halikadhalika wanaume wengi wanaujuzi pia. Kwani wengi wanaelewa kuwa dalili ya ujauzito ni kukosekana kwa siku za mwanamke yaani hedhi kwa vipindi zaidi ya kipoja. Lakini itambulike kuwa hii sio dalili pekee, kwani siku zinaweza kukosekana na isiwe mimba. Katika makala hii tutakwenda kuonesha kwa utani dalili kadhaa za ujauzito.


Kabla ya kiziona dalili hizo ningependa kutumia muda kidogo kueleza tatizo la kukosa kwa hedhi. Hedhi ni muhimu kwa kila mwanmke ambaye amefikia umri wa kupata ujauzito. Afya ya mwanmke huyu huwa salama kama hedhi yake ipo salama. Kwa kawaida hedhi huweza kukatika yaani kukata kutoka kabisa pindi umri wa mwanamke unapokuwa mkubwa yaani kuanzia miaka ya 45 na kuendelea. Katika kipindi hiki mwanamke huyu kupata tatizo la kutokupata siku zake ni la kawaida sana, ama siku zake kutokuwa na mpangilio maalumu.
Kwa wanawake walio wadogo kukata kwa hedhi kuna sababi nyingi sana. Watu wengi wamezoea kuwa lamda kupata ujauzito ndio sababu ya kutokupata siku zake. Hii sio swa kabisa. Kukata kwa siku za mwanamke kunaweza kusababishwa na maradhi kama kisukari na baadhi ya maradhi yanayoipata ovari ya mwanamke. Ovari ndio sehemu pekee ya mwanamke ambayo mayai huzaliwa. Hivyo sehemu hii ndio ambayo inatoa homoni ambazo huchochea upatikanaji wa hedhi ama huzuia hedhi isipatikane kutokana na kupata ujauzito. Pia matumizi ya njia za uzazi wa mpango huweza kusababisha tatizo hili la kutokuona siku zake mwanamke. Matumizi ya vyakula, hali ya hewa na madawa ni katika visababishi vikuu vya kutokupata hedhi kwa muda sahihi.


Baada ya kugusia kidogo kipengele hiko sasa tukaone baadhi ya dalili za ujauzito. Kwa hali ya kawaida dalili hizi huweza kuwa tofauti kwa mwanamke mmoja hadi mwingine. Ijapokuwa hali ni kama hii pia zipo dalili ambazo huwapata karibia wanawake wote:-


Kuonekana kwa damu iliyo chache. Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa asilimia 25% (yaani robo) ya wanawake wote wanaopata ujauzito hutokwa na damu kidogo, na rangi ya damu hii haikuiva kama ile ya hedhi. Damu hii hutokea siku 6 mpaka 12 baada ya kutungwa kwa mimba. Ila kwa wanawake walio wengi huiona damu hii kwenye wiki 12 za mwanzo za ujauzito.


Kujaa au kuuma kwa chuchu; mwanzoni mwa wiki ya 1 mpaka ya 2 ya ujauzito mwanamke anaweza kuona kuwa matiti yake yanajaa ama kuwa mazito tofauti na kawaida. Wanawake wengine chuchu za matiti yao zinakuwa ngumu na huwa zinajaa. Wanawake wengine wanaona chuchu ama maziwa yao huwa kama na maumivu wakiyaminya.


Uchovu isio wa kawaida; karibia wanawake wote wanaopata ujauzito huhisi uchovu usio wa kawaida. Mara nyingi dalili hii hutokea mwanzoni mwa wiki ya kwanza toka kupata kwa ujauzito. Na hii ni kutokana na kuwa mwili unazalisha homoni za kuweza kuufanya mwili uweze kulea ujauzito, upatikanaji nwa maziwa kwa ajili ya mtoto ajae. Pia kwa kuwa mwili wa mama unaongeza kuwango cha usukumaji wa damu, hivyo uchovu kutokea ni hali ya kawaida.


Mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya ujaozito, mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya ghafla ya kichwa. Na hii ni kutokana kuwa mwili umeongeza kazi ya uzalishaji wa homoni, hivyo ongezeko hili linaweza kusababisha maumivu ya kishwa. Hali si kwa siku nyingi hali hii itapotea.


