image

ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN

ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido.

ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN

zIJUWE ASBAB NUZUL ZA SURA NA AYA KWENYE QURAN

Bongoclass Dini

ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN

ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN
Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido. Ilikuwa ikishuka kwa matukio ili kutoa ufafanuzi juu ya utaratibu maalumu wa dini unaotakiwa kutumiwa. Wakati mwingine zilikuwa zikishuka aya hata bila ya kutokea tukio. Katika makala hii tutakwenda kuona sababu zilizopelekea kushuka sura na aya mbalimbali kwenye quran. Makala hii ni ya mwendelezo hivyo ukimaliza kuisoma leo ukija tena siku nyingine unaweza kukuta mwendelezo zaidi:



Fadhila za surat al-Fatiha
1.SURAT AL-FATIHA.
Muhadithina wengi wanaeleza ya kuwa sura hii nzima ilishuka Makka, na toka mwanzo ilikuwa ni sehemu ya maombi ya Waislamu. Hii ndiyo sura iliyotajwa katika aya ya Qur'an, Na kwa yakini Tumekwisha kupa (Aya) saba zisomwazo mara kwa mara na Qur'an kubwa (sura 15:88), ambayo ilishuka Makka. Habari zingine zinaeleza ya kuwa sura hii iliteremshwa tena mara ya pili, Madina. Sura hii ilishuka mapema tu Mtume s.a.w. alipoanza kazi.


MAJINA YA SURA HII NA MAANA YAO.
Jina maarufu la sura hii ni Faatihat-ul-Kitaab (Inayofungua Kitabu) (Tirmidhi na Muslim). Baadaye jina hilo lilifupishwa kuwa Surat-ul-Faatihah, au Al-Faatiha. Sura hii imepewa majina mengi, na haya kumi ndiyo yaliyo sahihi zaidi: Al-Faatiha, As-Salaat (Sala), Al-Hamdu (Sifa njema), Ummul-Qur'aan (Mama ya Qur'an), Al-Qur'aan-ul-Adhiim (Qur'an Kubwa) As-Sab'ul-Mathaani (Aya saba zinazosomwa mara kwa mara), Ummul-Kitaab (Mama ya Kitabu), Ash-Shifaa (Ponyo), Ar-Ruqya (Kago), Al-Kanz (Hazina).
Maulamaa wa elimu za Qurani hawakutoa zaidi ufafanuzi wa sababu ya kushuka kwa sura hii. Au jambo hili halikuwashughulisha kabisa.


FADHILA ZA SURA HII
Amesimulia Ibn ‘Abas kuwa “wakati ambao jibril alikuwa amekaa na Mtume akasikia sauti ya mlango uliofunguliwa juu yake akanyanyu kichwa chake kisha akasema “hiyo ni nsauti ya mlango uliopo mbinguni umefunguliwa siku ya leo, na katu haujawahi kufunguliwa ila ni leo tu (ndio mara ya kwanza kufunguliwa). Basi akashuka Malaika kutoka kwenye mlango huu akasema (Jibril) huyu ni malaika ameshuka duniani na hajawahi kushuka kamwe ila ni leo tu akatoa salamu (malaika huyo) kisha akasema (kumwambia mtume) tuo habari za furaha kwa nuru mbili ulizopewa na hakuwahi kupewa mtume yeyote kabla yako kamwe (ambazo ni) surat al-fatiha na aya za mwisho za surat al-baqarah hatusoma herufi yeyote isipokuwa utapewa” (amepokea Muslim). Amesema Mtume “surat al-fatiha ni dawa ya kila gonjwa” amepokea Bayhaqiy)



Sababu za kushuka surat al-Falaq na surat an-Nas na fadhila za kusoma sura hizi
SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS)
Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s.a.w) alirogwa na wachawi wa kiyahudi kwa kutumia nywele zake kisha uchawi ule wakautumbukiza kwenye kisima cah Banu quraidha, na aliyewapa nywele wachawi hao ni labid ibn Aa€™swam. Mtume aliumwa kwa muda wa miezi sita iala uchawi huu haukuathiri akili yake. Hata sikumoja alipolala wakaja malaika wawili na mmoja wao akauliza kumuuliza mwenziwe ana nini huyu (Mtume) yule wa pili akajibu amerogwa kisha akaeleza namna alivyorogwa na mwisho akaeleza tiba ya uchawi ule ndipo akasoma sura mbili hizi. Na hii ndiyo husemwa sababu ya kushuka kwa sura hizi. Sura hizi zimeteremka madina.


