JIFUNZE NAMNA YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA MAFUA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

JIFUNZE NAMNA YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA MAFUA

5.MAFUA
Mafua ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya mafua na pia inasadikika kuwa zipo takribani aina 200 za virusi hawa wa mafua wakiwemo rhinoviruses, parainfluenza viruses, enteroinfluenza viruses na vingine vingi. Virusi hivi hupatikana kwa kukutana na hewa yenye virusi hawa, pindi unapovuta hewa yenye mchanganyiko wa virusi hawa. Sababu zingine zinazosadikika kusababisha mafua ni panoja na sigara, moshi, mavumbi, baridi kuwa kali au kuchafuka kwa hewa.

Udonjwa wa mafua unadalili tofauti tofauti na huenda zikafanana na ugonjwa wa malaria. Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na kukosa hamu ya kula, kuhisi uchovu, kutokwa na makamasi mengi, koo kukereketa, maumivu ya kichwa na kupiga chafya mara kwa mara. Japo dalili za mafua hutofautiona kwa mtu na mtu kulingana na uwezo wa mwili wake kupambana na magonjwa ila hizi dalili tulizozitaja huwa maarufu kwa watu wengi.

Mgonjwa wa mafua huenda akawa amechoka sana kiasi kwamba analala kitandani kwa homa kali aliyo nayo. Mafua huwaathiri zaidi watoto na wazee kwani miili yao haina kinga za kutosha kupambana na maradhi. Kwa wale wenye HIV+ ugonjwa wa mafua pia hueza ukawaletea athari kubwa sana ikiwemo homa kali na uchovu.

Mtu ana weza kujikinga na mafua kwa kuosha mikono kabla na baada ya kula, kuziba mdomo anapopiga chafya. Kula vyakula vyenye vitamin A na C kwa wingi, kunywa maji mengi na kupunguza mawazo yaani ”stress” kwa lunga ya kigeni hapa kinacho maanishwa ni kuwa na furaha. Jambo la msingi limgine ni kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mare humuepusha mtu na mafua kwa kiasi kikubwa.

Miongoni mwa vyakula anavyotakiwa ale mwenye mafua ni kama mboga za majani zenye vitanimi kwa wingi, kwa mfano spinach, na mchicha. Pia kula matunda yenye vitamin C kwa wingi kama mapapai, na machungwa. Vyakula hivi husaidia katika kuupa mwili uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi na mashambulizi mengine. Maji ya kutosha humsaidia mtu mwili wake kuweza kufanya kazi ya kudhibiti maambukizi kwa urahisi. Hali kadhalika kufaya mazoezi husaidia mwili kufanya kazi vizuri. Pia anashauriwa mgomjwa wa mafua awe chai.

Wapo baadhi ya wataalamu wa tiba mbadala wanazungumzia matumizi ya kitunguu maji kuhusu kutibu mafua. Wanatumia harufu ya kitunguu maji kutibu mafua. Mgonjwa atachukuwa kitunguu kasha ataondowa majani, au maganda ya juu kisha atakuwa anavuta haruvu ya kitungu. Atafanya hivyo kwa mara kadhaa hasa anapokwenda kulala.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 643

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Dua za Mitume na Manabii    πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

Ukuaji wa mmea

Je wajua kwa nini mmea kama nyasi na miti hukua? Posti hii inahusuΒ  zaidi ukuaji wa mimea katika mazingira yetu kwa sababu watu hawatambui kwamba mimea .ni chanzo cha mahitaji kwa binadamu.

Soma Zaidi...
utaratibu wa lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
kitabu cha matunda

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
dondoo 100 za Afya

Basi tambua haya;- 61.

Soma Zaidi...
YANAYOATHIRI AFYA KUTOKANA NA VIZAZI, FAMILIA NA KURITHI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Masomo ya Afya kwa kiswahili

Makala za afya zilizopata kusomwa zaidi kutoka bongoclass kitengo cha afya

Soma Zaidi...
Dua Sehemu ya 02

Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa.

Soma Zaidi...
Dondoo za afya 1-20

Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya

Soma Zaidi...
KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI)

Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika.

Soma Zaidi...