Kutapika; kwa kawaida hii hali huwapata wanawake wenye ujauzito kuanzia wiki ya pili mpaka wiki ya nane. Kitaalamu hali hii hutambulika kama “morning sickness”. na huenda hali hii ikaendelea katika kipindi chote cha ujauzito.


Kukojoa mara kwa mara; hali hii hutokea kwa sababu mwili huzalisha homoni iitwayo human chorionic gonadotropin ambayo hii huongeza damu kupita maeneo ya chini yaani kuzunguka sehemu za siri, hivyo hali hii hupelekea mwanamke kwenda kukojoa mara kwa mara.


Kutokupenda baadhi ya vitu ama vyakula. Hii hutokea kwa ghafla mwanamke anachukia baadhi ya vitu ama hususani vyakula bila ya sababu yotyote.


FANGASI SEHEMU ZA SIRI
Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Fangasi ni hatari sana, kwani wanaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya na kiakili kama wasipitibiwa mapema. Kuna aina nyingi za fangasi ambao wanaweza kuathiri mwili wa binadamu.


Kuna mamilioni ya aina hizi za fangasi, katika hawa kuna kuna mamia ya aina za fangasi ambazo huweza kumfanya mtu kuumwa. Fangasi wanaweza kuathiri makwapa, vidole, sehemu za siri kwenye tumbo na maeneo mengine.


Fangasi wa sehemu za siri husababishwa na fangasi waitwao candida. Hawa wanaweza kuathiri sehemu za siri kuzungukia uume ama uke. Kunatafiti zinaonesha kuwa fangasi hawa wanaweza kuambukizwa kwa kufanya mapenzi. Japo tafiti zaidi zinahitajika ili kuthibitisha hili.


FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI DALILI ZAO KWA WANAUME
1.Kuvimba kwa kichwa cha uume
2.Kuwasha kwa sehemu za siri, hususan kichwa cha uume
3.Uume kuwa mwekundu kwa kuchubuka ama kuvumba ama kwa mashambulizi ya fangasi hawa.
4.Kuota kwa mapele na maruturutu kwenye uume
5.Kuwasha uume ama kuungua moto kwa uume.
6.Kutokwa na majimaji meupe kwenye uume, majimaji haya huwa na harufu mbaya.
7.Maumivu wakati wa kukojoa na kufanya tendo la ndoa.


DALILI ZA FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE
1.Maumivu na miwasho kwenye mashavu ya uke na sehemu ya juu ya uke
2.Maumivu wakati wa kukojoa ama kufanya tendo la ndoa
3.Uuke kuwaka moto kwa ndani
4.Kuvimba kwa mashavu ya uke na kuwa mekundu
5.Kuot mapele na maruturutu kwenye uke
6.Kutokwa na majimaji kwenye uke
7.Kutokwa na majimaji mazito meupe na yenye harufu mbaya kwenye uke.


WATU WALIO HATARINI KUPATA FANGASI HAWA
1.Wachafu
2.Kuwa na mikunjomikunjo kwenye ngozi kama kitambi
3.Wenye kisukari
4.Wenye HIV
5.Wenye saratani
6.Wenye kutumia baadhi ya madawa ya kuzuia mimba
7.Wajawazito


NJIA ZA KUPAMBANA NA FANGASI HAWA
1.Kuwacha kutumia madawa ya kusafishia ama kuunga uke
2.Kutokuvaa nguo mbichi
3.Kutokuvaa nguo za kubana hususani za mpira
4.Kuwa msafi muda wowote
5.Kuosha kichwa cha uume na ngozi ya govi mara kwa mara
6.Kuosha uke mara kwa mara
7.Kutumia pedi zilizo kavua na safi na kubadilisha mara kwa mara


DALILI ZA KUTOKA KWA MIMBA
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Yaani karibia robo ya mimba zinazopatikana hutoka. Kitendo hiki cha kutoka kitaalamu huitwa misscarriage. Hiki ni kitendo cha kupotea kwa ujauzito kabla ya wiki ya 20. karibia mimba nyingi hutoka ndani ya miezi mitatu ya mwanzo. Mimba iliyotoka inakuwa na dalili kadhaa. Pia wakati mwingine dalili hizi huashiria kuwa ujauzito upo hatarini.