FADHILA ZA SURA HIZI
Amesimulia ‘Abdallah Ibnhabib kuwa Mtume amesema “QUL HUWA LLAHU AHADU na mu’awadhatayn (qul a’udhu birabin-nasi na qul a’udhu birabil-falaq) (mwenye kuzisoma ) asubuhi na jioni zinatosheleza kwa kila kitu.(amepokea ahmad, Tirmidh na Nisai).



Sababu za kushuka surat al-Ikhlas
3.SURATUL-IKHLAS.
Inaelezwa kuwa walimfuata Mayahudu kumfata mtume (s.a.w) na kumwambia awasifie namna ambavyo Mola wake alivyo ndipo Allah akaishusha sura hii. Pia katika kauli nyingine ni kuwa Makafiri waliokuwa wakiabudia masanamu walimwendea Mtume (s.a.w) na kumwambia awaeleze sifa na namana Mola wake alivyo ndipo Allah akateremsha sura hii. Sura hii ni katika sura za mwanzo kabisa kushuka Makka na mafundisho yake yanavunja kabisa ibada ya masanamu na Ukristo na kila mafundisho ya miungu wengi.


Mama Aisha anasimulia ya kwamba Mtume s.a.w. alipokuwa akienda kitandani kwake kila usiku, aliunganisha vitanga vya mikono yake, kisha anavisomea Qul huwallaahu na Qul a'uudhu birabbil falaq na Qul a'uudhu birabbinnaas, na anavipulizia, kisha anavipaka mwili wake wote kila anapoweza kupagusa toka kichwani; na akifanya hivyo mara tatu (Bukhari jalada la 3).


FADHILA ZA SURAT AL-IKHLAS
Amesimulia ‘Abdallah Ibnhabib kuwa Mtume amesema “QUL HUWA LLAHU AHADU na mu’awadhatayn (qul a’udhu birabin-nasi na qul a’udhu birabil-falaq) (mwenye kuzisoma ) asubuhi na jioni zinatosheleza kwa kila kitu.(amepokea ahmad, Tirmidh na Nisai).



4.SURATUL-MASAD
Sura hii pia ni katika sura za kushuka Maka. Wanaeleza Maulamaa kuwa sababu ya kushuka sura hii ni kuwa mtume (s.a.w) alipopewa amri ya kulingania bila ya siri aliwaita watu wa Maka ili awalinganie na hapo baba yake mdogo Mtume (s.a.w) aitwaye Abdul a€?Uzza ambaye Qurani imemuita Abuu Lahabi yaani baba wa moto alitowa maneno ya upumbavyu na upuuzi juu ya ujumbe wa Allah na hapo Allah akateremksha sura hii.


Huyu Abu Lahab jina lake hasa ni Abdul Uzza, naye alikuwa baba mdogo wa Mtume s.a.w. Neno Abuu Lahab - baba wa miali ya moto - ni jina ambalo hutumika kwa ajili ya mtu ambaye hali yake n nya asili ni ya moto na ya uasi, na pia hutumika kwa ajili ya mtu ambaye anawachochea wengine. Hivyo bwana huyu amepangwa jina hili na Qur'an kwa sababu ya uadui wake kwa Mtume s.a.w.