Dalili hizi ni kama;
1.Kutokwa na damu nyingi ukeni. Mjamzito anaweza kuona damu ikitoka ikiwa chache yaani matone kadhaa ama madoa hii ni kawaida. Lakini ikiwa nyingi huashiria hatari kwa ujauzito.
2.Kupungua uzito kwa ghafla. Bila ya kujuwa sababu yeyote mjamzito anapungua uzito wake kwa ghafla sana.
3.Kutokwa na uteute wa rangi ya pink iliyo pauka kwenye uke
4.Kuondoka kwa dalili za ujauzito kwa ghafla
5.Kutokwa na tishu yaani kama vipande vya nyama vinatoka ukeni
6.Maumivu makali ya mgongo ama tumbo


SABABU ZA KUTOKA KWA MIMBA
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Yaani karibia robo ya mimba zinazopatikana hutoka. Kitendo hiki cha kutoka kitaalamu huitwa misscarriage. Hiki ni kitendo cha kupotea kwa ujauzito kabla ya wiki ya 20.


Sababu za kutoka kwa mimba:
1.Sababu za kurithi (genetics): hutokea mwanamke akarithi hizi sabau kutoka kwenye familia yake. Sababu hizi huenda zikapelekea matatizo ambayo baadaye huchangia mimba kutoka. Matatizo haya ni kama
?Mtoto kutokuendelea kukuwa tumboni
?Kiini tete (embriyo) kutokutengenezwa
?Placenta kuwa kubwa zaidi tofauti na kawaida.


2.Afya ya mama; hutokea mwanamke mjamzito afya yake ikawa ni sababu ya ujauzito wake kutoka. Mwanamke akiwa na maradhi yafuatayo ujauzito wake unaweza kuwa hatarini:
?Kisukari
?Maradhi ya moyo
?Presha ya kupanda (hypertension)
?Maradhi ya figo


3.Maambukizi; mwanamke mjamzito anweza kuweka ujauzito wake hatarini kama atakuwa na maambukizi ama mashambulizi ya maradhi kama:
?Chlamydia
?Gonoria
?Syphilis
?Malaria
?Ukimwi


4.Udhaifu wa cervix; cervics ni mlango wa nyumba ya mimba.
5.PCOS (Polycystic Ovary Syndrome). hii hupelekea ovary kuwa kubwa tofauti na kawaida. Ovary ndio sehemu ambayo mayai ya mwanamke hutengenezwa.


HAYA NI HATARI KWA UJAUZITO (MIMBA)
Tofauti na mambo matano yaliyotajwa hapo juu kuwa yanapelekea ujauzito kutoka, kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuuweka ujauzito kuwa hatarini. Mambo haya yenyewe hayawezi kusababisha ujauzito kutoka ila yanaweza kuongeza hatari ya ujauzito kutoka pindi yakiambatana na mambo matani niliyotangulia kuyataja hapo juu. Mambo haya ni kama:
1.Kuwa na umri mkubwa kuanzia miaka 35 mpaka 40
2.Kuzidi kwa uzito mwilini
3.Uvutaji wa sigara
4.Unywaji wa pombe
5.Ulaji wa caffeine nyingi kupita kiasi. Caffein hupatikana kwenye chai.
6.Sumu za kwenye vyakula, kama kwenye nyama.
7.Matumizi ya baadhi ya madawa kama
?Misoprostol
?Retinoids
?Methotrexate
?NSAIDs kama ibuprofen
8.Maambukizi na mashabulizi ya
?HIV
?Cytomegalovirus
?Bacterial vaginosis
?Gonorrhea
?Chlamydia
?Malaria
?Syphilis
9.Kisukari


HAYA HAYASABABISHI MIMBA KUTOKA
1.Kufanya mazoezi
2.Kufanya kazi
3.Kula vyakula vinavyowasha kama vyenye pilipili
4.Kufanya tendo la ndoa
5.Kupata msituko
6.Kuwa na mawazo


MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA
Maumivu wakati wa tendo la ndoa kitaalamu huitwa dyspareunia. Maumivu haya hutokea kwa namna mbalimbali. Mara nyingi maumivu haya huwapata wanawake. Mara chache wanaume wanapokuwa na maradhi flani kama fangasi kwenye uume ama maradhi mengine ya ngono ndipo hupata maumivu haya.


Maumivu haya hutokea pundi:
1.Pindi uume unapoingia ukeni kwa mara ya kwanza
2.Kila wakati uume unapoingia ukeni
3.Maumivu wakati wa kupushi na kutoka kwa uume
4.Kuhisi kuungua ukeni
5.Maumivu baada ya kufanya tendo la ndoa


Sababu za maumivu haya
?Kutokuwepo kwa uteute wa kutosha wa kulainisha uke
?Majeraha na makovu ukeni kama waliotahiriwa
?Kuvimba kwa uke ama kuwa na mashambulizi ya bakteria
?Matatizo ya saikolojia
?Kukaza kwa misuli ya uke
?Maumbile ya uuke kama kuwepo kwa utando unaozuia njia ya uke kuwa wazi
?Kufanyiwa upasuaji kama hysterectomy ama matibabu ya saratani
?Kuwa na msongo wa mawazo


SABABU ZA KUKOSA HAMU YA TENDO LANDOA
Hii ni hali inayompata mtu kukosa hamu kabisa ya kushiriki kitendo chochote kinachohusiana na kufanya tendo landoa au bunyeto. Hali hii kitaalamu hufahamika kama hypoactive sexual desire disorder (HSDD). Pia kuna watu wengine wanakuwa na hisia chache kuhusu kitendo hiki. Hali hii huwapata wanaume na wanawake. Sababu za kukosa kabisa hamu ya tendo la ndoa ama hamu kuwa ndogo, sababu zao wote hufanana.


Sababu za kutokea kwa hali mbili hizi:
1.Mumivu wakati wa tendo la ndoa
2.Matumizi ya baadhi ya madawa ya arthritis, saratani, kisukari, presha ya kupanda, maradhi ya moyo na maradhi ya mfumo wa fahamu
3.Namna ya mtu anavyoishi kwa mfao unywaji wa pombe kupitiliza
4.Kama mtu alifanyiwa upasuaji maeneo ya nyeti kama matiti, kwenye uke
5.Uchovu
6.Matatizo katika homoni
7.Afya ya akili
8.Kuwa na msongo wa mawazo
9.Kutokujiamini
10.Mahusiano yasiyo mazuri na mwenza
TATIZO LA NGUZU ZA KIUME NA SABABU ZAKE
Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa. Hii huwenda kuwa uume unashindwa kusimama (kutisa) kwa kwa muda mrefu, ama unashindwa kabisa kusimama. Kitaalamu hali hii hufahamika kama erectile dysfunction. Hali hii haihusishi wale wenye tatizo la kumaliza hamu mapema (premature ejaculation) yaani wanaomaliza haja yao hata kabla ya mwenza kuridhika.


Sababu za tatizo hili
1.Kuwa na maradhi ya moyo
2.Kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis)
3.Kuwa na mafuta mengi mwilini (high cholesterol)
4.Kuwa na presha ya kupanda (high blood pressure)
5.Kisukari
6.Matumizi ya baadhi ya madawa
7.Uvutaji wa sigara
8.Maradhi kwenye uume kama peyronie
9.Unywaji wa pombe
10.Utumiaji wa madawa ya kulevya
11.Matibabu ya saratani ya korodani
12.Upasuaji katika maeneo nyeti au ugwe mgongo
13.Kuwa na mdongo wa mawazo ama woga
14.Mahusiano yasiyo mazuri
15.Kuwa na uzito kupitiliza


KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA MAPEMA
Hii ni hali inayowapata sana wanaume huwa wanamaliza hamu ya tendo la ndoa mapema kabla ya mwenza kuridhika. Hii hutokea pale mwanaume anapomwaga mbegu mapema sekunde chache ama muda mchache baada ya kuingiza uume ukeni. Wengi wenye tatizo hili humwaga ndani ya dakika moja na tatizo huwa baya zaidi kwa wengine ambao humwaga ndani ya sekunde 30 baada ya kuingi za uume. Hali hii kitaalamu hujulikana kama premature ejaculation.