Siku ya kwanza Mtume alipowaita Wakureishi ili kuwaeleza habari za ujumbe wake, huyu Abu Lahab, alimkaripia akasema, "Uangamizwe, je umetuitia maneno haya!" (Bukhari). Na ilikuwa desturi yake kila mara kumfuata Mtume aendako na kuwaambia watu wasimsikilize, akisema, Mtume ni jamaa yake na ni mwehu. Kadhalika mkewe Abu Lahab aliyeitwa Ummi Jamil bint Harb, dada wa Abu Sufiyan, alikuwa mwanamke mbaya sana aliyekuwa anamwudhi sana Mtume na kumsumbua na hata kumsingizia-singizia mambo ya upuuzi. Na kwa sababu ya masingizio yake ameitwa mchukuzi wa kuni (Bukhari), ambazo kwazo amejikokea moto wa Jahanamu, (Razi).


FADHILA ZA SURAT HII
fadhila za sura hii ni kama za sura nyingine kuwa utapata thawabu. Hakuna hadithi sahihi iliyonukuliwa kueleza fadhila za surahii kama zinavyotajwa sura nyingine. zipo baadhi ya nukuu zinanukuliwa kuwa Mtume (s.a.w) amesema "mwenye kusoma sura hii, hatakuwa makazi sawa na Abuu lahab". Haikunukuliwa hadithi hii katika vitabu vikuu va hadith, na sikuweza kupata ushahidi juu ya usahihi wa hadithi hii.



Sababu za kushuka surat an-Nasr (idhaa jaa)
SURATUN-NASR
Sura hii imeteremka wakati Mtume (s.a.w) hupo maka wakati wa hija ya mwisho, hija ya kuaga. Sura hii matika mashafu imewekwa katika sura za Madina kwa sababu imeshuka wakati mtume ameshafanya hijira kwenda madina.


Sura hii inaitwa ya Madina kwa kuwa ilishuka baada ya Mtume kuhama ingawa iliposhuka ilikuwa ni katika Makka wakati Mtume alipokwenda kufanya Haji ya mwisho. Sura hii imekuja kutabiri kifo cha Mtume (s.a.w).


Kutokana na mapokezi ya hadithi sura hii ndiyo sura ya mwisho kushuka katika quran ila sio aya ya mwisho kushuka. Sura hii ilishuka kwenye masiku ya tashriq katika mwezi wa dhul-hija. Baada ya kushuka sura hii Mtume (s.a.w) ndipo akahutubia waumini.


Sura hii tukufu inaashiria kugomboka kwa Makka. Na sababu khasa iliyo pelekea kugomboka Makka ni Maqureshi walipo vunja mkataba wa amani wa Hudaibiya kwa kuwashambulia kabila ya Khuzaa', ambao walikuwa wana masikilizano na Mtume s.a.w., na wakawasaidia Bani Bakri katika hayo. Yalipo tokea hayo Mtume akaona waliyo yafanya Maqureshi kuvunja mapatano imembidi ende kuigomboa Makka. Basi akakusanya jeshi la nguvu lenye wapiganaji elfu kumi. Akenda mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa nane wa Hijra (Desemba mwaka 630 B.K.) Akawazuia watu wake wasipigane ila wakilazimishwa. Na Mwenyezi Mungu alipenda aingie Nabii na jeshi lake Makka bila ya vita. Na kwa hivi akapata ushindi mkubwa kabisa katika taarikhi ya wito wa Kiislamu, bila ya vita. Na Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola ya kwanza duniani bila ya vita na bila ya kumwagwa damu.


Na huo ugombozi wa Makka ulikuwa na athari za kufikia mbali kwa pande za Dini na siyasa, kwani ilikuwa ni kuung'oa upagani, kuabudu masanamu, katika ngome yake kubwa, kwa kuvunjwa masanamu yaliyo simamishwa katika Al-kaaba, na yakaondolewa mapicha na masanamu yaliyo kuwemo.
Na kwa kuingia Makka kwenye boma la Uislamu Nabii s.a.w. aliweza kuzishinda kabila zote zilizo bakia katika Hijazi, ambazo zilizo kuwa zina kani za kijahiliya, kama Hawazan na Thaqif. Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola si juu ya kabila wala nchi bali juu ya Imani, nayo ni Imani ya Kiislamu, na bendera ya Kiislamu


Na Ushindi mkubwa uliotajwa hapa ni ushindi wa Makka ilipoingia katika mamlaka ya Waislamu, mwaka wa 8 wa Hijra, na mwaka uliofuata ikawa makundi-makundi ya makabila ya Waarabu yanakuja ingia Uislamu. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotimiza bishara Zake za ajabu; na Mtume s.a.w. anaambiwa aombe ghofira kwa ajili ya makundi hayo yatakayoingia Uislamu maana kazi ya kusimamisha sheria ilikuwa kubwa. Seyidna Abu Bakar iliposhuka sura hii alilia. Watu wakamwuliza mbona unalia? Akajibu, Kazi ya Mtume s.a.w. sasa imekwisha na Atatutoka.



Sababu za kushuka kwa Surat al-Kawthar
SURATUL-KAUTHAR
Imeteremshwa maka, na sura hii imeshuka kwa sababu al-aAs ibn Waail. Siku mija Mtume (s.a.w) alikuwa anatoka msikitini na akakutana na al-aAs ibn Waail na wakawa wanazungumzwa. Basi walipoachana Al-aAs alipokuwa anaingia msikitini wakamuuliza Maquraish ulikuwa unazungumza na nani, akajibu nilikuwa nazungumza na mtu aliyekatikiwa na kizazi.


Yaani Mtume alifiwa na mtoto wake Abdullah ambaye ndiye mtoto wake wa kiume hivyo hakuna tena wa kumrithi na kuendeleza kizazi chake kwa imani kuwa kizazi kinaendelea kwa watoto wa kiume. na katika mapokezi mengine al-aAs alisema kuwa atakapokufa mtume hakuna mtu atakayemkumbuka maana hatakuwa na kizazi tena. Hivyo Allah ndipo akashusha sura hii.



Sababu za kushuka kwa surat al-Mauun
SURATUL-MAM’UUN
Imeteremshwa Maka, anasimulia Ibn Jurayj kuwa Abuu Sufyan ibn Harb alikuwa na kawaida ya kuchinja ngamia wawili kila wiki, hivyo siku moja yatima mmoja alikuja kwake na kumlilia shida, na hakumsaidia kwa chochote na hatimaye akampiga yatima yule. Hhpa Allah akateremsha surahii.



Sababu za kushushwa kwa surat al-kafirum
SURATUL-KAFIRUN
Imeteremshwa maka na inaelezwa katika sababu za kushuka kwake ni kuwa Kundi la makafiri lilimfuata mtume (s.a.w) na kutoa rai ya kuwa Mtume (s.a.w) ajiunge nao na aabudu miungu yao kwa muda wa mwaka mmoja na wao wataabudu Mola wake kwa muda wa mwaka mmoja. Na kisha ikionekana dini ya mtume (s.a.w) ni bora zaidi wataifuata na kama yao itakuwa ni bora zaidi ataifuata. Allah akalipinga jambo hili na akateremsha sura hii.



Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil
SURAT AL-FIIL
Sura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah. Sura hii imeshuka ili kueleza kuhusu tukio la kuangamizwa kwa jeshi la tembo. Na hii ni katika sura ambazo zinataja neema ambazo wamepewa Maquraysh, nao ni ule ushindi dhidi ya Makafiri walotaka kuvunja Al-Ka’abah. Tukio hili limeelezwa kwa kirefu kwenye vitabu vya Sirah na hapa nitaleta kwa ufupi zaidi


Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Hivyo akaamuwa kujenga kanisa kubwa sana ambalo alifikiri kuwafanya waarabu wasiende Makkah ila waende kuhiji kwenye kanisa lake. Kulikuwa na kijana mmoja kutoka katika kabila la Kinana alifahamu jambo hili la Abraha. Hivyo akaingia kwenye kanisa wakati wa usiku kisha akachafua ukuta wa kanisa kwa kuupaka vinyesi. Abraha alipolijuwa jambo hili akaandaa jeshi kubwa sana ili akaivunje Al-ka’aba. Jeshi la Abraha lilikuwa na washujaa elfu sitini (60,000). kisha akachaguwa tembo aliye mkubwa ndio akampanda yeye. Katika jeshi hili kulikuwa na tembo kati ya tisa mpaka kumi na tatu. (9-13)