Hali hii huweza kuambatana na mambo mengi hususani matatizo ya kisaikolojia, maradhi ama maumbile. Wakati mwingine hali hii humpata mwanaume yeyote hata kama sio muathirika wa tatizo hili. Ila hii huwa ni tatizo kama hali hii itakuwa inajirudia rudia muda mwingi.


Sababu za tatizo hili:
1.matatizo kwenye mfumo wa homoni
2.Maradhi na kuwepo uvimbe kwenye korodani
3.Kurithi tatizo hili kwenye familia
4.Kuwa na msongo wa mawazo
5.Kuwa na tatizo la uume kunywea mapema
6.Uwoga na msongo wa mawazo
7.Kutokupendezewa na umbo la mwenza
8.Mahusiano yaliyo mabovu
9.Kuogopa kumaliza tendo mapema


VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA
Matatizo yahusianayo na nguvu za kume na kukosa hamu ya tendo la ndoa kwahuweza kuchangiwa sana na mpangilio mbovu wa vyakula pamoja na saikolojia ya mtu. Ni vyema kujiweka tayari kisaikolojia kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Kwa upande wa vyakula ni vyema kuchaguwa vyakula vilivyo salama kwa afya. Vyakula vyenye mafuta kupitiliza vinaweza kuleta athari mbaya kwa afya ya nguvu za kiume. Katika makala hii nitakuletea vyakula vitano ambavyo husaidia katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa:


Vyakula hivyo ni:
1.Vyakula vyenye arginine . Vyakula hivi vina ni vyakula vyenye chembechembe itambulikayo kama arginine. Ndani ya miili yetu arginine huweza kubadilishwa kuwa oxide ya nitric (nitric oxide). Arginine ni chembechembe za asidi ya amono (amino acid). vyakula vyenvye arginine ni kama maharage ya soya, mbegu za maboga, karanga, korosho, samaki, nyama, kuku na samaki.


Arginine imafaida nyingi sana mwilini. Chembechembe hii huweza kutibu tatizo la kusinyaa kwa uume kabla ya kumwaga, ama kusinyaa mapema, ama kugoma kabisa kusiama. Kama tatizo hili linahusiana na mishipa ya damua kama kuziba kwa mishiba ya damu basi arginine ni msaada mkubwa. Pia husaidia kuimarisha afya kwa wenye kisukari na wenye maradhi ya moyo hususani yanayohusiana na mishipa ya damu kama kujaa mafuta ama kuziba.


2.Vyakula vyenye phytochemical: vyakula hivi ni kama maepo (apples),mboga za apricots, broccoli, Brussels sprouts, kabichi (cabbage), karoto (carrots), cauliflower, kitunguu thaumu (garlic), mimea jamii ya kunde (legumes), kitunguu maji (onion), pilipili kali (red peppers), maharage ya soya (soybeans), viazi vitamu (sweet potatoes), na nyanya (tomatoes).


3.Vyakula vya fati iliyo salama kwa afya ya moyo. Afya ya moyo huchukuwa nafasi kubwa katika tendo la ndoa. Uzima wa moyo huweza kufanya damu kutembea vyama maeneo yote ya mwili hususani maeneo yanayohusika katika tendo la ndoa.


Miongoni mwa vyakula hivi ni palachichi. Ndani ya palachichi kuna fat, vitamini B6 asidi ya folik (folic acid) kwa hamoja hizi husaidia kuongeza nishati mwilini na kuimarisha afya katika kushiriki tendo la ndoa. Vyakula vingine ni kama aina flani ya samaki, mayai, mbegu za chia, chokleti, bidhaa za maziwa kama siagi n.k


4.Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe hii ni kuwa arginine. Faida za arginine tumeshaziona hapo juu. Chemikali hizi pia husaidia katika kuufanya mwili uweze kuwa shwari (relax) kama vile viagra inavyofanya kazi.


Miongoni mwa vyakula hivi ni tikitimaji. Tunda hili lina citrulline kwa wingi sana tofauti na matunda mengi. Vyakula vingine ni kama maboga, matang n.k. citrulline pia husaidia katika kutanua misuli na kuboresha mishipa ya damu kufanya kazi vyema hivyo ni nzuri kwa wanaofanya mazoezi. Kwa upande wa afya ya tendo la ndoa husaidia katika kupeleka damu kwenye maeneo nyeti.


5.Vyakula vyenye Indole-3-carbinol: hii husaidia katika kuboresha homoni hasa kwa wanaume. Huweza kupatikana kwenye mboga za majani kama kabichi, broccoli na mboga nyinginezo. Tofauti na faida hizi pia huweza kusaidia katika kuzuia na kupunguza athari za saratani ya matiti, tumbo, na nyinginezo.


KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO
Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito. Kitaalamu hali hii hutambulika kama odema. Wakati mwingine si miguu tu ndio huvimba bali mikono, nyayo na uso huweza kuvimba. Ijapouwa huku kukuvimba kwa ghafla kwa uso na mikono ni dalili ya maradhi mengine kama preeclampsia.


Hali hii ya kuvimba kwa miguu huweza kuwapata wanawake katika kipindi chote cha ujauzito, iwe wajauzito ulio mchanga, ama kipindi cha katikati cha ujauzito ama kipindi cha mwisho cha ujauzito. Katika hali ya kawaida kuvimba kwa miguu kwa wajawazito sio jambo la kusumbua kiafya yaani kusema kuwa ni tatizo kubwa. Hapana hii ni kawaida kwa wajawazito.


Kuvimba huku kunaweza kuwa ni tatizo kama kutaweza kuambatana na baadhi ya matatizo mengine ya kiafya kama maumivu makali ya kicha, kizunguzungu, kutokwa na damu, kushinwa kuona kwa usahihi ama kushinwa kupumua ama kupumua kwa taabu, hali hizi kuweza kuashiria hatari. Ni vyema mjamzito awahi kituo cha afya kama ana hali hizi.


Sababu za kutokea kwa vimbe hizi ni mabadiliko ya mwilini yanayopatikana wakati wa ujauzito. Kuongezeka kwa damu mwilini na kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kuchangia zaidi hali hii. Halikadhalika ongezeko la homoni maalumu zinazotolewa wakati wa ujauzito. Haya yote kwa pamoja huchangia kutokea hali hizi za kuvimba.


Tofauti na sababu hizi pia zipo nyingine kama mabadiliko ya hali ya hewa. Hapa tunazungumzia joto, ambalo pia ni sababu ya kuvimba. Sababu nyingine ni kutokunywa maji ya kutosha, matatizo ya homoni yaani homone imbalance. Kukaachini kwa muda mrefu ukaaji wa kukalia miguu. Ama kusimama kwa muda mefu.


Kupunguza ama kuepuka hali hii ni vyema kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kukaa kivulini, kulalia upande kwa kushoto unapolala. Hakikisha unakula mlo kamili, hakikisha kuwa unakunywa maji ya kutoka kwa siku. Na hata ukizidisha ni faida kwako. Epuka kusimama kwa muda mrefu ama kukaa kwa kukalia mguu. Epuka kukaa kwa muda mrefu kwa staili moja.


ENDELEA NA DARASA HILI


Unaweza kuendelea na somo hili la afya ya uzani, mama na mwana. Kuendelea na darasa hili pata kitabu chetu kizima kwa bei poa tu. Wasiliana nasi kwa mawasiliano hapo chini.


Unaweza pia kupata mwendelezo wa darasa hili ukiwa kwenye tovuti yetu www.bongoclass.com. bongoclass imejipanga vyema kukupatia elimu bure.


Mawasiliano:
Phone: 0620555380
Email: [email protected]
Tovuti: www.bongoclass.com


[ www.bongoclass.com
]Download kitabu hiki hapa