Safari ya Abraha iliendelea mpaka akafika sehemu inayoitwa Magmas. Na hapo ndipo akaliweka sawa jeshi lake na akaliweka tayari kwa kuingia Makkah. Akaendelea mpaka akafika sehemu iitwayo Bonde la Muhassar bonde hili lipo kati ya Muzdalifah na Mina. Na hapo ndipo tembo wa abraha akakataa kuendelea na safari. Tembo alipiga magoti na kukaa chini, na kugoma kabisa kuelekea upande wa Makkah. Basi akimuelekeza upande mwingine anakubali lakini pindi akimuelekeza upande wa Makkah anagoma kabisa.


Na hapo ndipo Allah alipoleta jeshi la ndege waliobeba vijiwe vya moto na kuwapiga nvyo jeshi la Abraha. Ndege hawa kila mmoja alibeba vijiwe vitatu, kijiwe kimoja kwenye mdomo na viwili kwenye miguu yao. Kila kijiwe kiliuwa mtu katika jeshi la Abraha. Kuna wengine walikufa palepale na wengine walikimbia na kufia mbele ya safari. Abraha alibahatika kukimbia kwani alijeruhiwa vibaya, alipofika sehemu iitwayo San’a hali yake ikawa mbaya zaidi na akafariki.


Kwa upande mwingine wakazi wa Makkah walikimbia mji na kujificha kwenye majabali. Na huu ni ushauri walopewa na kiongozo wao Abdul Al-Muttalib. Baada ya maombi waloyaomba kwa Allaha na hatimaye wakamuachia Allah ailinde Nymba yake na wao wanusuru maisha yao. Basi jeshi la Abraha baada ya kuangamizwa wakazi wa Makkah wakarudi majumbani kwao wakiwa salama.


Tukio hili lilitokea mwezi wa Muharram siku hamsini aua hamsini na tano kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w) ambapo ni sawa nan Mwezi wa Pili au mwanzoni mwa Mwezi wa Tatu mwaka 571 B.K. na hii ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Allah kwenda kwa mtume wake na watu wa familia yake. Na hapo ndipo Nyumba ya Allah yaani Al-ka’aba ilipata maarufu kwa utukufu wake. Na mwaka huu waarabu wakauita mwaka wa Tembo



ITAENDELEA…….






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1800


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Maswali yanayohusu quran
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Tafsiri na mafunzo ya sura zilizochaguliwa - Saratul-fiyl
Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

quran na tajwid
TAJWID Utangulizi wa elimu ya Tajwid YALIYOMO SURA YA 01 . Soma Zaidi...

Qur-an Kushuka Kidogo Kidogo kwa Kipindi cha Miaka 23:
Soma Zaidi...

QURAN: TAJWID, FADHIKA ZA KUSOMA QURAN, FADHILA ZA KUSIKILIZA QURAN, FAIDA ZA SURAT FATIHA, YASIN, BAQARA, TABARAK
Soma Zaidi...

Sifa za waumini katika quran
Soma Zaidi...

Ni nini maana ya id-gham katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake. Soma Zaidi...

quran na sayansi
2; mbegu ya uhai uliyo changanyikaUmbile la mwanadamu limepitia hatua nyingi sana kama tutakavyoendelea mbele kuonalakini ukiachilia mbali na hatua zote alizopitia mwanadamu wakati wa kuumbwa lakiniumbile la mwanadamu bado limebakia kuwa dhalili kama ALLA Soma Zaidi...

Dai kuwa Muhammad Alitunga Qur-an ili Ajinufaishe Kiuchumi
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al-Falaq na surat an-Nas na fadhila za kusoma sura hizi
SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS) Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s. Soma Zaidi...

Kulaaniwa Bani Israil
Pamoja na kuteuliwa na Allah(s. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat al qariah
Surat Al qariah, ni moja katika sura zilizochuka miaka ya mwanzoni mwa utume. Soma Zaidi...